kuna watu wanataka tucheze kama liverpool au man city, wengine wanataka tubane space kati ya mstari wa beki, midfield na attacking kama timu nyenginezo kwa sababu ya kucheza kwetu na higher line tokea aje varane.
wengine tunalalamikia pressing yetu, wengine tunalalamikia jinsi tunavyolinda kuanzia chini na si juu n.k
ifikie hatua tukubaliane hilo haliwezekani kwa mwalimu aliyekuwepo, tuendelee tu kuziangalia hizi mechi zetu (tukishinda tufurahe na tukiharibu tuje tumtukane mwalimu kama kawaida yetu), makocha wa ulaya ni wagumu sana kubadilika kifikra (angelianza mourinho) kwa sababu kila kocha anaamini njia yake ndio sahihi
kwa jicho la kawaida nilioyaona (tactics watafute wataalamu waliobobea hapa nilipo nasubiria thread ya eric laurie na wengineo), muda mwingi jana tulikuwa tunacheza 2-4-4(impact ya varane)
- nafasi ya cavani ndio imeshamezwa na uwepo wa CR7, njia pekee ya kuepusha hilo either ni kucheza 4-4-2 kama nyakati zile za Fergie jambo ambalo ni ngumu kuwezekana, lazima umuondoe bruno ambaye anacheza kama second striker au umpeleke ronaldo mwenye miaka 36 pembeni na kufanya hivyo itakulazimu utoe sadaka wachezaji wengineo muhimu (mlengwa zaidi ni greenwood).
- rashford atarudi mwezi Oktoba au November, hatorudi kama nyota kama ilivyokuwa zamani bali atarudi kugombania namba
- kwa jinsi nilivyomuona sancho hapo jana amenipa matumaini ya kutupa kile tunachokihjitaji kutoka kwake ndani ya muda mfupi ujao (tuwe wavumilivu atalia mtu, dogo kumbe anasumbua kama coman)
- mchezaji rahisi wa kumtoa kafara bila ya kuangalia mchango wake ni mason greenwood, ngoja tusubirie hiyo vita ya kugombania nafasi kwa sababu simuoni greenwood akipunguza moto wake (cut inside, weka sawa mpira piga shuti)
- double pivot (mcfred) imezikwa rasmi kwa sababu sioni njia ya kumweka nje paul pogba, kwanza tuna tatizo la kimkataba dhidi yake hivyo tunahitaji kumtengenezea mazingira bora ya kiushawishi, pia ni ngumu kumchezesha upande wa kushoto kwa sababu ya uwepo wa mchezaji ghali anayeitwa sancho na pia lingard anaishambulia space vizuri. Je tunaweza kumweka nje pogba kwa ajili ya mcfred kwa mechi tatu mfululizo?......labda wakala wake awe amekufa
- wan bissaka atatuchelewesha japokuwa ni bora sana kwa kuholding his width (going forwards and creativity namtamani sana mfano wa alexander arnold ndani OT)
- mara nyingi tunapo pokonywa mpira tunakuwa vulnerable, huwa tunabaki wawili au watatu nyuma na hili tatizo tusipolifanyia kazi tutakuja kufungwa 3 (wolves walitusamehe, newcastle nao hivyo hivyo), hapo ndipo unapouona umuhimu wa mwanadamu mfano wa kante (anacover space kubwa na kwa haraka), tusije tukafanya ujinga huu dhidi ya liverpool yenye salah na jota
- mwili wa matic hauwezi mikiki ya dakika 90 especilly covering large space kama fred ila miguu yake haijachoka kupiga pasi zinazovuka mstari wa adui, most prograssive passing kwa mechi ya jana, scott na fred wana mengi ya kujifunza kutoka kwake, kwa timu zinakaa nyuma matic ndiye solution ila ukicheza na wahuni wanaotembe sana matic atakuchukiza
- ubingwa wa ligi utaamuliwa na matumizi ya uwanja wa ugenini kwa kila timu, kwa vurugu zile za mashabiki ndani ya old trafford, anfield, etihad, stamford bridge takribani timu zote ndogo zitaadhibiwa
- tukiwafunga west ham nyumbani kwao kwa ushindi safi basi kila timu ndogo itaingiwa na khofu