PTER,
Kwanini asiwe Dries Mertens au Raul Jimenez?
Nimemchagua Edin Dzeko kwa sababu namuona kama ni mshambuliaji mzoefu aliye sawa kwa sasa na anaweza kupatikana. Pia Edin ni mshindi, ni mchezaji anayeweza kucheza mahala penye pressure na panapohitaji makombe.
Edin, pia anaweza kuwa mwalimu wa hawa wapuuzi wawili (Marcus Rashford & Anthony Martial). Sioni kama tunaweza kuwa-offload tumejifunga nao kimikataba, so the best way forward ni kuwa-train tu wawe wazuri japokuwa so far sina imani nao tena tumewapa nafasi ila wametuangusha wana ujinga mwingi sana.
Hofu yangu kubwa sana watamfundisha hata Mason Greenwood kuwa mchezaji average kama wao. Kijana bado ana umri mdogo (18) anajifunza kutoka kwa wakubwa wake, kama una wakubwa wapumbavu ni kheri umtafute mkubwa mwenye akili ili aje kuwa role model kwa kijana huku akitusaidia ku-buy time muda tunatafuta mbadala wa kueleweka.