Manchester United (Red Devils) | Special Thread

We jamaa unapenda kuamisha goli..si ulisema kuwa Fred/Matic atakuwa replaced na VDB ndo watu wakakuambia kuwa labda tucheze 442 diamond au 4312 ndo tutakapoweza kuaccomodate viungo wanne?

Halafu Mata alicheza kama winga sio kiungo..Balance ipo ya kutosha kwenye hicho kikosi Matic na Scot wote wapo na ni defensive minded
 
Manchester United midfielder Dylan Levitt has joined League One Charlton on loan. The 19-year-old made his full debut for Wales last week and United are keen for Levitt to build on the experience. James Garner, Ethan Laird and Max Taylor also set to have loan spells away from OT.
 
Ni kweli mkuu nilifurahi sana kuja kwa Donny sasa tunadepth nzuri kwenye midfield yenye wachezaji wazuri 6 hapo tunaweza kubadili mfumo uwanjani kadri tunavyotaka lakini pia tunaweza kufanya sub ya Pogba au Bruno bila shaka pale wanapochoka.
 
tukijificha kwenye hoja ya kupata majeruhi kwa wachezaji wetu muhimu msimu uliopita ndio kumepelekea tulingane na chelsea kwa alama nafikiri tutakuwa tunafanya makosa makubwa sana ya kiutetezi na huenda tukaishia kufungwa sisi gerezani. Ni kwa sababu hata chelsea na wao watakuja na utetezi wa kwamba walikosa nafasi ya kusajili wachezaji walioondoka (mfano eden hazard aliyekuwa key player) na pia walikosa nafasi ya kuimarisha kikosi chao kutokana na mapengo yaliojitokeza chini ya kocha sarri, wakati sisi nafasi hiyo tuliipata lakini tukashindwa kuitumia ipasavyo kwenye dirisha kubwa la usajili.

kiuhalisia ndani ya timu yetu tulianza kupata matokeo mazuri baada ya kuibuka kwa nemanja matic na bruno fernandez, bado naamini ya kwamba kama kocha wetu angelikuwa serious kifikra basi usajili wa bruno ulikuwepo uwezekano mkubwa sana wa kukamilishwa ndani ya dirisha kubwa la usajili ila kujidanganya kwa mwalimu na mabosi wake ndio kulipelekea klabu yetu kupata matokeo mabovu kwenye nusu ya kwanza ya msimu.
=====================================
wakati ligi kuu ya uingereza inaanza (mechi dhidi ya chelsea) eneo la kiungo alikuwepo nemanja matic pamoja na juan mata lakini hao wote walianzia benchi ili kutoa nafasi kwa mmoja wao kati ya jesse lingard au andreas perreira (tokea pre-season tuliongea humu ndani baadhi yetu ya kwamba kwa kuwategemea hawa makatuni wawili hatutofika popote).

  1. ok, tumeshindwa kumsajili bruno fernandez, cha ajabu mechi nne za mwanzo Ole alikuwa analazimisha paul pogba acheze namba 8 pamoja na scott mctominay nafasi ambayo ulikuwepo uwezekano wa kumtumia nemanja matic then paul pogba acheze namba 10 (kama anavyocheza bruno) kinyume chake alikuwa anamtumia andreas perreira au jesse lingard eneo la namba 10.
  2. baadae paul pogba akapata majeruhi, kuumia kwa pogba pia ndio ulikuwa mwanzo wa fred kurudi kwenye kikosi baada ya harusi na ishu nyenginezo (match fitness) na ilikuwa ni mechi ya 5 ya ligi kama nitakuwa nipo sahihi, cha ajabu ole akaendeleza tabia ile ile ya kumbeba perreira na lingard na hatimaye fred akaendelea kukaa benchi.
  3. mechi ya arsenal paul pogba akarudi tena kwenye kikosi cha kwanza baada ya kupona majeruhi, OLE na benchi lake la ufundi wakaendelea kulazimisha jesse lingard na andreas wawemo kwenye kikosi cha kwanza huku benchi letu wakiwepo juan mata, fred na nemanja matic ambao hao wote wana ubora mkubwa kuliko wawili hao hata wasipofanya mazoezi.
  4. mechi iliofuata tunapoteza dhidi ya newcastle united na kwa mara nyengine tena andres perreira anacheza mbele ya nemanja matic, kwa ufupi mpaka tunafika mwezi oktoba hakuna hata mechi moja ambayo OLE na benchi lake la ufundi waliacha kuwatumia andreas perreira au jesse lingard kwenye kikosi cha kwanza, baadae matic na paul pogba wakapata tena injury.
tokea mwanzo (dirisha kubwa la usajili) bwana ole alishaweka akili yake kwa wachezaji wawili (andreas perreira na jesse lingard) waongoze jahazi la kiungo mshambuliaji ndio maana paul pogba akashushwa chini zaidi, ila baada ya kuona wachezaji hao wameshindwa kufikia matarajio makubwa aliyoyaweka kupitia wachezaji hao na paul pogba kuendelea kuwa majeruhi ndipo alipoamua dirisha dogo la usajili amrudie bruno fernandez.


tujiulize tokea bruno fernandez asajiliwe na nemanja matic apewe nafasi hao wahuni wawili(lingard na perreira) wameanza mechi ngapi?
bado naamini zile mechi tulizopoteza point kizembe dhidi ya timu ndogo kama tungelianza na midfield ya pogba, mata, scott na matic/ fred tungelipata ushindi.


=============================
naamini hatujaangushwa na majeruhi, bali tumeangushwa na team selection.
paul pogba + marcus rashford
ndio wachezaji pekee waliopata majeruhi ya muda mrefu.​
 
Hivi mata ni winger? Au attacking midfielder?
Sasa kwa mfumo huo kwann pogba ..Fernandez,,na VDB wasicheze pamoja?
 
Hivi mata ni winger? Au attacking midfielder?
Sasa kwa mfumo huo kwann pogba ..Fernandez,,na VDB wasicheze pamoja?
Mata Natural ni no 10, ila mechi nyingi man U anachezeshwa kama winga wa kulia, inside forward wa kulia etc mara chache sana kukuta yupo 10, na ukimkuta ni mechi ndogo ndogo.

Pogba/fernandez/VDB kucheza pamoja umeshajibiwa kwa mfumo wa sasa hatuwezi, labda mfumo ubadilike
 
Mkuu hoja yangu ni kwamba hao viungo wote wanacheza pamoja,,
Zikaja hoja kwamba haiwezekani,,wacheze pamoja sababu sio defensive midfielders..
Sasa hivi baada ya kukupa proofs kwamba watacheza hivi..
Unasema nahamisha goal.
Nilisema VDB hakuletwa kukaa benchi. Au acheze na Fred,,VDB ameletwa acheze pamoja na Fernandez,, pogba na VDB..
Kuhusu hoja ya haiwezekani kucheza pamoja hiyo nimeshaipangua, hapo yupo mata kulia ,kwani mata ni winger? Au attacking midfielder?
Tatizo lako wewe huelewi ninachomaanisha..
Fernandez,, pogba,,VDB together wanacheza pamoja,,
Na option zote za mifumo nimewapa,,
 
Aliyekuja na hii idea na wote waliopitisha hawakufikiri vizuri, hii rangi design haiendani na brand ya man u

Kuna kitu kimoja kuhusu hii jezi. Mchoro wa hii jezi unaitwa Dazzle Camouflage.
:
Dazzle camouflage ni mchoro ambao ulikuwa unatumika kwenye vita vikuu vya kwanza vya dunia.
:
Dazzle camouflage kwenye meli za Kivita ilikuwa inachorwa kwa kumaanisha hao ni MA - FIGHTER , WANA SPEED , HAWAPIGWI OVYO.
:
Wenzetu kibiashara kila kitu huwa kina kuwa na theme au meseji ya kibiashara.
:
Meseji ambayo wateja wengi huwa wananunua kwa ajili ya kunimotivate n.k.
:
Wenzetu hawauzi bidhaa wanauza feelings iliyopo ndani ya bidhaa.
:
Feelings zinazowekwa kwenye bidhaa ndiyo huwa zinanunuliwa.
:
Mtu ananunua feeling ya NIKE na siyo kiatu pamoja na kwamba kiatu kinaweza kikawa kizuri lakini ile feelings ya JUST DO IT inanunuliwa sana.
:
NDIYO maana asilimia kubwa ya Campaigns za Nike ni kuhusu na ujumbe wao wa Just Do It na siyo Campaign za kutangaza mchoro wa kiatu.
:
Watu wana focus kwenye kuuza na kununua feelings iliyopo ndani ya bidhaa.
Turudi kwenye hii Dazzle camouflage. Kwanini Nike walifanya vyema kwenye design ya Dazzle camouflage ? kwenye viatu na jezi ya timu moja huko Marekani ?Walichukua meseji ya (FIGHTER , SPEED , UNBEATABLE ) afu wakachanga na yao ile ya Just Do It .
:
Wakawezeka kutuambia Just Do It kwa sababu wewe ni fighter , una speed ya kukimbilia mafanikio na uko unbeatable.
Watu wanatumia aspirations na siyo price na uzuri kuuza jezi zao.Adidas baada ya kuona hivo wakacop design ya dazzle camouflage.
:
Lengo lile lile kuichukua meseji iliyopo kwenye Dazzle Camouflage. Meseji ambayo ilikuwa inatumika kwenye vita kuu vya kwanza vya dunia.
:
Meseji hii itafanya kuuza jezi nyie dunia ya tatu mtalalamika kuhusu ubaya wa jezi lakini dunia ya kwanza kwenye soko la Adidas watakuonesha namna ya kuuza feelings za hizi jezi ambazo sisi tunasema ni mbaya.
 
Hatuwezi kivipi mkuu ? Kwani wewe ndy ole?
Yeye kasema wanacheza wote ili apate magoli zaidi,,
Na hata kuhusu mata unasema ni no 10,
Kumbuka hata hao akina pogba na Fernandez na VDB wote wanacheza no 10 na 8 kama mata,,
Ila mata ni left footed attacking ..
Muda utaongea,,au pengine mfumo huo usitoe matokeo chanya,,
 
Siyo wote mkuu Reguillon ni fullback wa kawaida tu siyo upgrade ya Brandon wala Luke Shaw.

Fullbacks za Real Madrid za sasa ni za kawaida tu na Marcello alikuwa na majeraha ya muda mrefu kwanini Reguillon hakuchukua nafasi.
kama pesa ipo ya kutafuta mlinzi mwengine wa kushoto mwenye kuvuka ubora wa hawa tulionao basi si vibaya kama tutasajili tena mlinzi wa pembeni kwa mara nyengine (dalot, wan bissaka, luke shaw, rojo, darmian)

nikimuangalia brandon williams anavyocheza inaniwia vigumu sana kuamini ya kwamba siku moja ataweza kufikia level ya ubora waliokuwa nao walinzi wengine wa kushoto waliokuwa wanatumia mguu wa kulia kwa kiwango kikubwa sana (mfano phillip lahm na javier zanetti).

kwa ufupi brandon williams anateseka sana pindi anapocheza upande wa kushoto na kuteseka kwake kunapelekea timu yetu iwe dhaifu sana pindi tunapokwenda mbele kushambulia (kiwango kibovu cha rashford na kuumia kwa luke shaw kulipelekea kwa kiasi kikubwa upande wetu wa kushoto kuwa butu mwishoni mwa msimu)

brandon williams hana msaada mkubwa sana tunaposhambulia (si hodari wa kuoverlap, passing accuracy bado ni tatizo, hawezi kumzidi mpinzani akiwa outside, hawezi kupiga krosi ya uhakika kwa kutumia mguu wa kushoto) ukimlinganisha na luke shaw (japokuwa shaw hana maamuzi bora tunapofika eneo la hatari lakini bado analeta faida kubwa sana, link-up na uhuru kwa winga wa kushoto).

kama ni kweli tunahitaji kufanikiwa kupitia huu mfumo wa 4-3-3 basi tunapaswa tuongeze nguvu kubwa sana eneo la pembeni, ni lazima tuwe na wachezaji wenye uwezo wa kupenetrate, break low blocks and provide natural width, kwa sasa hatuna traditional wingbacks wa uhakika lakini kufidia tatizo hili hatukupaswa pia kukosa attack-minded fullbacks ((nimeumizwa sana na usajili wa mchezaji aina ya wan bissaka kwa gharama, huyu hana kisingizio cha kutumia mguu wa kushoto akiwa ni mlinzi wa kulia kama ilivyo kwa brandon williams)

angalia timu kama real madrid wanamtumia marcelo wa zamani, juventus (alexsandro), barcelona (jordi alba wa zamani), robertson (liverpool), davies (bayern munich) na wote hawa wanatumia miguu ya kushoto ya asili.

ikiwa ole hana imani na diogo dalot basi ni bora auzwe halafu brandon williams arudishwe upande wa kulia apambane na wan bissaka.
uzuri ni kwamba wan bissaka na brandon wana takwimu nzuri sana za kiafya,

ningeliitumia nafasi hiyo kwa kumtoa kwa mkopo ethan laird akapate uzoefu. Kuendelea kumtegemea brandon williams upande wa kushoto kama ni backup ya mgonjwa luke shaw itakuwa tunazidi kutengeneza tatizo (kwa sababu kiwango cha rashford hakieleweki)
 
Hata Ole mkuu anafuata mifumo ambayo ipo tayari, unaweza mchezesha pogba/bruno/Vdb labda timu pinzani imepaki basi unatafuta goli, ila unaCheza na Man City ama Liverpool then 6 Pogba ni majanga hayo.

Kuna kipindi Aliumia Mc tominay/pogba/matic na midfield wa kati akacheza perreira, tulikuwa tunafungwa kijinga sana, mpira ndio ulivyo.

Na ole amesema wapi atawachezesha wote watatu kwa mfumo wa sasa?
 
Nimeona tetesi za Man united kumtaka Alex Telles wa FC Porto
 
Kuna mfumo wanacheza wote watatu kwa pamoja,,
Matic anakuwa defensive midfielder na VDB anacheza kulia ,,pogba na Fernandez wanacheza kati,,
Tukishambulia VDB anaingia ndani,,
Na tukishambuliwa VDB anarudi kati ,,,mfumo huo upo na huwa wanacheza sn ktk attacking football,, especially timu ikitaka magoli zaidi..na kutawala mchezo zaidi,,
Hata PSG kuna kipindi Herrera anacheza kulia kama winger..wakikutana na timu sumbufu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…