Safari ya Ole Gunnar Solskjaer ndani ya manchester united (3)
msimu mpya, usajili na mfumo mpya
msimu wa 2019/2020 tulishuhudia kwanza mabadiliko rasmi ya kimfumo kutoka ule alioanza nao akiwa caretaker (4-3-3) hadi kuelekea 4-2-31 akiwa kama kocha mkuu na tukumbuke mfumo ulichukua takribani miezi mitatu hadi kuanza kutumiwa rasmi.
tulianza msimu mpya huku tukiongozwa na maswali mengi yaliokosa majibu rasmi kwa nyakati zile.
wachezaji wapya wataleta impact gani ndani ya kikosi (james, bissaka, maguire)?
ilikuwa ni sahihi kumuondoa ander herrera bila ya mrithi wake kutafutwa huku tukiwaamini zaidi waliopo?
ilikuwa ni sahihi kumundoa romelu lukaku kwa kumtegemea martial kama ni false 9?
je ni lini tutatatua tatizo la winga wa kulia au ndio usajili wa james ndio muokozi wa eneo hilo kutoka Championship?
ni yupi mchezaji wetu wa kutegemewa?
pia nakumbuka nyakati zile za maandalizi ya msimu mpya humu ndani mijadala inayohusu mustakabali wa timu iliendelea mara kwa mara, kupitia matokeo ya mechi za pre season baadhi yao waliamini timu imebadilika na wengineo waliamini bado tupo vile vile kama tulivyomalizia msimu. Nimeikumbuka kauli yangu kabla ya ligi kuanza msimu ule
"mashabiki wa man utd tuache kujificha kwenye kivuli cha mchicha tukiamini hatutoathiriwa na mvua"
dhumuni kuu la usajili linaendelea kuwa ni lile lile la kuimarisha kwanza safu ya ulinzi ilioruhusu magoli takribani 54 kwa mechi 38, kutengeneza safu ya ushambuliaji itakayoongozwa na wachezaji vijana wenye ari ya kupata mafanikio huku lengo kuu ni kuzigeuza zile mechi tulizotoa suluhu au kufungwa kuwa ni ushindi utakaotokanwa na uimara wa safu ya ulinzi iliiongezewa mabeki wawili wa gharama kubwa kwa pamoja (paundi millioni 140).
herrera aondoka na 4-3-3,
kuondoka kwa herrera na kushindwa kuletwa mchezaji mbadala wake ulileta tafsiri ya kwamba yule paul pogba aliyepewa uhuru wa kucheza kushoto na Ole sasa anarudi rasmi katika hali yake ya mwanzoni (mfumo wa viungo wawili wa mourinho). Kutokana na performance mbovu ya fred kwa msimu wa mwanzo wa ligi hapakuwepo na mchezaji mwengine mwenye uwezo wa kudeliver performance mfano wa ile tulioishuhudia kwa ander herrera kwa wachezaji waliokuwepo (fred, mctominay, perreira)
mabadiliko ya mfumo na uwepo wa martial na rashford
Ole alijenga timu kwa kuwaangalia zaidi wanadamu hawa ambao msimu uliomalizika walishatuonyesha kwa mara nyengine tena ile sura yao ya kukosa makali ya kudumu (consistency).
martial alifunga magoli 4 ndani ya miezi sita ya mwanzo ya Ole (naruhusu masahihisho)
rashford alianza kwa kufunga magoli 6 ndani ya mechi 9 za mwanzo za ole, mwishoni mwa msimu rashford alimaliza na goli moja tu ukiachana na lile alilofunga dhidi ya psg kwa njia ya penalty (naruhusu masahihisho)
Ole alisahau yote hayo badala ya kumalizika kwa msimu na hatimaye akaamua kuulisha ubongo wake mawazo hasi tu juu ya wachezaji hao wawili (alijisemea moyoni hawa ndio watakaonifikisha nchi ya ahadi).
faida moja kubwa ya martial ni ubora wake wa kufunga pindi anapokuwa karibu na goli ila anakuwa useless akiwa nje ya box, hivyo basi ilihitajika plan itakayomfanya martial awe anakimbia kuelekea golini mara kwa mara
ligi inaanza rasmi, ushindi mkubwa dhidi ya chelsea, matic na sintofahamu yake
mechi nne za mwanzo Ole alimtumia paul pogba namba 8 pamoja na scott mctominay nafasi ambayo ulikuwepo uwezekano wa kumtumia nemanja matic then paul pogba acheze namba 10 au juan mata, kinyume chake alikuwa anamtumia andreas perreira au jesse lingard kwa takribani miezi minne ya mwanzoni.
licha ya paul pogba kucheza chini zaidi bado aliendelea kuwa muhudumu bora kwa safu ya ushambuliaji kwa kutumia ufundi wake wa kupiga pasi ndefu, jambo lililokuwa likisaidia washambuliaji wetu wawili kuweza kukimbia kutoka nyuma ya nafasi ilioachwa wazi na adui na mfumo huu ulitusaidia sana kwenye mechi dhidi ya chelsea tulipopata ushindi wa magoli 4.
majeruhi yaanza tena, je ole alijifunza ya msimu uliopita?
mkakati huu wa kumdeploy pogba ulifanya kazi kwa kiasi kikubwa sana mpaka pale martial na paul pogba walipopata majeruhi na hatimaye rashford akarudi eneo la ushambuliaji. Majeruhi ya paul pogba yaliodumu kwa takribani majuma sita tofauti yalipelekea timu ikose creativity ndio maana si ajabu ilifikia hatua timu ilifunga magoli mawili.
twende na counterattacks
kutokana na ufinyu wa wachezaji wenye ubora si vibaya kama nitasema wachezaji wa manchester united wa kikosi cha kwanza walikuwa wakijichagua wenyewe ukiachana na baadhi ya maeneo kama vile beki tatu na namba 10 yaliokuwa na wagombeaji wengi wa nafasi.
Ole alishape timu kuelekea 4-2-3-1 ambapo tulishuhudia martial akiwa ndiye false 9, huku rashford na daniel james wakishuka chini zaidi kupitia pembeni ili kutengeneza space ya kukimbia.
Kupitia mfumo huu tulishuhudia marcus rashford akifunga magoli 11 kutoka oktoba hadi january (magoli 8 ni open play),
kwa upande wa daniel james kwa kutumia zaidi mbio zake tulishuhudia akiwa ni creators zaidi ya ufungaji japokuwa tulishuhudia mwanzoni mwa msimu alifunga magoli matatu ndani ya mechi 4, kutoka oktoba hadi January alifanikiwa kutengeneza assist 6 ndani ya mechi 11.
kipi kitatokezea unapocheza na wajanja zaidi yako
kupitia mfumo huu mmoja wa kiuchezaji baadae ulipelekea wingu zito kwa upande wa timu ya manchester united, timu nyingi ziliamua kuja na mfumo wa kukaa chini zaidi (low blocks) kwa kucover space behind.
kwa kuwa man utd imekosa creativity hususani kwa midfields (lingard, perreira, fred, scott) wenye profiles bora kwenye eneo la upigaji wa pasi through the lines na kutengeneza movements (mpaka sasa tatizo hili lipo) mwenendo wa manchester united ukaendelea kuwa ni mbovu.
baada ya kumaliza mechi ya chelsea, mchambuzi wa sky sports anayeitwa jose mourinho alisema
I think United will find it much more difficult to play against teams with low compact blocks, if the block is low blocks, it will be really difficult for them without pure striker"
kilichotokezea kwa baadhi ya mechi dhidi ya low blocks mpaka september.
wolverhampton 1 vs man utd 1
man utd 1 vs crystal palace 2
southampton 1 vs man utd 1
man utd 1(penalty) vs leicester city 0
man utd 1 vs astana 0
westham 2 vs man utd 0.
je tatizo la ukosefu wa creativity ole alitatuweje na dirisha limekaribia?
============================
itaendelea Insha'allah