Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mimi binafsi kufungwa kwa chama langu nimefurahi sana. Kwa sababu naona kuna faida kadhaa tutapata kabla dirisha la usajili halijafungwa. Ya kwanza tutasajili wachezaji siyo chini ya mmoja, sancho uhakika. Vilevile naona jinsi martial na rashford watakavyotengenezewa competition mulemule, ataanza martial then rashford sub and vice versa is true, kitu ambacho ole na benchi lake la ufundi, lazima wamekiona. Mwisho ole nimwonavyo ni mnafki mwenye faida upande mwingine, ile timu imecheza kiboya vile usikute waliambiwa na kocha na benchi la ufundi, maana bila hivyo hakuna njia nyingine ya kuwashawishi board ya man utd, maana ni vichaa wale(kumbuka waliwahi muambia mourinho kuhusu kutokubaliana na hoja ya kumuuza martial kwa sababu wanamuona kama nacmento pele). Hayo ni mawazo yangu.
Nadhani sasa mmeona rashford na martial wameanza kutengenezewa mazingira ya kupigania namba, the rebuilding takes the progress, tutakuja kuwa tishio baadae.
 
Wakati mwingine mwalimu wetu anafail sana kwenye management ya kikosi chetu yawezekana tuna wachezaji wa kufunika mapungufu yetu lakini mwalimu hajajua awatumie vipi.

Mfano alifanya kosa kumuondoa Diogo Dalot ambaye alitosha kabisa kuwa mbadala wa winger wa kulia.

Sasa hivi timu yetu haina hata uwezo wa kumiliki mpira walau dakika moja uwanjani haijalishi tuko eneo lipi la uwanja hii inatufanya tuwe vulnerable muda wote wa mchezo.

Rashford na Martial wanapaswa wacheze wing ya kushoto Greenwood na Cavan wacheze hiyo centre forward lakini mwalimu bado anaamini wale wehu wake wawili wanafaa kucheza hiyo central role.

Sidhani kama Pogba ataondoka inaelekea Ole kashamlainisha hivyo anaweza kuongeza mkataba tena.

Ni heri tuwaondoe Matic na Juan Mata tutafute wachezaji watakaokuja kuwa mbadala wa kina Scot na Fred au mbadala wa kina Donny na Bruno tunapohitaji a new dimension uwanjani.

Sioni sababu ya kuendelea kumtunza Juan Mata anayecheza mechi tatu kwa msimu.
Kumuuza Diogo Dalot na kuanza kumuwania Max Arons kunaweka doa kwenye benchi la ufundi. Hakuna tofauti na kuuza Lukaku kisha kuanza kuhangaika na akina Ighalo na Cavani.
 
Nasikia kwenye mkataba mmeweka kipengele cha kuto nunuliwa huko westham ,mlijua kama atakiwasha hahaaaaaa
...!

United haiwezi Fanya biashara na city kwa sawa ...

Sema united haijui inataka nin Lingardinyo anaenda westham anatupia magoli ila united mlikuwa mnamuona useless ...

Yupo kwenye timu ya level yake ww ndio umeshindwa kutambua hana cha kupoteza kule wala pressure
 
Kwa mwenendo huu wa Rashford pamoja na mwenzake Martial,nadhani ni wakati muafaka wa kuirudisha mezani hoja ya uwezo sahihi wa hao madogo wawili kama kweli wanaweza kutubeba msimu ujao au tunaendelea kucheza kamari na kumuachia Pep atuadhilishe atakavyo.

Ningependa kuona madhaifu ya mwalimu yanafichwa na ubora wa wachezaji wake kama alivyofanya Zidane na Madrid yake kabla CR7 hajawa historia pale bernabeu,lakini mapenzi ya Ole kwa hawa vijana ndio yatamfukuzisha pale OT.
 
ujio wa winga mpya wa kulia mfano wa sancho utakuwa na maana gani kwa amad diallo?

nafikiri usajili wa donny ulitokanwa zaidi na urahisi wake, klabu ina mahusiano mazuri sana na CEO wa ajax bwana edwin van der sar jambo ambalo lilileta urahisi sana wa kimazungumzo ya kibiashara kati ya pande mbili, halafu thamani yake ilikuwa ni nusu ya gharama za usajili wa jack grealish.

changamoto ninayoiona mimi inatokanwa zaidi na mwalimu mwenyewe kushindwa kutengeneza mfumo utakaowanufaisha wachezaji wetu wote muhimu pindi wanapokuwa wazima (pogba, bruno, donny), solution ninayoiona mimi ni mfumo ule ule wa diamond lakini hilo litawezekana zaidi kama midfield wetu wanaolinda defence line watafanya kazi yao ipasavyo bila ya kusahau awe more intelligence, awe na uwezo wa kusoma mchezo kama carrick, awe mtaalamu wa kunusa position mfano wa xavi (yule thiago alcantara kama angelikuwa na takwimu nzuri za kiafya na umri sahihi basi angelipendeza sana).
Mkuu tupe muono wako kwenye kikosi kilicho na pogba pamoja na bruno (haijalishi nafasi wanazocheza) tunapocheza big game hasa kwenye uwiano wa kiulinzi.
 
Mpaka sasa tungekuwa title contender iwapo recruitment department ingekuwa inatatua matatizo sahihi ya United badala ya kufanya patchwork.

Kama walikuwa wameshamsajili Bruno Fernandez hawakuwa na sababu yoyote ya msingi ya kumsajili Donny kwa sababu ni midfielders ambao hawana ball retention capacity wanapocheza, japokuwa Donny na Bruno wote ni wachezaji wazuri na wanatofautiana quality lakini wana weakness inayokaribiana hawatunzi mpira timu inapokuwa nao tatizo hili linakuwa kubwa zaidi ukizingatia pia Fred na Scot hawana uwezo mkubwa wa possession pia.

Mpaka sasa United inahitaji usajili tena wa wachezaji watatu muhimu ili timu iweze kuwa na balance nzuri.

Wing ya kulia, Center back mmoja na Central Midfielder au Holding atakaye complement weakness za Bruno na Donny.

Pogba anaweza kufanya hiyo kazi ya CM lakini anahitaji holding midfielder makini na mpambanaji sawa na Ng'olo Kante, Joshua Kimmich, Goretzeka au Fernandinho.

Center backs wetu kuendelea kuwa pazia msimu huu ni ishara kuwa either hawaendani kiuchezaji au wanauzembe unaofana.

Tuendelee kuupa muda nafasi huenda ukatupa mwanga zaidi juu ya mwelekeo wa timu yetu.

Na striker kwa mfumo wa sosha panahitajika striker pia scott ni mzur shida yake anakaa sana na mipira anataka kumiliki katikati wakat hana uwezo huo fred si mzur kwenye pasi hata kwa scott hivyo hivyo ndio maana timu inahangaika sana ila kwenye kukaba wapo vizur timu inahitaj wapiga pasi za chap kama carick na scholes walivyokuwa
 
Ni heri tuwaondoe Matic na Juan Mata tutafute wachezaji watakaokuja kuwa mbadala wa kina Scot na Fred au mbadala wa kina Donny na Bruno tunapohitaji a new dimension uwanjani.

Sioni sababu ya kuendelea kumtunza Juan Mata anayecheza mechi tatu kwa msimu.
sijaangalia takwimu zinazoangazia mechi alizocheza juan mata kwa hii miaka minne iliopita ila sidhani kama anafikisha mechi 50 alizocheza za ligi kuu. Nafikiri uwepo wa juan mata klabuni unatokanwa zaidi na sababu za kiuongozi kuliko sababu za kiuchezaji. Juan mata anaonekana kuwa ni mwanadamu mwenye taswira ya upole, uvumilivu, aliyeridhika, mpinga fitna(hajawahi kuanzisha mgogoro wowote dhidi ya mwalimu), mwingi wa ihsan na ikhlaq nafsini mwake.

Naweza kusema huu ni msimu wa nne kumshuhudia Juan akikosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza lakini sijawahi kukutana na malalamiko yeyote kutoka kwake kupitia media tofauti ukilinganisha na wachezaji wengineo wenye changamoto inayoshabihiana na ya kwake kwa kuanzia utawala wa mourinho ambaye tuliamini havutiwi na uchezaji wa mata (rejea sakata lake pale chelsea) mpaka huu utawala wa Ole gunnar. Si hivyo tu pia juan amekuwa akichezeshwa nafasi asiyoipendelea kiuchezaji tokea asajiliwe manchester united lakini ameendelea kujitolea kwa moyo wake wote pindi anapopewa nafasi

Nafikiri Ole anamtumia juan mata kama ni mfano kwa wachezaji vijana na hata wale wapya walioshindwa kuingia kwenye mfumo wawe wavumilivu licha ya kukosa dakika nyingi za kucheza, hakuna umuhimu wa kuwatumia mawakala kuleta vitisho vya mikataba na wala hakuna umuhimu wa kuongelea mambo ya klabu kwenye media.

Sitoshangaa endapo juan mata atapewa tena mkataba iwe wa mwaka mmoja au miwili (najua atakubali), nafikiri klabu ina mpango wa kumtumia juan mata siku za mbeleni kuwa ni balozi wa klabu ndio maana wanazidi kumweka karibu.

si hivyo tu pia nimeona vugu vugu kubwa la usajili wa wachezaji vijana kutoka Spain kwa miaka hii ya karibuni kama vile:
  • alvaro fernandez: mlinzi wa kushoto kutoka real madrid na amepandishwa timu ya miaka 23 licha ya kuwa na miaka 17.
  • marc jurado: anatokea barcelona, amezaliwa miaka 16 iliopita
  • armau puigmal: anacheza timu ya miaka 23
  • Mateo Mejia
  • alejandro ganacho: miaka 16 na amesajiliwa kutoka atletico madrid
uwepo wa mata utaweza kuwa ni kichocheo cha kuendeleza huu mkakati wa kusajili vijana kutoka spain, vijana watamchukulia juan kama ni mlezi wao pale Manchester kutokana na uzoefu wake na haiba yake.
 
Sir Ryan Giggs

#GGMU

manutd |
IMG_20210302_234053_399.jpeg
 
Back
Top Bottom