Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mkuu mimi ni mfuasi na shabiki kindakindaki wa Manchester United. Nina jezi za kina York, Cantona, Beckham na Vernistrooy hadi leo kabatini...Sharp, Vodafone, Aon, AIG..nk.Nimeisifia Leeds kwa ubora wao katika kipindi ambacho team yangu inavurugwa na wapuuzi kadhaa pale kwenye uongozi. Hii ni sawa na kuvutiwa na mchepuko kwa upuuzi wa mke wa ndani, which is normal for a complete MAN.
Sawa mkuu..tupo pamoja,,kushabikia timu mbili inawezekana,,lakini isiwe sehemu moja,,au unawezaipenda Barcelona,,au madrid lakini huwezi penda zote kwa pamoja,,
Unaweza penda man u,,au Liverpool,, au Leeds lakini huwezi penda zote kwa pamoja..hapo ndy shida ilipoanzia..
Ila nimekuelewa mkuu..
Cavani kapiga hodi man u..atakutoa stress...usijali..
 
Mimi binafsi kufungwa kwa chama langu nimefurahi sana. Kwa sababu naona kuna faida kadhaa tutapata kabla dirisha la usajili halijafungwa. Ya kwanza tutasajili wachezaji siyo chini ya mmoja, sancho uhakika. Vilevile naona jinsi martial na rashford watakavyotengenezewa competition mulemule, ataanza martial then rashford sub and vice versa is true, kitu ambacho ole na benchi lake la ufundi, lazima wamekiona. Mwisho ole nimwonavyo ni mnafki mwenye faida upande mwingine, ile timu imecheza kiboya vile usikute waliambiwa na kocha na benchi la ufundi, maana bila hivyo hakuna njia nyingine ya kuwashawishi board ya man utd, maana ni vichaa wale(kumbuka waliwahi muambia mourinho kuhusu kutokubaliana na hoja ya kumuuza martial kwa sababu wanamuona kama nacmento pele). Hayo ni mawazo yangu.
Nadhani kuna umuhimu wa kuwa wavumilivu.
Naona kama mambo yanajipa.
Wale wa kupiga gap pointi 40 sijui, wasahau hilo msimu huu.
#MUFC
 
Penison,

Ktk front 3 yetu kwangu mimi binafsi mchezaji mwenye akili timamu pale ni Mason Greenwood. Japo ni mdogo kiumri na ni hatari kumpa majukumu makubwa ila kawazidi sana Rashford na Martial almost kila kitu. Kitu pekee wanachomzidi ni umri tu.
 
Penison,

Ktk front 3 yetu kwangu mimi binafsi mchezaji mwenye akili timamu pale ni Mason Greenwood. Japo ni mdogo kiumri na ni hatari kumpa majukumu makubwa ila kawazidi sana Rashford na Martial almost kila kitu. Kitu pekee wanachomzidi ni umri tu.
Hakika mkuu..
Ndy maana nikasema martial atabadilishana na rashford.. Yule Dogo greenwood asisumbuliwe...wamwache atuletee starehe mashabiki wa man u
 
Cavani, hapa angalau zile cross hazitakua zinapita bila kutendewa haki
Huyo jamaa ni hatari sana mkuu,,mm nimemwangalia karibu mechi zake zote za leage one..France,,
Jamaa analijuwa sn goal,,
Tena ni mchezaji style ya Diego Costa,, au gabriel batistuta,,,,anakufunga kwa vyote,,miguu na vichwa..amefungia PSG magoli 200 ktk mechi 300 ...sio mtu wa mchezo mchezo...
Man u tunataka watu serious...hapo tunatakiwa tupate centre back na left back ya kuingiza ndani mfano wa evra..mengine tumuachie ole
 
Zinazowafanya muone man u haina natutal 9
Kwanza Man united haichezi mpira wa kupiga cross cause haina wingers na full backs wake siyo wapiga cross.

Pia Mwalimu ana prefer kucheza na kutengeneza magoli centrally.

Kwa vyovyote vile usajili wa Cavani hautakuwa na impact yoyote kwa sababu hatapata service sahihi from both flanks.



Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom