mr37
Senior Member
- Jul 7, 2020
- 107
- 209
Kwa tulipofikia na hizi tetesi za usajili zisizo na tija , naona tu man u wasitishe usajili mpaka dirisha dogo na tuendelee na wachezaji walewale. Maana kama ndio inafikia kutaka wachezaji walioflop kama Bale, yaani akija United ndio anakuja kupaki basi nyumbani kwake huku akila mshahara wa bure kama yule jirani mwenzetu tuliyemtoa Arsenal.
Yaani sasa hivi siamini kama Man u ndiyo inataka kusajili wachezaji ambao ni wazee kama Bale na Douglas Costa na alafu ni tatizo kubwa sana katika injuries.Mara tena eti tulikuwa tunamtaka Ndembele wa Barcelona aje kuungana na Phil jones , Eric bail na Rojo kwenye kitabu cha majeruhi. Hivi jamani! ligi ina mechi 38 alafu tunataka wazee wa miaka 30 waliofeli ligi zao ambao hata ligi zao wameshindwa kucheza hata mechi 25. Na hata hawana uwezo wa kufunga bao zaidi ya 3 ambacho ni kinyume na kanuni za kuitwa Winger bora. Kiukweli tumeishiwa mipango msimu huu kwenye swala la usajili, yaani tumetekwa na mchezaji mmoja tu (Sancho) ambaye hawezi kuja labda tu maajabu ya Musa.
Mimi naona kuliko kuchukua wachezaji walioflop ligi zao kuja kucheza ligi ngumu kama Uingereza ni bora tubaki na wachezaji tulionao kwa msimu huu lasivyo kuna hatari ya kuchukua failed projects sawa na mchezaji hewa.

★

- Rio ferdinand played his 400th appearances for MUFC