Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

★Wamebana Wameachia

Napoli are reprortedly willing to sell Koulibaly for €70M + bonuses despite previosuly wanting up to €100M for the defender

#GGMU
 
Pale kwa maguire tulipigwa kabisa...halafu sioni sababu ya kocha kuhangaika na wachezaj wa kiingereza pale.....anapaswa kwenda ulaya mashariki na south america kuna vipaj ving sana tena kwa bei chee kabisa
Wachezaji wa kingereza wenye vipaji walishaisha enzi za kina Rooney na Beckham.

Waliobaki sasa ni walamba midomo tu.
 
Bavaria,

Tuna mitizamo inayofanana sana, kuna kipindi niliwahi kuandika hapa kwamba sisi tuna watendaji wakuu wa juu wabovu sana wakiongozwa na Ed Woodward.

Ed, yupo smart on business persipective ila as a football executive ni hovyo sana. And worse part, board yetu nzima ina watu 12, sita ni familia ya Glazer na hawa sita wengine wakiwemo wakurugenzi huru wasio na uelewa na masuala ya mpira wengi ni watu wa mitindo na fedha. Just imagine una bodi ya wakurugenzi wanaojua kusoma financial statements na business strategy zaidi kuliko mpira. Ni sawa na kampuni ya mafuta na gesi au ya magari ijaze football executives ktk bodi yao.

Hii ndio bodi yetu ya wakurugenzi wanaoamua nani aje au nani asije maana ndio wanaoidhinisha cheque isainiwe na Ed Woodward. Hawa wanaamini kila tatizo ni kurusha pesa tu and they are not timely benchi la ufundi likitaka watu kwa wakati, hawa ndio wana-inflate hata viwango vya mshahara vya wachezaji. Mshahara wa kulipa watu wawili kama Bruno analipwa mchezaji mmoja, mwisho wa siku mnakuwa hamuwezi ku-accommodate vipaji vingi kwa wakati mmoja kila mtu anataka kulipwa sana.

  • Ed Woodward - Makamu mwenyekiti nz & Mkurugenzi
Huyu hamna hata maelezo amefika nafasi hii kwa urafiki wa yeye na familia ya Glazer na sio kwa uwezo wake kama Peter Kenyon au David Gill. Ni mzuri kibiashara ila sio uendeshaji wa klabu ya mpira.

  • Richard Arnold - Mtendaji mkuu & Mkurugenzi
Huyu amesoma darasa moja na Ed chuo kikuu cha Bristol 1990 -1993 (yeye ana shahada ya baolojia na Ed, fizikia) na wakaenda kufanya kazi pamoja auditing firm ya PwC baada kuhitimu chuo kikuu mwaka 1993 mpaka 1999. Hata mitihani ya uhasibu walifanya pamoja mwaka 1996. Amekaa hii nafasi kiushikaji, ni mshikaji wake toka ujanani. Uelewa wake wa mpira ktk bodi ni kama mshikaji wake ED tu, Don't bother to ask!

  • Cliff Baty - Mkurugenzi/Fedha
Huyu sio tatizo, yeye ni fedha tu.

  • Robert Leitão - Mkurugenzi huru
Uzoefu zaidi ya miaka 30 ktk masoko ya mitaji na uunganishaji wa mabenki, Nafasi yake ya kwanza kuwepo ktk bodi ya timu ya soka.

  • John Hooks - Mkurugenzi huru
Umri wake miaka 62, uzoefu zaidi ya miaka 35 anafanya kazi ktk fashion. Nafasi yake kwanza kwake kuwepo ktk bodi ya timu ya soka.

  • Manu Sawhney - Mkurugenzi huru
Umri miaka 51, zaidi ya miaka 26 ktk media, kidogo alikuwa mkurugenzi wa ESPN Star sports. Na yy same WhatsApp group na hao wengine.

Hoja yangu juu ya hawa wakurugenzi hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kusimama na kocha akihitaji watu kwa wakati ili awe fasta kufanya programmes zake. Mwisho wa siku analetewa watu nje ya wakati wengi hawaoni umuhimu wa kuwa timely ktk usajili. Ukiwa unavuta vuta kasi unafanya usajili when you're desperate kila mtu ana-take advantage unabambikiwa bei na unaleta mtu mmoja badala labda ya watu watatu.
Tunaivunja nyumba yetu sisi wenyewe.

Kwa maneno mengine hizi porojo tunazopiga hapa ni geresha tu. Maana hakuna sehemu sauti zetu zitasikika.

Ole atafanya vibaya uwanjani, mashabiki tutaanza Ole out ilihali tatizo lipo kwa management.
 
Tungeongeza quality kwenye kikosi chetu,msimu ujao tungekuwa title contender mapema sana ila bodi inazingua

I'm pretty sure Liverpool na City hawatakuwa na same rythm na kama tuki-close gap kidogo tutaenda nao toe to toe
 
Liverpool walituacha 33 points

City walikuwa na msimu mbovu baada ya kukosa champions league they will come back stronger

Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
 
Liverpool walituacha 33 points

City walikuwa na msimu mbovu baada ya kukosa champions league they will come back stronger

Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
City wamekuwa na msimu mbovu pia kwenye ligi,wamefungwa mechi nyingi tu.

Tukiongeza quality kama tatu na Ole aka-up his game kidogo,we may challenge this..
 
City wamekuwa na msimu mbovu pia kwenye ligi,wamefungwa mechi nyingi tu.

Tukiongeza quality kama tatu na Ole aka-up his game kidogo,we may challenge this..
Licha ya kuwa wabovu still walituzidi 15 points Pep alifanya mistake ku-tofanya replacement ya Kompany na kumchezesha Fernandinho as CB

Baada ya kushinda kesi against UEFA they will spend more this season and they know how to spend
it's clear Sane,Silva,Garcia,Stones,Otamendi wanaondoka tayari wameshajili 2 players

Msimu huu muda wa preseason ni mchache sana EPL inaanza 12 September zimebaki siku 28

Liverpool,City, Chelsea walishafanya usajili wao muhimu as usual United will negotiate zaidi ya mwezi kusajili mchezaji mmoja

Tumecheza bila Pogba na Martial baada ya mechi chache tu za kwanza za msimu..na hapa ndo tulipoharibu..wangekuwa fit hilo gap lisingekuwa hivi..Either way,tunahitaji kuimarisha kikosi agressively
 
kila la kheri tahith Chong,
kipaji unacho ila ukazanishe mwili wako ili uje umuondoe goi goi asiyependa kudribble
1597575266559.png
 
Licha ya kuwa wabovu still walituzidi 15 points Pep alifanya mistake ku-tofanya replacement ya Kompany na kumchezesha Fernandinho as CB

Baada ya kushinda kesi against UEFA they will spend more this season and they know how to spend
it's clear Sane,Silva,Garcia,Stones,Otamendi wanaondoka tayari wameshajili 2 players

Msimu huu muda wa preseason ni mchache sana EPL inaanza 12 September zimebaki siku 28

Liverpool,City, Chelsea walishafanya usajili wao muhimu as usual United will negotiate zaidi ya mwezi kusajili mchezaji mmoja

Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
Msimu uliopita Man city walipoteza mechi nyingi kuliko tulizopoteza sisi ila sisi tulipata sare nyingi sana.

Reinforcement yetu inapaswa kuwa kwenye striking force na ndiyo tuna mapungufu makubwa sasa hivi akiumia Martial au Rashford hatuna mbadala wao. Hata wakiwa off form hatuna mbadala wa kutumia tunapaswa kuimarisha striking force yetu.
 
Back
Top Bottom