mfarisayo
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 5,160
- 2,004
Chifu, what's your point on this? Maana sielewi unachokikomalia hapa; wakati nimeshasema Antonio hakucheza vizuri kama alivyocheza katika mechi za awali. Ila tatizo lilikuwa la timu nzima.
Chifu, kama ndio unafanya hivi argument. Kwa heri. Naona hutuwezi kuelewana katika hili la positions na style of playing katika dimba.
Dah! Wewe ni kiboko! Anyway, nilichosema ni kwamba, pamoja na kucheza vibaya kwa Antonio, timu nzima haikucheza vizuri. Timu ilikosa mtu pale mbele ambaye angekuwa anawaweka roho juu mabeki wa City. Ndio maana nikasema, hiyo inaonyesha tunahitaji mtu mwingine (namba 9) wa kusaidiana na RvP kama RvP hayupo. Sijasema tatizo ni kutokuwepo kwa RvP. Timu nzima haikucheza vizuri.
Nimeshasema hayo huko nyuma pia. Nilimlaumu David kwa kuwaanzisha Danny na Ashley badala ya Javier ama Kagawa/Nani. Kukosekana kwa RvP kungelazimu hao kuwemo ndani ya dimba.
RvP alikosa jana mechi kutokana na thigh injury; sasa hizo fununu ni udaku tu! Mimi sijadili udaku, jaribun mwingine.
Ngoja na mimi nijaribu kuchangia kadiri ya uelewa wangu, Kwanza katika Mechi ya jana Valencia hakucheza kama kawaida kutokana na Timu nzima kuwa vibaya na Hapakuwa na Maelewano kati yake na Smalling ambaye jana hakuwa kwenye form kabisa (Binafsi jana ningependa kuona Smalling anatoka then Valencia arudi kucheza nafasi yake na kuingia winga mwingine ambaye wangeshirikiana kusukuma mashambulizi)
Kuhusu Nafasi na Mfumo wa Kiuchezaji
Katika Mpira position mara nyingi hutegema na mfumo wa timu, But general speaking namba za wachezaji zipo in pair,
Defense
Mabeki wanawezwa kugawanywa katika Makundi Makubwa mawili au Matatu kulingana na Mfumo. Kwanza kuna Pair ya Mabeki wa pembeni (yani Full back left and Right), Pili kuna Mabeki wa Kati hawa wanatofautina kidogo kimajukumu japo kwenye mfumo unaweza kuwaona wanacheza kwenye line moja. hapa kuna Centre-Back (Center half) na kuna Sweeper (Libero) ambao wanatofautina kimajukumu. Center Back yeye kazi yaki ni kumtrack na kumkaba namba 9 pamoja na kucheza mipira yote ya Hatari ya kwanza (Kwa Utd hii ni kazi ya Vidic) na Libero au Sweeper (kwa Utd ni Rio /Evans au Smalling) kazi yake kubwa ni kusoma mchezo na kuorganize/kupanga wenzake, kuclear lose balls baada ya Centre back kutibua move, pamoja kusaidia Kuziba mianya au kufuta makosa na wenzake.
[h=3][/h]Midfield
Viungo nao wanaweza kugawanywa katika makundi Matatu, kwanza kuna Mawinga au washambuliaji wa pembeni wenye jukumu la kusaidia walinzi wa pembeni na zaidi kusaidia Washambuliaji wa mbele au kati, Pia kuna kiungu mkabaji yani namba 6 na Kiungo mshambuliaji na mchezeshaji yani namba 8
Forward
Hawa wapo wa aina mbili kuna Msambuliaji Mfungaji (Centre forward/Finisher/Predator/Goal scorer/Goal Hunter/Goal Gater) huyu kazi yake kubwa ni kufunga tu hana kazi nyingine.
Pia kuna mshambuliaji tunaweza kumuita msaidizi (Second Striker/Goal maker/Support Striker) huyu kazi yake kubwa ni kumtengenezea mazingira mazuri Goal Scorer kufunga pamoja kusaidia na Viungo kati na pembeni katika kuchezesha timu
Hapa ndo inapokuja point kuwa Rooney sio Class Striker kwa kuwa hachezi kwenye nafasi ya Finisher kama Chicharito au Van Persie ingawa Van Persie ana iwezo wa ziada wa kucheza kama Second striker pia.