Bavaria,
Tuna mitizamo inayofanana sana, kuna kipindi niliwahi kuandika hapa kwamba sisi tuna watendaji wakuu wa juu wabovu sana wakiongozwa na Ed Woodward.
Ed, yupo smart on business persipective ila as a football executive ni hovyo sana. And worse part, board yetu nzima ina watu 12, sita ni familia ya Glazer na hawa sita wengine wakiwemo wakurugenzi huru wasio na uelewa na masuala ya mpira wengi ni watu wa mitindo na fedha. Just imagine una bodi ya wakurugenzi wanaojua kusoma financial statements na business strategy zaidi kuliko mpira. Ni sawa na kampuni ya mafuta na gesi au ya magari ijaze football executives ktk bodi yao.
Hii ndio bodi yetu ya wakurugenzi wanaoamua nani aje au nani asije maana ndio wanaoidhinisha cheque isainiwe na Ed Woodward. Hawa wanaamini kila tatizo ni kurusha pesa tu and they are not timely benchi la ufundi likitaka watu kwa wakati, hawa ndio wana-inflate hata viwango vya mshahara vya wachezaji. Mshahara wa kulipa watu wawili kama Bruno analipwa mchezaji mmoja, mwisho wa siku mnakuwa hamuwezi ku-accommodate vipaji vingi kwa wakati mmoja kila mtu anataka kulipwa sana.
- Ed Woodward - Makamu mwenyekiti nz & Mkurugenzi
Huyu hamna hata maelezo amefika nafasi hii kwa urafiki wa yeye na familia ya Glazer na sio kwa uwezo wake kama Peter Kenyon au David Gill. Ni mzuri kibiashara ila sio uendeshaji wa klabu ya mpira.
- Richard Arnold - Mtendaji mkuu & Mkurugenzi
Huyu amesoma darasa moja na Ed chuo kikuu cha Bristol 1990 -1993 (yeye ana shahada ya baolojia na Ed, fizikia) na wakaenda kufanya kazi pamoja auditing firm ya PwC baada kuhitimu chuo kikuu mwaka 1993 mpaka 1999. Hata mitihani ya uhasibu walifanya pamoja mwaka 1996. Amekaa hii nafasi kiushikaji, ni mshikaji wake toka ujanani. Uelewa wake wa mpira ktk bodi ni kama mshikaji wake ED tu, Don't bother to ask!
- Cliff Baty - Mkurugenzi/Fedha
Huyu sio tatizo, yeye ni fedha tu.
- Robert Leitão - Mkurugenzi huru
Uzoefu zaidi ya miaka 30 ktk masoko ya mitaji na uunganishaji wa mabenki, Nafasi yake ya kwanza kuwepo ktk bodi ya timu ya soka.
- John Hooks - Mkurugenzi huru
Umri wake miaka 62, uzoefu zaidi ya miaka 35 anafanya kazi ktk fashion. Nafasi yake kwanza kwake kuwepo ktk bodi ya timu ya soka.
- Manu Sawhney - Mkurugenzi huru
Umri miaka 51, zaidi ya miaka 26 ktk media, kidogo alikuwa mkurugenzi wa ESPN Star sports. Na yy same WhatsApp group na hao wengine.
Hoja yangu juu ya hawa wakurugenzi hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kusimama na kocha akihitaji watu kwa wakati ili awe fasta kufanya programmes zake. Mwisho wa siku analetewa watu nje ya wakati wengi hawaoni umuhimu wa kuwa timely ktk usajili. Ukiwa unavuta vuta kasi unafanya usajili when you're desperate kila mtu ana-take advantage unabambikiwa bei na unaleta mtu mmoja badala labda ya watu watatu.