Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

We ungekua kocha ungemuacha Wan Bissaka ili uwe offensive?

Mbona na wewe ungefeli kama ndiyo hivyo.
United waliniacha hoi walipotoa pesa mingi kwa ajili ya Bissaka wakati wanaye Dalot ambaye alihitaji tu program ya kumjengea fitness. Kubaki na AWB na T. Fosu Mensah ni miongoni mwa mambo yanaweza kuelezea uwezo wa kocha.
 
United itakapomuachia Pogba atakuwa na miaka karibu 30. Raiola anajua tafsiri yake ndiyo sababu anajitahidi kufanya fujo ili United ifanye muamala mapema. Sema Woodward keshaijua janja yao maana yeye ni genius wa biashara ya soka. Unaweza usiamini Pogba akaja kuishia OT.

Wachezaji wengi wafaransa kipaumbele chao siyo mafanikio ya uwanjani ndiyo sababu wana low mentalities kunako game. Angalia Martial, Bakayoko, Griezmann, na sasa Mbappe. Sisi ilibidi Levy aingilie kati ili asiingie hasara kwa Ndombele. Angalia namna anavyoisadia timu sasa hivi wakati msimu uliopita alikuwa anajifanya mgonjwa kila mechi.

Display zao uwanjani haziwiani kabisa na potential zao.
That french boy "Ndombele" was shit last season..msimu huu naona mourinho amekick-his ass kidogo anajitahidi..

Hawa mabishoo wa kifaransa pasua kichwa kweli..Kuna Martial,yaani talent unaiona ila sasa yeye anachofanya uwanjani unabaki umeduaa,hawajali kabisa
 
Pogba ana miliki mansions, super & luxury cars, private jets, shares kwenye makampuni mbalimbali. Anahitaji nini zaidi hapa duniani?
Hiyo ndiyo tofauti kubwa ya Neimar na akina Ronaldo na Messi. Tafsiri ya mafanikio kwa mchezaji. Yako uwanjani au nje ya uwanja!
 
Kocha mpya bila shaka atataka kikosi chake. Mko tayari kufanya overhaul? Usidhani kuwa kocha atakipokea tu kikosi anachokikuta kwa kuwa wachezaji wengi wazuri. Kuna suala la personalities ambalo makocha wazuri huangalia zaidi.
Listen,yatakuwa ni makubaliano kabla ya kupewa timu..kwamba mimi hawa siwataki kwenye timu yangu,nataka niongeze hawa..sisi tunampa frame time tu ya kutuletea trophies..
 
Kwahiyo ukiitwa brown kwa rangi yako uliyoisema hapo utakubali? Weusi umetofautiana ila wote ni weusi. Unewahi sikia njano iliyokolea/kuivia na njano mpauko? Zote hizo ni njano. Umewahi kuona ama kusikia bluebahari? Na blue za kaptura za watoto wa shule za msingi? Zote ni blue. Sasa iwe brown ama ckokoleti au mangara au weusi kama mkurungu hizo zote ni nyeusi.

Mtizame binti huyu aliye pembeni ya wenzake
Halafu umwite black girl aanze kuvuta mdomo


View attachment 1645352
Lakini pia hawa wasuatao uwaite nyie mabinti weusi naomba kuzungumza nanyi halafu nawao wavute midomo kisa wameitwa hivyo?
View attachment 1645353View attachment 1645354
Ama ukibisha na hapa mchukue mdogo wako au katoto ka dadako ukaambie nani mweupe hapo na nani mweusi hapo halafu uje na majibu.
We jamaa buana
 
That french boy "Ndombele" was shit last season..msimu huu naona mourinho amekick-his ass kidogo anajitahidi..

Hawa mabishoo wa kifaransa pasua kichwa kweli..Kuna Martial,yaani talent unaiona ila sasa yeye anachofanya uwanjani unabaki umeduaa,hawajali kabisa
Noma aisee. Huyo Ndombele Jose alimwambia Levy kuwa hatacheza mpaka arekebishe attitude. Kuna siku Jose alisema anatamani uje ufike wakati Martial acheze kwenye full potential yake. Jamaa wana talents ila ndiyo hivyo pasua kichwa. Jiulize ingekuwaje Cantona asingeamua kuikacha soka akafuate starehe za kwenye movie industry. Aliyofanya misimu minne tu kuyaelezea lazima uchoke.
 
Listen,yatakuwa ni makubaliano kabla ya kupewa timu..kwamba mimi hawa siwataki kwenye timu yangu,nataka niongeze hawa..sisi tunampa frame time tu ya kutuletea trophies..
Hivyo ndivyo inapaswa kuwa. Na kama ingekuwa hivyo huenda United ingeyumba msimu mmoja tu ule wa Moyes. Sasa tatizo la timu yenu haina structure nzuri ya kuwezesha hicho kitu kutokea. Ni nani anaye fanya vetting ya requests za kocha?

Woodward

Scouting team

Na hapo ndipo noma la usajili wa Mani linapoanzia. Kwenye soka la kisasa anayepaswa kumwambia kocha mchezaji huyu hafai ni "mtaalamu wa soka" yaani DOF au wengine huwaita technical directors.

Watu wa scouting uwezo wao mkubwa ni kufuatilia haiba ya mchezaji na kuziripoti kwa wataalam wa soka ambao watamshauri mkurugenzi mkuu (Woodward) nini afanye. Watu wa scouting wasifanye vetting ya wachezaji.

Ukitaka kunipata fresh rejea ishu za wachezaji Alphonso Davies, Harry Maguire, De Ligt, Alex Sandro, Perisic, nk. Ukijua majibu ambayo Woodward alideliver kwa kocha baada ya kushauriwa na watu wa scouting utabaki mdomo wazi.

Sasa hapo ndiyo shida kwa kuwa huyo kocha mpya atanegotiate na Woodward kwa usaidizi wa scouting team kitu ambayo ilimfanya LVG adai bosi wenu ana zero understanding of football.
 
United waliniacha hoi walipotoa pesa mingi kwa ajili ya Bissaka wakati wanaye Dalot ambaye alihitaji tu program ya kumjengea fitness. Kubaki na AWB na T. Fosu Mensah ni miongoni mwa mambo yanaweza kuelezea uwezo wa kocha.
Mimi nasema ulifanya vyema kuhama Man U. Na umepiga timing nzuri kuhamia Tottenham kipindi hichi.
 
Hii iwafikie popote mlipo united fans
 
1607526929945.png


AWB aliachiwa gunia la misumari na bwana tactician akishirikiana na wachezaji wake, upande wa kushoto tulicheza na fullback wawili wanaopewa msaada mkubwa sana nemanja matic ndio maana leipzig hawakuweza kudominate eneo hilo na wakaamua kuswitch upande wa kulia uliokuwa na madhaifu kwa sababu greenwood alicheza kama striker hivyo basi alikuwa anashindwa kutimiza majukumu ya kulinzi upande wa kulia na hatimaye wan bissaka alibaki peke yake.

kimbinu Ole alikamatwa kwa sababu alikuja na akili ya mechi iliopita
 
Tactical OGS uwezo wake sio wa kufundisha United,na anashindwa kupanga timu kutokana na opponent anao kutana nao,recently imekuwa kawaida United kuanza kufungwa magoli ndani ya 30 minutes then second half anagundua makosa na kufanya sub.Moja ya sifa ya kocha mzuri ni kuwajua wapinzani wake (strength & weakness) na kuzifanyia kazi

Thomas Tuchel &Julian Nagelsmann baada ya kufungwa na United mechi za kwanza walifanya analyisis wakagundua makosa waliyofanya next game wakashinda na ku-qualify .
Mkwawa anakwambia tumekuwa kings wa comeback.

Sisi ni wa kushangilia comebacks leo hii.

Hata tukishinda, till Ole hajui anachofanya.

Moods za wachezaji ndo zinambeba.
 
Pogba ni mjinga sana, halafu haonagi kwamba umri unamtupa mkono. Anatimiza miaka 28 soon. Yeye ana amini bado ni mdogo eti ana bright years ahead. Hajui kwa ile mentality mbovu ataishia kuwa wonderful talent with no meaningful achievement. France kushinda WC sio kwamba ni direct credit kwake tu. Anatakiwa aoneshe anaweza ku shine nje ya kuwa covered na Kante na Matuidi
Hata wakina Rashford na Martial bado wanajiona makinda.
 
Solskjær anachagua timu kwa ajili ya mechi, wenzake wanachagua mipango kwa ajili ya mechi yenye kuambatana na well-drilled movements (jinsi gani adui atajiandaa na kuweza kumdhibiti).

angelino anafahamu fika ni eneo gani anapaswa kuwepo na nini cha kufanya pindi anapokuwa na mpira eneo fulani, kwa mfano kabla ya kupiga krosi tayari alikwishafahamu haidara atajiweka eneo fulani.

niliwahi kumsikia ole akisema yeye ni muumini mkubwa wa klopp na style yake ya uendeshaji wa timu, ukiwaangalia wawili hao wanachokifanya unagundua ya kwamba ole ni pragmatic manager na si progressive manager na kwa miaka hii miwili anazidi kutuonyesha ya kwamba si mwalimu mwenye uwezo wa kuitransform team kupitia mazoezi ukimlinganisha na huyo rolemodel wake

jamaa pumzi yake imekata, kwa kocha anayejielewa hahitaji kuwa na wachezaji bora 15 ili aweze kucheza soka la kiwango cha juu dhidi ya crystal palace, west bromwich, waturuki, psg iliojifia, southampton, arsenal na west ham huku ukiendelea kuomba upewe muda ujenge timu bora ya wachezaji 25(hata madrid na barcelona hawakuwahi kuwa na wachezaji bora 25 kwenye kikosi chao)
ole amejaaliwa kuwa na kikosi bora baada ya liverpool na man city lakini jinsi inavyocheza unaweza kudhani ni genge la wahuni linalohitaji overhaul ya wachezaji 10 kwa kila msimu
 
Back
Top Bottom