Ndiyo maana nasema kama unafuatilia mpira kuna vitu ukiuliza vinafanya ujifafanue wewe ni wa aina gani.
Ni kawaida timu ikipata kocha mpya au mchezaji mpya kuperform. Baada ya muda inarudi katika level yake, ole alivyofika united ilikua hivyo, lampard alivyofika chelsea ikawa hivyo, emery alivyofika Arsenal ikawa hivyo, James Rodrguez na Carlo walivyofika Everton ikawa hivyo the list goes on and on.
Watu wakisema kocha fulani hafai hii inamaanisha wanaona kocha yupo kwenye timu yenye facilities wezeshi, kikosi kizuri na financially strong ila hafikii lengo. Mfano Ole amekua akipoteza nusu fainali mara nyingi mpaka imekua signature yake.
Hapo ni ukilinganisha na timu zingine unaona hizo timu zingine zina kikosi cha kawaida ila kocha ana mbinu za kukabiliana na wapinzani. Mfano Lyon imechukua kombe mbele ya psg, hapo tunaona kwamba kocha wa lyon (ingawa kahama) ni trophy oriented na anafaa, Conte amechukua scudetto na Inter ambayo mastar walikua forwards Lukaku na Martinez, wengine ni wa kawaida.
Conte alikataa kazi ya Spurs kwakua spurs walisema hawana mpango wa trophy hivi karibuni. Kuna wakina Erik Ten Hag, the list goes on. Hii inamaanisha kuna baadhi ya makocha wakikabidhiwa kikosi cha united na full support ya bodi kuna matokeo zaidi ya sasa yanaweza kupatikana.
Kocha wa kawaida ni wa kawaida tu. Muangalie Pochettino anavyostruggle na PSG yenye mastar kuanzia chini mpaka juu na huku yupo farmers league.
So wewe ukiuliza aje kocha gani mi nachukulia haufuatilii mpira ila hua unaangalia mechi. Pamoja na yote hayo, jana Ole ilibidi afanye rotation isipokua amechelewesha sub (tatizo lake kuu) pia mimi sishabikii united.