D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,633
- 121,022
hii timu ya wanawake familia ya glazer inaelekea kuwashinda, nafikiri huyo atakuwa mchezaji wanne kuondoka, wiki mbili zilizopita nilikutana na taarifa inayowahusu wachezaji wa hiyo timu wamepanga kwenda kutafuta ushauri kwa chama cha wachezaji wa kulipwa juu ya mustakabali wao kwani mpaka sasa hajajulikana kocha mpyaLauren James ameachana na kikosi cha Casey Stone na sasa atajiunga na Club ya Chelsea anayocheza kaka yake Reece James.
Alikuwa ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Casey Stone lakini hakuna jinsi Chelsea wamefanikiwa kumshawishi kujiunga nao.
==========
nimeshangazwa na gharama za usajili wake, hawa wachezaji wa kike bado wanapatikana kwa bei ya kawaida sana.
amenunuliwa kwa rekodi ya paundi laki 2 itakayoongezeka mpaka kufikia laki 3.
huo ni mshahara wa david de gea
