- sevilla wameshika nafasi ya tatu kwenye la liga
- sevilla wamefunga magoli 13 kwa njia ya set pieces
- wameruhusu magoli 34 kwenye mechi 38 za la liga
tatizo lao kubwa lipo kwenye ufungaji na sababu kubwa ni aina ya midfield walionao (wanacheza 4-3-3) contributions yao ni ndogo sana eneo la ushambuliaji ila ni wazuri sana kwa kuharibu mipango ya adui wakiongozwa na ever banega.
Lopetegui ni mwalimu anayeamini sana possession (tunapaswa tujiandae na mapema yasije yakatukuta ya southampton), udhaifu wa midfields wao kwenye utengenezaji wa nafasi kunawalazimisha sevilla wategemee zaidi miujiza ya wachezaji wao wa pembeni (tukicheza walinzi wanne yule williams atakuwa na kazi ngumu sana ya kumzuia jesus navas).
pia washambuliaji wao si wazuri sana kwa kumiliki mipira hivyo basi tunapaswa kuutumia udhaifu huo pamoja na udhaifu wa midfield wao.
cha muhimu zaidi ni kujiamini na kumchunga zaidi ocampos