Hama hii timu itakuja kupa presha rafiki yangu.
imeshaniongezea presha na msongo wa mawazo kana kwamba nafaidika nayo kiutajiri..
leo nimepata usingizi saa 11 alfajiri (mawazo yamenitawala nafsini)
cha kwanza kinachoniuma ni kwamba jana jioni nilitembelea ukurasa wa instagram wa
george ambangile alipost video yake akiwa ndani ya kipindi cha michezo akiwazungumzia leipzig jinsi wanavyocheza kuanzia pale katikati wanavyojazana kwa kuua winga zao, jinsi wanavyotumia
angelino kuset mashambulizi baada ya kufanikiwa kumhamisha mlinzi wa pembeni eneo lake, pressing yao na ball possession na jinsi wanavyokuwa watano pale nyuma wasipokuwa na mpira kama umewaangalia vizuri(alitolea zaidi mfano wa mechi ya bayern munich).
yaani george anayeishi Tanzania anawafahamu leipzig kiundani kuliko kocha wetu na benchi lake la ufundi linaloongozwa na football analyst na wataalamu wa IT wanaotambulikana duniani.
kipindi chote cha kwanza
wan bissaka alikuwa analazimika kuwa nje ya eneo lake(mara nyingi alikuwa anacheza katikati), ina maana leipzig walifanikiwa kimbinu ya kumhamisha eneo lake ili asikutane mara kwa mara na angelino (one against one) na hapo ndipo angelino alipata fursa ya kutukhanithi anavyotaka (goli zote zimetokea kwake na hata hizo walizokosa zinatokea kwake)
baadae nikaangalia video
statman dave (kwa mashabiki wa man utd wengi wao watakuwa wanamfahamu) naye alikuwa anawafanyia analysing leipzig na jinsi gani unaweza kuwabypass (kuwadhibiti), huyu ni mzungu mwenzake ina maana kama ameangalia ile video basi angalijifunza, cha ajabu aliyoyazungumza dave ndio yale yale yaliokwenda kujitokeza uwanjani masaa matano baadae.
second half yule baradhuli wa kinorway anamtoa telles (sidhani kama ameumia) then anambakisha shaw ambaye hana match fitness kwa wiki za karibuni na dakika 20 baadae anamtoa luke shaw then anamuingiza brandon williams.
nilitamani televisheni niivunje kwa hasira.