Kama umeangalia mechi ya West brom, kwa dakika Chache ambazo martial alienda Kushoto, rashford akaenda Kulia na cavani katikati, tulikuwa fluid sana.
Unapozungumzia fluid Attacking kwenye mpira unamaanisha ule uwezo wa wale wachezaji pale mbele kucheza nafasi zaidi ya moja. Wanaposhambulia wanaweza kubadilishana nafasi haraka haraka kutengeneza movement na kuwatoa defenders kwenye nafasi.
Kwa Timu yetu fluid ipo kushoto tu baina ya Martial na Rashford, hawa wapo comfortable kucheza striker ama ku cut in toka kushoto, na ni jambo la kawaida martial kumkuta kushoto japo anachezeshwa kati ama kumkuta Rashford kati japo yeye ni wa kushoto.
Mata alicheza Kulia mechi na WBA, Mata hawezi ku echange na wenzake, hawezi kudrible past player na muda mwingi anakuja katikati hivyo fluid inaharibika kulia.
Ndio maana mshabiki yoyote wa Man Utd anaefahamu hata basics za Formation utaona anataka winga wa kulia na makocha wote kuanzia LVG, mou mpaka Ole wanataka winga Lakini Bwana Mkubwa Woodward anajua zaidi.
Mkuu umeeleza vizuri kuhusu martial na rashford na cavani..
Naomba niweke nyama kidogo kwenye comment yako,,
Ni kwamba mata analazimika kuingia katikati kwa maelezo ya Mwalimu kufuatana na kucheza double defensive medifilder..
Fred na tommy.
Pale mbele mchezaji creative ni Bruno peke yake,,
Kwahyo mata anacheza kati na kuua winger ni ktk kuongeza nguvu eneo la kiungo wa juu..
Ndy maana watu wengi wanazungumzia mfumo wa ole kuchezesha double defensive midifilder..
Siku man u wakipata beki imara hawatachezesha tena double defensive midifilder,,
Na hapo kila mchezaji atacheza kwa mfumo uliozoeleka wa man u kutegemea winger..
Nakuhakikishia hata Sancho akiwasili man u,,still watatumia double defensive medifilder sababu beki ni mbovu..
Ni sawa na bati linavuja sasa tunaweka nylone juu yake ili kupunguza bati kuvuja..
Ole anapaswa anunuwe beki imara,,na winger imara,,
Hapo utaiona man u ile ya Ferguson