Ndo maana nilikuuliza tokea mwanzoni kuwa why do you need another top striker wakati tayari mnaye Rooney?
Au unataka kusema kuwa Rooney is not a top striker let alone a striker?
Jaribu tena na maelezeo yako ya wikipedia.
Mimi naelewa soka, kwa sababu nlifundishwa kucheza soka.
Katika soka kuna positions kuu 3 ukitoa ya golikipa, nazo ni: back, midfield na forward. Sasa humo ndimo kuna aina mbalimbali za uchezaji. Iwe kwa back, midfield na forward; ndiyo maana kuna right and left back ambao wanacheza kama right and left wingers; vilevile uitwa attacking full-back right or left. Kina Evra, Maicon, Alves, Cafu, R. Carlos etc. Pia katika back kuna malibero na stoppers; kina Terry, Vidic, Cannavaro, Baresin.k. Kuna midfielders walio playmakers ama creative midfielders kama akina Ozil, Sneijder, Kagawa, Iniesta, Cesc, Kaka; kuna defensive midfielders ama box-to-box midfielder kama akina Mascherano, Makelele, Keane, walio kama mabeki. Nikienda kwa forwards, napo kuna goal poachers kama akina Shaun Goater, Nistelrooy, Inzaghi, Chicharito n.k. Kuna target man kama walivyo Cristiano na Messi katika timu zao; uwa upewa mipira kila mara ili kufunga. Wanakuwa kama roho ya timu katika kufunga.
Nikirudi kwenye mada. Rooney siyo namba 9 ni namba 10 kwa United. Namba zote ni za forwards; tofauti yao ipo kwenye uchezaji. Uchezaji wa namba 9 siyo sawa na wa namba 10. Unaposema Rooney ni striker ni sawa, lakini siyo namba 9. Cristiano naye ni striker; lakini anacheza namba ngapi?!? CR ucheza kama right forward, lakini ni striker wa Real; huku Karim akiwa kama namba 9 wao. Hivyo mtu kuitwa striker ina maanisha ni aina tu ya uchezaji akiwa kama forward, iwe centre forward ama right au left forward.
Kitu kingine, United has always played with a classic number 9; that is United's style. Whether you call it outdated or whatever, that is United's business. It is such a formation that has won United over 30 titles over the past 20 years.
Who are you to question the style now?!?
Hivyo kukosekana kwa RvP kama namba 9 wa United kumeonyesha umuhimu wa kuwa na namba 9 mwingine. Nimeshasema Javier anafaa kama super sub; uchoka mapema sana.