Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

IMG_9704.JPG
 
Hii timu ina wachezaji wamesajiliwa kwa pesa kubwa. Kisha wanaenda kupita mbele ya Copenhagen kwa penati.

Wanaanza game na Sevilla wanapata penati. Bruno Penalties akascore. Sevilla wakasawazisha kwa goli zuriiii halafu Pogba, Fred na Maguire wakamzunguka refa kudai lile siyo goli.

Hawakua na uhakika wa kurudisha goli ndiyo maana wakaanza kulilia lile goli likataliwe.

Mkuu sidhani walimzunguka Refa kwa sababu hiyo bali throw in ya upendeleo iliyopelekea goli. Mchezaji wa Seville aligusa mpira.
 
Bora mlivyo tolewa na Sevilla mngekutana na Inter mngepasuka vibaya sana,hii combination ya Lukaku na Martinez ni hatari,jana kila mmoja alitupia magoli mawili.
 
Usimfananishe Klopp na Sosha!

Klopp alipoteza 2 za UEFA (Bayern & Real Madrid) na katika michuano yote hiyo aliyopoteza timu yake ilionyesha kiwango kizuri japokuwa alikuwa na wachezaji wa kawaida.

Wewe umeshindwa kufika fainali, tena umetolewa na Sevilla, ukiwa na beki ghali duniani (Maguire) na kiungo ghali duniani (Pogba).

Mtu kama huyo hata tukisema tumpe Messi, Mbappe, Neymar, Ronaldo.. Hana atakachokifanya, usijidanganye!
Siwezi kukupinga mkuu! Kila mtu na mtazamo wake!
 
Tangu mwanzo nimekuwa nikiamini kuwa waingereza ndani ya united ndio kansa yenyewe. Angalia kuanzia mishahara yao,mikataba yao mirefu,back up wanayopata kutoka kwenye media za nyumbani,hawafanyiwi subs pindi wanapokuwa off na la muhimu kabisa hawana ufundi ndani ya uwanja.
Wakati mwingine naombea huyu Sancho naye deal lake life tupate talent ya America ya kusini au ulaya mashariki tutapona huu ujinga unaoendelea hapa
Talent nyingi za America ya kusini hazijawahi kuwa na mafanikio United na wengi huchelewa sana kusettle.
 
Back
Top Bottom