Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hongera sanaaaaaaa Evra.
PSX_20210925_134805.jpg
 
Najaribu kufanya stress testing ktk kikosi chetu, Je Ole ana mbinu mbadala ya kucheza bila Ronaldo, Bruno, Pogba na Greenwood endapo watapata majereha au kadi nyekundu?

Ule mchezo wa juzi dhidi ya Westham umeonyesha waziwazi jinsi kikosi B kinavyocheza ni sawa sawa na jinsi kikosi A kinavyocheza utofauti wake ni kikosi A kina wachezaji wanaoweza kuamua mchezo wenyewe kwa uwezo wao.

Hofu yangu ni kwamba huwezi kushinda kombe kama timu haiwezi kupata ushindi bila key players. Ole tunapoteza muda, watu wanaomtetea naamini tutaongea lugha moja siku si nyingi sana.

Kwahiyo unashauri nani awe mbadala wa Ole?
 
NYUMA YA PAZIA: Sir Alex alituonya kwa Pogba na bwana Kibonge INAKERA sana. Sidhani kama ametuonyesha heshima yoyote ile kama nikiamua kusema kweli. Nina furaha kwamba kama wanasoka wakiendelea kufanya hivi ni bora wasifanyie mambo haya kwetu,” alisema Sir Alex Ferguson huku sura yake ikiwa nyekundu akiwaka kwa hasira kali mbele ya vyombo vya habari.

Ni miezi 132 sasa imepita. Ilikuwa mnamo Julai 2012 wakati Sir Alex alipokuwa akimshutumu kinda Paul Pogba kwamba alikuwa amesaini Juventus muda mrefu uliopita ingawa yeye na wakala wake, Mino Raiola walikuwa wamemficha na walikuwa wanajifanya wapo katika mazungumzo ya mkataba mpya na Manchester United.

Sir Alex alikuwa ameshtukia dili. Kilichobaki kilikuwa historia. Pogba alisaini Juventus Turin. Akageuka kuwa staa mkubwa. Baadaye akarudi Old Trafford kwa pesa nyingi. Mpaka leo sijajua kama Sir Alex aliridhika kuona Jose Mourinho na mabosi wake wakivunja rekodi ya uhamisho wa dunia 2016 kumrudisha Pogba, Old Trafford. Na kama Sir Alex alitabiri kwamba wachezaji wenye tabia kama za Pogba wakae mbali na Old Trafford na bado hakusikilizwa, basi huenda jinamizi la Pogba limerudi tena Old Trafford. Miaka kumi na ushee sasa hivi na United imejikuta katika mtego uleule. Tuliambiwa tusikilize wazee. Paul Labile Pogba mpaka sasa hajasaini mkataba mpya Manchester United. Mkataba wake unakaribia kumalizika mwishoni mwa msimu. Jana nilikuwa nasoma mahala kwamba Manchester United wameweka mezani mshahara wa Pauni 400,000 kwa wiki. Utamfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi Ligi Kuu ya England.

Swali ni je atasaini? Bado sijaamini. Nyuma yake ana mtu fulani hivi kibonge mpenda pesa anayeishi Monaco katika jumba la kifahari akitengeneza noti kwa vurugu kupitia dili kama hizi. Mino Raiola. Sina uhakika Raiola anawaza nini.

Wakati Pogba akiondoka 2012, ilidaiwa kwamba alikuwa amechoka kusubiri kumuona Paul Scholes akizeeka. Alidai kwamba alikuwa anaondoka kwa sababu za kisoka. Kumbuka kwamba aliondoka bure licha ya United kumkomaza.

Nadhani Raiola aliichungulia pesa mbele ya safari. Alikiangalia kipaji cha Pogba, akamnong’oneza asisaini mkataba mpya. Nadhani walitengewa kitita na Juventus. Akasaini bure Juventus. Baadaye akageuka kuwa staa mkubwa.

Kwa sasa sijui Raiola ana mawazo gani. Amefanikiwa kukaribia kuifikisha United kule ambako aliifikisha 2012. Kuwa na bidhaa adimu isiyo na mkataba. Kuna uwezekano mkubwa Pogba asisaini mkataba na United kisha akaondoka bure msimu ujao. Mpaka sasa Raiola anachukiwa pale Milan. Ametoka kufanikisha dili la uhamisho wa bure kwa mteja wake Gigi Donnarumma mwenye miaka 22 tu. Milan imemlea vilivyo lakini Raiola kafanikiwa kumshawishi asisaini mkataba mpya mpaka ameenda bure PSG.

Swali kwa Pogba ni je, kuna uwezekano akiondoka bure akalipwa Pauni 500,000 kwa wiki mahala? Inawezekana. Pogba ni mchezaji mkubwa. Manchester United watakubali aondoke bure mwakani akiwa na umri wa miaka 29? Ni swali linalofikirisha. Vipi kama Pogba alikataa dau lao la Pauni 400,000 kwa wiki? Vyovyote ilivyo Mino Raiola ametulia tu. Ana bahati kwamba ana kila sababu ya kutulia. Pogba ameishia pazuri. Aliuwasha moto katika michuano ya Euro kiasi kwamba United wametamani kuendelea kuwa naye hata kama kuna watu ambao mioyo yao imegawanyika.

Lakini pia ametengeneza kombinesheni nzuri na Bruno Fernandes. Alikuwa na msimu mzuri wakati akiipeleka Manchester United katika Top Four na kuifikisha katika fainali za Europa ambapo walifungwa na Villarreal ya Hispania. Hapa anaigawanya mioyo ya United.

Kuna kina Roy Keane na waandamizi wengine wa United wamekuwa wakimpa presha Ole Gunnar Solskjaer aachane na Pogba. Lakini unapokumbuka mambo aliyofanya Euro unajiuliza mara mbilimbili ni wapi unaweza kumpata Pogba mwingine kirahisi katika dunia ya leo. Yote haya Raiola na Pogba hawajali. Wameiweka United katika kona ambayo Sir Alex aliwahi kuionya kuhusu aina ya wachezaji kama Pogba. Kwa sasa hata United ikiamua kumuuza Pogba haiwezi kuwa na nyodo kwa sababu upande wa kina Pogba ndio umeshika mpini. United wameshika makali. Na hakuna kitu ambacho kina Keane watachukia kama kumuona Pogba akiondoka na kitita cha Pauni 400,000 kwa wiki katika mkataba mwingine wa miaka minne au mitano ambao amewekewa mezani kwa sasa. Kina Keane watang’ata meno kwa hasira kali. Hii inatokana na ukweli kwamba licha ya Pogba kuwaweka United katika kona nzuri kwa sasa, lakini kuna wakati anaudhi. Kuna wakati fomu yake inapotea na mara nyingi anajikuta akibadilisha staili ya nywele zaidi kuliko kufunga mabao.

Timu pekee ambayo inaweza kumchukua Pogba kwa sasa ni PSG. Wale mapacha wa Hispania, Real Madrid na Barcelona hawana kitu. Ni PSG tu ndio ambayo inaweza kumrudisha nyumbani Pogba. Iwe kwa dirisha hili au kumchukua bure msimu ujao. Katika dirisha hili PSG imechukua wachezaji wengi wa bure. Kwa hiyo haitashangaza wakikwepa kuvunja kanuni za masuala ya matumizi ya pesa za Uefa hata kama wakimchukua Pogba. Kina Lionel Messi, Donnarumma na Sergio Ramos wote wamekwenda bure Paris. Watu wengine ambao wangeweza kumchukua Pogba ni Manchester City, lakini sioni uwezekano huo. Pep Guardiola hana uhusiano mzuri na Raiola. Lakini hapohapo City wana Kelvin De Bruyne. Wana Ilkay Gundogan. Hawana shida na Pogba.
 
Viungo wetu wakabaji wanapoteza sana mipira pindi wakiwa nayo na wanatumia nguvu nyingi sana kutafuta mpira huohuo walioupoteza.....
 
First half, tukubali Wan Bissaka kaupiga asee sikutegemea penetration passes kama zile ukiwa umezungukwa na watu. Improvement kidogo ipongezwe.


Hili suala la Pogba kukaa namba asiyoijua huku Sancho tuliyekuwa tunamlilia yupo linakera.

Kakocha Ovyo, nimeamini kuna wachezaji hataki kuwaudhi, ukute anataka Van De Beek acheze ila hataki kuwaudhi Fred, tommy, matic, pogba.

Na Martial asee ana mkanda wa Sosha sio bure.
 
Shaw was poor..bora ametoka

Bissaka+Fred trash as usual.

Maguire...Shamble again..kila mechi lazima atoe blunder..captain gani huyu?

Anyway..we better win the 2nd half.
 
Kalilia no 7 kapewa anamuweka benchi ukweli ole hajui kutumia wachezaji wengi alionao kuanzia middle almost wote wanacheza nje ya positions zao.
 
Back
Top Bottom