Sishangai Maguire kula umeme, tayari jamaa asha-lose confidence. Wachezaji wetu wanapata dhihaka sana mitandaoni. Kwa mchezaji kama Maguire sasa hivi anapambana zaidi kuudhihirishia ulimwengu kuwa ni bora kitu kinachomfanya akose umakini uwanjani.
Ukiangalia page za United na za wachezaji katika comments 10; 7 utakuta ni trolls kumu-attack mchezaji au timu nzima. Maguire mara aitwe fridge. Tumeona watu kama wakina Lingard wametukanwa sana hata juzi kuna takwimu zilitoka wachezaji wanaoongoza kutukanwa mitandaoni Rashford alikuwa wa kwanza na watu wengi walishangaa ni vipi Lingard hayupo kwenye list.
Wachezaji wetu wanahitaji socia media detox kwa angalau mwezi mmoja na ikiwezekana accounts zao za mitandao wapewe watu wa kuziendesha, afya ya akili ni muhimu kwa wachezaji. Hii timu nishaanza kuona watu watatupiana sana fuko la misumari ila shida pia ipo kwa mashabiki wa United na mashabiki wa timu pinzani wanashambulia sana wachezaji wetu.