Tatizo letu kubwa wachezaji wa kingereza ndo wanaleta inflation pale united. Tunauabudu uingereza kuliko mahitaji ya timu.
Haiingii akilini unamnunua Maguire kwa £80M wakati ulikuwa unaweza kupata option nyingine kwa nusu bei. Unamuongeza mkataba Phill Jones, unashindwa kumuuza Jesse.
Matatizo yalianza pale unapompa Rooney 250K kwa week. Kutoka hapo kila mmoja lazima atake cha juu. Hadi DeGea sasa anataka mshahara mkubwa na kuleta uzembe wa kijinga.
Management ya United ivunjwe, iletwe mpya, wachezaji washushwe mishahara. Atakaetaka kubaki abaki, anaetaka kuondoka mlango uwe wazi. Recruitment staff walete wachezaji wanaohitajika kwa bei sahihi na aletwe kocha sahihi.
Tofauti ya hapo tunageuka kuwa Liverpool mpya.