Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

yani mechi ilivyoanza na mvua ikaanza ya magol

nilikua naona man u inacheza kama timu iliyochoka, kutata tamaa na inaonewa, mara ya mwisho kujiskia hivi ilikua kipindi moyes ni kocha
 
Huyu jamaa naomba kuuliza anaung'ang'ania nini ukocha/umeneja,
amepewa kandarasi ya miaka mitatu mwanzoni mwa msimu huu, kabla ya hapo kumbuka huu ndio ulikuwa msimu wake wa mwisho kuitumikia klabu kwa mujibu wa mkataba wake wa mwanzoni (nafikiri alipewa mkataba wa miaka mitatu na nusu).

sina uelewa mkubwa sana wa masuala ya mikataba ila akili yangu inanilazimisha niamini ya kwamba endapo Ole ataamua kung'atuka mwenyewe bila ya shinikizo la klabu hatoambulia chochote (fidia ya mkataba wake).

tukiachana na maswala ya mkataba ni ukweli uliodhahiri ndani ya manchester united alikuwa na muda mzuri sana wa kujijenga professional kwenye career yake ya ufundishaji kifalsafa na vision kuliko huko alikotokea (molde, cardiff), yupo kwenye timu inayompa kila kitu anachokihitaji kuanzia bajeti ya usajili, miundombinu bora ya ufundisha na still ameshindwa kudeliver matokeo bora na soka bora ndani ya uwanja licha ya uzoefu aliokuwa nao.

kwa sasa ana miaka 48 na bado hajajijengea heshima inayostahili itakayozifanya timu nyenginezo washawishike kuhitaji huduma yake pindi atakapoondoka united, kwa tafsiri ya haraka kama atashindwa man utd huenda itakuwa ndio mwisho wa career yake ya ukufunzi, ni nani atakayemuhitaji pale pale ulaya kuu(german,england, france, spain).

Ole ni tofauti na mourinho, bwana jose husubiria kwanza mamilioni ya pesa yake yatakayopatikana baada ya kuvunjwa kwa mkataba wake.
Bwana ole anayapigania maisha yake ya baadae pamoja na fedha yake aliyozawadiwa kijinga na ed woodward mwanzoni mwa msimu.

je kama ni wewe utachukua uamuzi wa kung'atuka?
 
amepewa kandarasi ya miaka mitatu mwanzoni mwa msimu huu, kabla ya hapo kumbuka huu ndio ulikuwa msimu wake wa mwisho kuitumikia klabu kwa mujibu wa mkataba wake wa mwanzoni (nafikiri alipewa mkataba wa miaka mitatu na nusu).

sina uelewa mkubwa sana wa masuala ya mikataba ila akili yangu inanilazimisha niamini ya kwamba endapo Ole ataamua kung'atuka mwenyewe bila ya shinikizo la klabu hatoambulia chochote (fidia ya mkataba wake).

tukiachana na maswala ya mkataba ni ukweli uliodhahiri ndani ya manchester united alikuwa na muda mzuri sana wa kujijenga professional kwenye career yake ya ufundishaji kifalsafa na vision kuliko huko alikotokea (molde, cardiff), yupo kwenye timu inayompa kila kitu anachokihitaji kuanzia bajeti ya usajili, miundombinu bora ya ufundisha na still ameshindwa kudeliver matokeo bora na soka bora ndani ya uwanja licha ya uzoefu aliokuwa nao.

kwa sasa ana miaka 48 na bado hajajijengea heshima inayostahili itakayozifanya timu nyenginezo washawishike kuhitaji huduma yake pindi atakapoondoka united, kwa tafsiri ya haraka kama atashindwa man utd huenda itakuwa ndio mwisho wa career yake ya ukufunzi, ni nani atakayemuhitaji pale pale ulaya kuu(german,england, france, spain).
Germany ndiyo haiwezekani kabisa hana uwezo wa kuaminiwa na wajerumani
 
Germany ndiyo haiwezekani kabisa hana uwezo wa kuaminiwa na wajerumani
  1. atachukua likizo then atarudi kufundisha timu za nyumbani kwao,
  2. ooohhhh!! kumbe mtoto wake wa kike anacheza manchester united ya wanawake pale academy, nafikiri pia atafikiria kuigeukia kazi ya uchambuzi wa soka (ni kazi rahisi sana hata scholes na ukimya wake anaiweza bila ya kujali anachokizungumza) ili awe karibu na familia yake
 
Kwa tulipofika mi pia nimenyoosha mikono mkuu, I hope tu kuna succession plan na sio kukurupuka.
hatuna succession plan ndio maana klabu bado inamuona Ole ni mtu sahihi.
si conte wala zidane atakayeridhia mwenendo wa uwendeshwaji wa klabu kama afanyavyo Ole,
kama bodi itamuhitaji yes man nafikiri graham potter anaweza kuwa chaguo sahihi kwao.
au hata steve bruce
😀😀😀😀
 
Tatizo man u na arsenal mabosi wao ni wafanyabiashara hawako tayari kuvunja mikataba na kupoteza mabilioni ya paundi na wakati huo walishatoa mapesa mengi ya usajili bila mafanikio hao jamaa wako kibiashara zaidi hawana uchungu na timu kama abromovic boss wa Chelsea yule jamaa anaipenda Chelsea haswa ikifungwa unaona anaumia kabisa ndio maana haangalii hasara yeye anaipenda furaha na kwa staili hii naona kabisa Chelsea watawatesa sana nyie manyumbu na arsenal
 
waheshimiwa acheni kumsagia kunguni baby face, sisi bado twamuamini
1635162130097.png
 
1635162225614.png

antonio conte na sajili zake, mara anakuletea victor moses, matteo darmian, arturo vidal.
lakini atawageuza watumishi halali, akiondoka tu wanakuwa vimeo
na ule mzuka wake itabidi ajengewe nguzo maalumu kwenye jukwaa lake
teh teh teh
======================
bangi za mchana
  1. eric bailly + victor lindelof + raphael varane/ maguire
  2. wan bissaka/ dalot + nemanja matic / fred + paul pogba/ van de beek + luke shaw
  3. rashford/ greenwood + bruno / pogba + ronaldo
 
mwenyewe anasema anakaribia kuifikia nchi ya ahadi,
jana alitaka kutuonyesha pressing yake.
siku ya Ijumaa alisema hatutawapa nafasi liverpool kama ilivyokuwa kwa atalanta
Hahaha jana tulifungwa kwa aibu sana.

Watu wanapiga pasi mpaka anabaki yeye na golikipa.
 
hatuna succession plan ndio maana klabu bado inamuona Ole ni mtu sahihi.
si conte wala zidane atakayeridhia mwenendo wa uwendeshwaji wa klabu kama afanyavyo Ole,
kama bodi itamuhitaji yes man nafikiri graham potter anaweza kuwa chaguo sahihi kwao.
au hata steve bruce
😀😀😀😀
Mimi naona Eric Ten Hag ni modern coach anayecheza kwa ujasiri sana kuliko Conte na Zidane
 
Nawasalimu kwa jina la kaputeni MANGWA,msifukuze kocha sasa ivi mapema sana ,gemu yenu na chelsea ikiisha fukuzeni ,msiwe wachoyo mmegawa kwa Leceister ,liverpool ,mtugawie chelsea kisha fanyeni mtakavyo ona ,vijana wa kaputeni MAGWA na OLETUKURU
Salam tumezipokea
JamiiForums1548956822.jpg
 
Back
Top Bottom