Uchezaji wa Pogba kwenye timu zote hizo ni ule ule isipokuwa kuna mambo kadhaa akiwa united yanayosababisha aonekane haperform.
1. League intense karibu kila mechi hivyo hawezi outperform every game.
2. Physicality ya kufunika mapungufu yake kwenye defence.
Nitatoa mifano katika timu zote alizozichezea.
Alipokuwa Juventus
Alikuwa anazungukwa na Andres Pirlo na Claudio Marchisio au Pjanic ambao kwa kiwango kikubwa walikuwa wakifuta makosa yake.
Pirlo alifanya kazi ya kumcomplement Pogba kwenye kudictate game while Marchisio au Pjanic waliongeza physicality kwenye midfield, hao watu walifanya pogba awe mobile zaidi uwanjani cause hana defensive duties.
France national timu anazungukwa na Blaise Matuid na Ng'olo Kante hao ni wachezaji ambao ni mobile na physical karibu wote hivyo wanamuondolea pogba defensive duties uwanjani anafanya kazi ya kudictate mchezo tactically.
Man united wakati wa Mourinho hapa timu ilikuwa inabadilika badilika hivyo sitazungumzia.
Wakati wa Ole akiwa interim Manager Ole alikuwa anamtumia Ander Herrera na Matic kwenye role zile za Pjanic na Pirlo au Pirlo na Marchisio ukizingatia wote Matic na Hererra wanakaba sana hivyo walikuwa wanaongeza mobility ya Pogba na kufanya adictate mchezo tactically.
Ukiangalia sasa hivi Pogba anatakiwa kutekeleza akicheza Matic Pogba na Bruno na Pogba kupewa defensive duties anageuka kuwa weaklink kwenye timu cause anafanya makosa mengi sana defensively.
Umewahi kujiuliza kwanini Pogba akicheza alongside Scot anaperform vizuri but akicheza na Fred defensively tunafanya makosa mengi sana ?
Sent from my SM-A105F using
JamiiForums mobile app