Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Pogba anapiga kazi kwa sasa
Umenifanya niichungulie hii comment. Fuentte, mwaka jana alinishtua sana aliposema tumuuze Paul halafu tumnunue Thiago.
fuentte,

Naamini labda ulikuwa umetoka usingizini uliposema tumuuze Paul Pogba endapo akija Thiago. Hapa umeteleza tena sio kidogo Jombaa, sizungumzi labda kwa mahaba pale Uingereza ni viungo wawili tu, Kevin De Bruyne na Bruno Fernandes pekee wana uwezo wa kumkaribia Paul akiamua kucheza mpira seriously.

Usifanye mzaha na Paul, yupo very talented almost 10 times ya huyo Thiago regardless ya majukumu wafanyayo uwanjani. Kitu pekee ambacho watu wengi hatukipendi kutoka kwa Paul ana behavioral inconsistency, ni mtu mwenye ushawishi hasi kwa wenzie ktk vyumba vya kubadilishia nguo hasa hasa akiwa kachukizwa labda na benchi la ufundi au mashabiki au yule wakala wake mwenye tamaa, Mino Raiola.

Kumuuza Paul na kumleta Thiago ni sawa na PSG wamuuze Kylian Mbappe halafu wamlete Jamie Vardy. Tunahitaji tuwe na world class wengi na sio kupunguza, Paul auzwe pindi akianza tabia zake za hovyo ila sio kwa sababu ya kiwango.
 
Ole aliingia defensively zaidi siku ile ila walikuwa wafe goli mbili.

Hata mechi na Arsenal tukiingia kibabe kama leo mapema kabisa watakufa goli 4.
Na sisi kama Gunners tunapenda mje mkiwa mmejiamini sio kinyonge,km kipindi kile mmefunga psg still mkapasuka hapohapo getoni kwenu
 
Back
Top Bottom