Tuache bias tunaposhinda mnasema wachezaji wamejituma kuficha makosa ya Ole
Tukifungwa tunakimbilia kusema Ole ni mbovu.
I don't understand
Sent from my SM-A105F using
JamiiForums mobile app
Mkuu nimekuwa nikifuatilia sana maoni yako juu ya Ole una positive view sana kwake (which is good) na ni dhahiri upo upande wake. Una point nyingi za msingi kumtetea Ole na naheshimu hilo kwa mawazo yako ila Ole HAJUI!
Msimu huu 'Ole Boys' mnasema ni match fitness ndiyo imeleta matokeo mabovu; kwa 40% nakubaliana na mawazo yako ila 60% sikubaliani na wewe. Hii timu ya Ole haijaanza kupata shida ikicheza na timu ndogo msimu huu, tumeona last season ilikuwa ni kama vile timu kubwa tu ndiyo Ole anaziweza kwenye mbinu zake.
Kipindi cha Ole tumefanikiwa kusajili wachezaji wazuri sana ila amekuja kuonyesha ni jinsi gani bench lake la ufundi linaua vipaji.
Nakumbuka maneno ya vibanda umiza mapema msimu uliopita:
"Wan, two, three Bissaka"
"James the Flash"
"Maguire" hii wadau walikuwa wanaitamka Kiswahili kuonyesha msisitizo.
Leo hii imebaki story, yapo mengi mazuri Ole kafanya ambayo yananifanya nitamani abaki ila kwa machache mabaya anayofanya ndiyo chanzo cha United kufeli.
Ukienda Everton utakuta World class player mmoja sidhani kama kuna mwingine, nenda Leeds sidhani kaka kuna World class player. Ila ukirudi Manchester United utakuta kuna Pogba, De Gea, Bruno na wachezaji wengi wenye uwezo binafsi mkubwa ambao ukiunganisha uwezo wao ndiyo unapata timu ya kueleweka.
Mimi sililii mataji kutoka kwa Ole, nataka mpira unaoeleweka uwanjani. Makombe yatakuja tukiweza kucheza soka safi as a team na kila mtu ajue namba yake na mbinu za kocha ibaki ku-deliver tu uwanjani.
Test yangu kwa Ole ni game ya Newcastle, hawa ni the likes of Crystal Palace na Brighton. Sasa hivi sitegemei kisingizio cha fitness sasa hivi mtatuambia shida ni wachezaji au mbinu na ufundishaji wa kocha.