Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Rooney x Evra ★

#GGMU
#PhotoOfTheDay

manutd |
IMG_20210302_233809_814.jpeg
 
★Solskjær: "We’ve had a light training session and we’re looking ok. A couple of doubts for tomorrow, Edinson [Cavani] trained which is good. Let’s hope there’s no reaction and hopefully he’ll travel with the squad."★

#GGMU

manutd |
 
Mkuu tupe muono wako kwenye kikosi kilicho na pogba pamoja na bruno (haijalishi nafasi wanazocheza) tunapocheza big game hasa kwenye uwiano wa kiulinzi.
niwe mkweli sina uelewa wowote wa kuchanganua mfumo wa kiuchezaji wa timu husika kama walivyo wengineo na ndio maana hujitahidi kupita vyanzo tofauti ili kujifunza japo kidogo. hilo swali ungelimuuliza mwanadamu mwenye ujuzi wa kuchanganua mifumo ya kiuchezaji ya timu(tactical analyst) pamoja na data analyst naamini ungelipata jibu sahihi na lenye kuridhisha kiu yako ya kutaka kujifunza.

labda nijaribu kujibu kwa mujibu wa jicho langu jinsi linavyozitazama hizi mechi tunazocheza ila fahamu jicho linadanganya ukilinganisha na data, safu yetu ya ulinzi pekee ina thamani ya takribani paundi millioni 300 lakini cha kustaajabisha mwalimu hana imani na safu hiyo iwe ni mechi kubwa au ndogo, mpaka sasa sijaiona hiyo faida ya kucheza double pivot kwa sababu bado tunaendelea kufungwa mara kwa mara tena magoli yenye kufanana.

unapoingia uwanjani huku ukiwa unaongozwa na fikra za uoga unamfanya adui yako abadilishe mfumo wa kiuchezaji na hicho ndicho kinachotukuta mara kwa mara, hatimaye tunajikuta tunakaribisha presha inayoepukika kwenye halfes space yetu

kuhusu bruno na pogba kucheza pamoja hakuwezi kuathiri safu yetu ya ulinzi kama tutaitumia mifano mengineyo iliyowahi kujitokeza, nakumbuka pale man city walishawahi kucheza kwa muda mrefu na namba 10 wawili ambao ni kelvin debruyne na david silva kwa pamoja na bado waliendelea kupata matokeo mazuri,

lakini ukija kwetu hata ikitokezea bruno na pogba wamecheza pamoja hususani ule mfumo wa diamond unakuta bado mwalimu analazimisha midfield wawili wawe chini sana hatimaye bruno anakosa msaada muhimu ambao unahitajika, hapo unagundua kwa kiasi kikubwa tatizo kuu ni mfumo wa mwalimu na ufundishaji wake.
 
hivi kwanini timu yetu haiwezi kumiliki mpira hata kwa dakika 2 tu? Hatuwezi fikisha pasi 10 bila kupoteza mpira.
nimejiuliza maswali:
  1. Je tukimsajili jack grealish na sancho ndio tutakuwa tumefanikiwa kutatua tatizo la umiliki wa mpira?
  2. mbona van gaal aliweza kujenga team yenye uwezo wa kutawala possession licha ya kuwa na wachezaji wa kawaida hususani wa kiungo, kwa nini wengine waliomfuata wanashindwa na uwanja wa mazoezi bado ni ule ule?
================================
rudi kaiangalie timu ya xavi hernandez jinsi inavyocheza, je tuseme wale waarabu wana wachezaji bora kuliko manchester united?
matatizo ya umiliki mpira ni ya mwalimu na falsafa zake na si wachezaji.
 
nimejiuliza maswali:
  1. Je tukimsajili jack grealish na sancho ndio tutakuwa tumefanikiwa kutatua tatizo la umiliki wa mpira?
  2. mbona van gaal aliweza kujenga team yenye uwezo wa kutawala possession licha ya kuwa na wachezaji wa kawaida hususani wa kiungo, kwa nini wengine waliomfuata wanashindwa na uwanja wa mazoezi bado ni ule ule?
================================
rudi kaiangalie timu ya xavi hernandez jinsi inavyocheza, je tuseme wale waarabu wana wachezaji bora kuliko manchester united?
matatizo ya umiliki mpira ni ya mwalimu na si wachezaji
Mkuu leo umeamua,kongole kwako.
 
labda nijaribu kujibu kwa mujibu wa jicho langu jinsi linavyozitazama hizi mechi tunazocheza ila fahamu jicho linadanganya ukilinganisha na data, safu yetu ya ulinzi pekee ina thamani ya takribani paundi millioni 300 lakini cha kustaajabisha mwalimu hana imani na safu hiyo iwe ni mechi kubwa au ndogo, mpaka sasa sijaiona hiyo faida ya kucheza double pivot kwa sababu bado tunaendelea kufungwa mara kwa mara tena magoli yenye kufanana.

unapoingia uwanjani huku ukiwa unaongozwa na fikra za uoga unamfanya adui yako abadilishe mfumo wa kiuchezaji na hicho ndicho kinachotukuta mara kwa mara, hatimaye tunajikuta tunakaribisha presha inayoepukika kwenye halfes space yetu

kuhusu bruno na pogba kucheza pamoja hakuwezi kuathiri safu yetu ya ulinzi kama tutaitumia mifano mengineyo iliyowahi kujitokeza, nakumbuka pale man city walishawahi kucheza kwa muda mrefu na namba 10 wawili ambao ni kelvin debruyne na david silva kwa pamoja na bado waliendelea kupata matokeo mazuri,

lakini ukija kwetu hata ikitokezea bruno na pogba wamecheza pamoja hususani ule mfumo wa diamond unakuta bado mwalimu analazimisha midfield wawili wawe chini sana hatimaye bruno anakosa msaada muhimu ambao unahitajika, hapo unagundua kwa kiasi kikubwa tatizo kuu ni mfumo wa mwalimu na ufundishaji wake.
Safi sana. I'm impressed! Umezungumza vitu vilivyo kichwani kwangu hususani maamuzi ya Ole juu ya utumizi wa wachezaji na mifumo sahihi.
 
Na striker kwa mfumo wa sosha panahitajika striker pia scott ni mzur shida yake anakaa sana na mipira anataka kumiliki katikati wakat hana uwezo huo fred si mzur kwenye pasi hata kwa scott hivyo hivyo ndio maana timu inahangaika sana ila kwenye kukaba wapo vizur timu inahitaj wapiga pasi za chap kama carick na scholes walivyokuwa
Scot na Fred siyo wabovu sana katika passing ukilinganisha na midfielders wengine

Kikubwa wanatakiwa waimprove katika foward passing na kuipandisha timu mbele badala ya kusubiri Bruno aamue mpira uende wapi.

Striking force yetu inapoteza nafasi nyingi sana kuliko msimu uliopita sijajua kuna nini kina wasumbua mastriker wetu.

Msimu uliopita timu yetu ilikuwa inatengeneza nafasi chache sana za kufunga magoli lakini tulikuwa clinical sana kwenye chances conversion.

Pattern yetu ya uchezaji haieleweki ndiyo maana hatuonekani kuwa mwelekeo mzuri kwenye uchezaji tunacheza kwa kubahatisha bahatisha tu this is down to coaching.
 
sijaangalia takwimu zinazoangazia mechi alizocheza juan mata kwa hii miaka minne iliopita ila sidhani kama anafikisha mechi 50 alizocheza za ligi kuu. Nafikiri uwepo wa juan mata klabuni unatokanwa zaidi na sababu za kiuongozi kuliko sababu za kiuchezaji. Juan mata anaonekana kuwa ni mwanadamu mwenye taswira ya upole, uvumilivu, aliyeridhika, mpinga fitna(hajawahi kuanzisha mgogoro wowote dhidi ya mwalimu), mwingi wa ihsan na ikhlaq nafsini mwake.

Naweza kusema huu ni msimu wa nne kumshuhudia Juan akikosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza lakini sijawahi kukutana na malalamiko yeyote kutoka kwake kupitia media tofauti ukilinganisha na wachezaji wengineo wenye changamoto inayoshabihiana na ya kwake kwa kuanzia utawala wa mourinho ambaye tuliamini havutiwi na uchezaji wa mata (rejea sakata lake pale chelsea) mpaka huu utawala wa Ole gunnar. Si hivyo tu pia juan amekuwa akichezeshwa nafasi asiyoipendelea kiuchezaji tokea asajiliwe manchester united lakini ameendelea kujitolea kwa moyo wake wote pindi anapopewa nafasi

Nafikiri Ole anamtumia juan mata kama ni mfano kwa wachezaji vijana na hata wale wapya walioshindwa kuingia kwenye mfumo wawe wavumilivu licha ya kukosa dakika nyingi za kucheza, hakuna umuhimu wa kuwatumia mawakala kuleta vitisho vya mikataba na wala hakuna umuhimu wa kuongelea mambo ya klabu kwenye media.

Sitoshangaa endapo juan mata atapewa tena mkataba iwe wa mwaka mmoja au miwili (najua atakubali), nafikiri klabu ina mpango wa kumtumia juan mata siku za mbeleni kuwa ni balozi wa klabu ndio maana wanazidi kumweka karibu.

si hivyo tu pia nimeona vugu vugu kubwa la usajili wa wachezaji vijana kutoka Spain kwa miaka hii ya karibuni kama vile:
  • alvaro fernandez: mlinzi wa kushoto kutoka real madrid na amepandishwa timu ya miaka 23 licha ya kuwa na miaka 17.
  • marc jurado: anatokea barcelona, amezaliwa miaka 16 iliopita
  • armau puigmal: anacheza timu ya miaka 23
  • Mateo Mejia
  • alejandro ganacho: miaka 16 na amesajiliwa kutoka atletico madrid
uwepo wa mata utaweza kuwa ni kichocheo cha kuendeleza huu mkakati wa kusajili vijana kutoka spain, vijana watamchukulia juan kama ni mlezi wao pale Manchester kutokana na uzoefu wake na haiba yake.
Hoja yako nimekuelewa lakini lazima tutafute namna ya kufanya ili tuweze kuleta wachezaji watakaoweza kutupa dimension mpya uwanjani.
 
OGS on manutd summer budget:
"All clubs in the world are going through the same situation so it’s no different for other clubs than for us. I think there’s just going to be less and less transfers happening in the world of football with all these changes."
============
wale tulioanza kuimba wimbo wa usajili wa wachezaji watatu hadi wanne tujiandae tena kisaikolojia na usajili wa mchezaji mmoja kila baada ya wiki 4
 
Probably hatutasajili kabisa kwa hali ninayoiona
 
kwanza tukubaliane man city ni bingwa kwa sasa
mechi zimebaki 12 na point katuzidi 13
MAN U tuliyumba pale tulipo pigwa na sheffild alafu tuka draw na west brown,everton chelsea na arsel

man u ikipata nafasi ya kushinda haishindi nazani tumeona man city wachezaji wana hari kubwa na kujituma na kila mtuu
aanajua wajibu wake

pale man u wachezaji tulio nao ambao ni wa kiwango cha dunia ni POGBA.BRUNO ,NA CAVAN TU
wengine ni vijana wanao baleeeeeeee
uza martial weka sunchez
uza matic let clinishi
uza phin jones,tunzabe leta............

sasa kesho kutwa man city si wanatufanya mbogaaaaaaaa
 
mpaka tarehe 27/01/2021 ligi kuu ya uingereza ilikuwa bado ina mvuto, nakumbuka ilifikia hatua timu ikiwa itapoteza alama 4 ndani ya mechi 2 basi inateremka mpaka nafasi ya 5. Tafsiri yake ni kwamba takribani timu zote zilikuwa na utofauti mdogo sana wa alama na hii ilitokanwa zaidi na ukosefu wa ushindi mfululizo.

udhaifu wa liverpool na manchester city mwanzoni mwa msimu ndio kulitupa fursa ya kuonekana wapigania kombe lakini ndoto hiyo kwa makusudi imefutwa.
  • unafungwa na sheffield = point 3
  • unatoa suluhu na everton ambayo umeifunga mechi mbili mfululizo uwanjani kwao = points 2
  • unatoa suluhu na arsenal = points 2
  • unatoa suluhu na west bromwich = points 2
hizo mechi zitaendelea kuniumiza kadri nitakavyoendelea kuzikumbuka, laiti kama man city angelituzidi kwa alama 6 bado ushindani ungelionekana dhahiri.
 
Back
Top Bottom