Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mkuu kwani Guardiola amekuzaje kipaji cha sterling?

Ole hakimbii lawama za kuflop kwa DJ mbona akiwa Wales anacheza kwa confidence na anaassist na kuscore kwanini isiwe kwetu? unamuanzisha mata 7 DJ benchi unataka afeel vipi yani mtu ambaye sio namba 7 acheze namba yako hata wewe lazima uhisi kudharaulika.....

na kama tetesi ni za kweli board wametumia akili kugoma kukubali mawazo ya Ole kuwa DJ auzwe Leeds....haiwezekani mchezaji mwaka mmoja tu alafu umuuze kwa kutegemea uongezewe hela ulete mwingine nooo....

Bissaka anafuatia amekuwa too sloppy hata confidence anakosa sikuhizi anashinda sana nusu ya uwanja ya mpinzani kiasi kwamba anasahau majukumu ya kukaba, kama sio kuona aibu basi Ole angeomba anunuliwe beki no 2 mwingine (Usinipe habari za Guardiola kwamaana hii ni machester united na sio City) by the way tuna scouting kubwa kuliko city so ni rahisi city kufanya mistake kuliko sisi

Ole anashindwa kutumia strengths za wachezaji alionao.... alizeti huchujwa na mashudu hubaki ambayo nayo huwa na faida zake pia.....Ole ameshindwa kuchuja mafuta (Uwezo) kwa wachezaji wetu ajabu alimkataa Lukaku anamchezedha martial hapo 9 Sahizi anamleta Cavani kwa €10mil (agent fees) 34yrs hapo usisahau ameshindwa mtumia Ighalo anaongeza mwingine.....

watu wengi wanatamani kuona tukicheza na Bruno,Pogba na VDB lakini sioni hilo likitokea kwa maana kocha hana uwezo wa kuwaaccommodate wote 3 kwenye midfield kwamaana hawezi kucheza attacking football (Ukiwa na aina ya hao viungo 3 inabidi uwe unacheza attacking football yenye kumiliki mpira kana city,bayern or liverpool)

Mbinu mbovu, uwezo mdogo, maamuzi mabovu na kutokusoma alama za nyakati ndicho kitakachomfelisha Ole defensive team kama Brighton wanatuzidi possession kwenye game ya ligi kweli tupo serious....

Ngoja tuone ila kichaka cha kujificha kinazidi kukauka nyasi, msimu huu ni either aoneshe kweli anauwezo au aoneshe sio mtu sahihi.....

Issue ya DJ ni very clear Ole alikurupuka kumsajili bila kumjua mchezaji alipewa feedback tu akajichanganya same kwa Bissaka....
daah we jamaa umeona mbali sanaa umeongea point wenye mapenzi na utd wanaelewa hili, tuache ushabiki ili kuficha makosa hata kama tunaipenda timu yetu tusifiche makosa,
Dj, bissaka viwango vyao vimedrop hata ukiangalia maguire pia kocha ameshindwa kuwajenga kisaikolojia hata kiufundi pia itafika wakati hata bruno tutamwona hafai hajui, Kocha kasajili Dj , ighalo lakini hawapati nafasi ya kujengwa kiakili sasa Dj auzwe. Tutazid kuona mafanikio ya wachezaji wetu wakiwa nje ya man utd ndo mana usajili unakua mgumu
 
Poa mtani. Tumepitia hayo maumivu for 30 years na tunayajua. Cha msingi mumvumilie tu OGS, sooner or later ataleta neema hapo OT

daaa mkuu bora nyie mlianza kuipenda liverpool kipindi makombe yamekata sasa sisi tulianza na raha ipo shida sana daaa
 
Duh ata sub yake inaonyesha ajui kufundisha na kusoma mchezo ana muacha Pogba na Bailey ana mtoa Matic na Bruno leo 1-8 zinahusu hapa
 
Tuwe wa kweli nyie mechi ya Crystal Palace na Brighton zote mlitakiwa mle tano,Sema Crystal hawakuwa makini,pili ya Brighton ile miamba ili wasaidia.

Leo hapa mpaka sasa mkono tayari.
 
Back
Top Bottom