Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mapungufu ya Paul ni ya kitabia zaidi ila kwa kiwango chake sioni mbadala wake kwa sasa tukienda sokoni bila kutoa pesa si chini ya $100M. Akiwa 100% fit anaweza kutoa mchango mkubwa sana ktk timu. Kitu cha kufurahisha ukiangalia takwimu zake toka tumemtoa Juventus miaka minne iliyopita ni zile zile wala hajabadilika hasa hasa msimu wa 2018/19 ndio msimu wake bora zaidi kitakwimu as a footballer ktk professional career yake.

Kitu kikubwa kilichomkwamisha Paul kwa kipindi kirefu sana Manchester United ya sasa imejaza wachezaji wengi sana ambao hawastaili kucheza pale. Na ndio maana utaona hata tukicheza na vitimu vidogo mechi inakuwa ngumu sana. Tofauti ya vitimu kama Southamptom au Sevilla au Leiceister ni jina la timu tu ila kiuhalisia wachezaji waliopo kwetu na kwao tunafanana nao tu.

As an individual, hawezi kubeba timu peke yake unahitaji uwe na wachezaji atleast watatu wa daraja lako ili muwe na nguvu ya kufanya maajabu. Juventus alizungukwa na watu wazito wengi alichokuwa akifanya kule ni hiki hiki tu tofauti ni quality ya watu aliocheza nao kule na huku. Juventus alikuwa akicheza na Andrea Pirlo, Paul Dyabala, Carlos Tevez, Arturo Vidal na Giorgio Chiellini hamna mchezaji wa kuunga unga hapa linganisha na aliokuja kucheza nao Manchester United.

Usisahau ubora wa timu ni collective responsibility. Individually kila mtu anaweza kucheza ila ili ufanye vizuri unahitaji watu kadhaa wa daraja la juu. Hakuna timu inayoshinda mataji bila kuwa na angalau wachezaji wa tatu wa kiwango kikubwa mno.
 
Asante sana Joh Doe. Binafsi nimekosoa kiwango cha pogba ndani ya united kwa kulinganisha na wakati wake pale juventus ingawa hapa umeisha pangua hoja kwamba hakuzungukwa na class players,lakini haiondoi ukweli kwamba kama unajua unajua tu. Angalia wachezaji wanaosemwa ni wa daraja lake kama kante,kdb,etc timu inakuwa haiko form lakini unaona uwanjani ni kama anacheza peke yake. Tabia hiyo pogba hana.

Kuna kufunga magoli lakini pia kuna kuwa bora miongoni mwa wote. Kwa united ya kipindi hiki kila anayekuja anaonekana bora zaidi ya waliokuwepo. Kuna wakati de gea alikuwa mchezaji bora wa timu karibu misimu 4 mfululizo,lakini alikuwa kwenye kiwango chake kweli. Ndio maana best 007 hamkubali lukaku pamoja na takwimu zake za magoli kisa hana ufundi wa mpira. Kwahiyo hizo takwimu hazitoshi kukosoa kwamba jamaa hajawahi kuwa na ubora aliotoka nao juve.

Work rate ya pogba akiwa juve na united ni tofauti. Kule alikuwa anakaba pamoja na kutengeneza nafasi lakini amekuja united amekuwa fadha kiasi kwamba anaona kukaba sio jukumu lake. Hapa nikiri kuwa mashabiki tumemuharibu naye akajifananisha na messi na ronaldo.
 
Nimetolea mfano mooyi kama midfielder wa timu za daraja la kati huwa wanampa tabu sana pogba. Mara nyingi sana anashindwa kumiliki sehemu ya kiungo kama tegemeo letu. Na sababu kubwa ni hajitumi vya kutosha.
 
Labda ile Akili yake mbovu aliyonayo ibadilike la sivyo atakuwa anajipotezea muda na hatofika anapotamani kufika. Na atakuwa mzigo pia kwa wenzake
Ukiangalia kwa umakini sana, Paulo amekuwa sababu ya udhaifu wetu eneo la kiungo ingawa hili halisemwi waziwazi kwa sababu zinazojulikana. Akiwa majeruhi,kiungo chetu chini ya matic,Fred na mctomminay kilikuwa kama kitu kimoja,na tulikuwa tunapata matokeo mazuri sana.
 
Mkuu mimi bado ninaamini hata msimu huu hatuko nafasi nzuuri sana kugombea taji,bali tunajenga timu. Hivyo tujipe muda maana kushoto bruno kuliko vdb hawa kwa kiasi kikubwa ni world class,tutegemee makubwa toka kwa pogba la sivyo tuwe na sababu ya kukubali man utd sio sehemu sahihi kwake pamoja na kipaji chake.
 
fuentte,

Hii comment yangu kama unaweza i-screenshot uje unitafute mwezi wa tano mwakani.

Utabiri wangu ni huu, kama Paul na Bruno wakacheza mechi zisizopungua 30 za ligi kuu msimu huu ukijumuisha Greenwood, Martial na Rashford kwa pamoja bila majeraha ya muda mrefu. Tuna nafasi kubwa sana ya kubeba ubingwa kwa zaidi ya asilimia 80%. Tuna mapungufu machache sana ya kuwekwa sawa hasa hasa beki wa kati kwa sasa. Golini sina mashaka Dean haondoki msimu huu anagombania namba na David.

Sisi changamoto yetu kubwa kwa sasa wachezaji wetu wengi muhimu huwa wanapata majeraha ya mara kwa mara. Kwa msimu uliomalizika juzi front 3's yetu yaani Anthony, 23 goals, Marcus, 22 goals, na Mason, 17 goals, wamefunga magoli mengi ( 62 goals) zaidi kuliko ya Liverpool (57 goals) yaani Mo Salah, 23 goals, Sadio, 22 goals, na Bob Firmino, 12.

Tofauti yetu sisi na Liverpool, wao huwa hawapati majeraha ya mara kwa mara ya wachezaji wao muhimu simaanishi labda sio bora hapana bali wanapata consistency ya wachezaji wao muda mrefu. Just imagine kama Liverpool Mo Salah na Virgil Van Dijk wakosekane angalau mechi 10 au 20 kila mmoja kama ilivyotokea sisi kwa Paul au Marcus Rashford au Martial.
 
Pamoja sana Mkuu Joh Doe. Binafsi ningependa iwe hivyo maana mbali na kuwa na mitizamo tofauti kuanzia kwa mchezaji mmoja mmoja,kocha na utawala wa juu,lakini wote lengo letu timu ibebe makombe turudi kileleni panapotustahili..

Timu yetu kwenye karatasi na kihistoria ni kubwa mara 2 ya city arsenal na Chelsea ukizijumlisha (hapa watabisha),ila napata shida kuamini ndani ya muda huu mfupi wa maandalizi watapata muunganiko mzuri kushinda mechi nyingi kirahisi. Kumbuka city na Liverpool wanaboresha padogo sana wakati sisi kila shabiki humu anafikiria usajili wa wachezaji kuanzia 4-5 wa kikosi cha kwanza. Hapo ndipo hofu yangu ilipo hadi naitoa united kwenye kulikimbiza taji msimu huu.

Pamoja na yote,UNITED WE STAND.
Asante kwa muda na uvumilivu wako hadi sasa.
 
Kila mara nasema, nje ya UK kuna wachezaji wengi tu wazuri na wana vipaji asilia na bei zao ni rafiki kwa soko.

Bruno na huyu dogo tumewaleta kwa bei nzuri tu. Na mishahara yao ipo chini kuleta wage balance.

Nadhani Ole angeanza na wachezaji wa aina hii.

Tusihangaike na waingereza wa bei ya juu.
 
Kweli kabisa na hata tm bora zaidi duniani ni zile ambazo hazina waingereza wengi.
 
Kwa usajili wa Van De Beek, naona tutakuwa tumeokoa Euro MIL40 kwa ajili ya eti yule Muingereza Grealish aliyepewa thamani ya Euro mil 80.
Maana naona jirani wenzetu pale London wameshapigwa mjini kwa Chillwell 50MIL 😀 😀 .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…