nadhani ishu ya uhitaji (demand) na uzalishaji (supply) inahusu zaidi kwenye hili sakata linalowahusu wachezaji wa kiingereza.
ni mara chache sana kukuta waingereza wanazalisha wachezaji wenye vipaji kwenye mashamba yao (academy) ukilinganisha na mataifa mengineo kama spain, brazil, germany ya miaka 10 hii ndio maana ikitokezea kipaji kimezaliwa ndani ya ardhi yao thamani yake inakuwa ni kubwa sana ukilinganisha na nchi nyenginezo.
halafu hii sheria ya kila timu lazima iwe na wachezaji takribani 8 wazawa wa uingereza ndio inazidi kuchochea wachezaji wao kuwa ghali kwa sababu unakuta kila timu inawahitaji (demands) ndio maana timu zinakuwa na jeuri kwenye mauzo.
===========================
pia media zao pamoja na wachambuzi wao wa soka kwa mapenzi yao binafsi ya timu zao walizowahi kuzichezea pamoja na utaifa wao kwa kiasi kikubwa wanawafanya raia wao wawe na sifa takribani tatu.
- wawe na gharama kubwa unapowahitaji hususani timu kubwa.(overpriced)
- wengi wao wanawapa sifa nyingi pasina ukweli wa sifa hizo.(overrated)
- wanawatangaza sana japokuwa si vibaya kwa sababu ni wachezaji wa nyumbani (overhyped)
binafsi sichukizwi na wachezaji wa kiingereza (wawe technically gifted or talented) ambao wana kitu muhimu zaidi wanachoweza kukupa ndio maana sijawahi kuwaponda wayne rooney, paul scholes, steven gerrard, frank lampard, joe cole, ferdinand, terry, robbie fowler, michael owen, shearer, andy cole na wote hao nimewashuhudia wakicheza tokea mwaka 2001.
nachukizwa na wachezaji wale wasiokuwa na maajabu makubwa ya kisoka either technically or talent halafu wakaongozwa na gharama kubwa sana za kihuduma (mshahara na fedha ya usajili)
jaribu kuangalia timu kama barcelona na bayern munich zote hizi kwa miaka mingi zimejaza wachezaji wazawa lakini wenye uwezo wa kujisimamia bila ya kutegemea msaada mkubwa kutoka kwa wageni tofauti na wachezaji wengi wa kiingereza waliojazana kwenye vilabu unakuta wengi wao wanasukumwa zaidi na uwepo wachezaji wa kigeni (mfano henderson na chamberlain wanachezea timu bora kwa sasa lakini uwezo wao ni wa kawaida sana)
=========================
asikwambie mtu hakuna kazi ngumu kama kulea mtoto ndio maana team nyingi huamua kutumia shortcut ya kusajili mchezaji aliyekwisha kuwa tayari kimapambano, ndio maana tulimsajili harry maguire, wan bissaka, pia tunavumishwa na usajili wa grealish, maddison, sancho licha ya kwamba tuna vijana wengi wa kiengereza kwenye academy.
kivyovyote wachezaji wa kiengereza hawaepukiki ndani ya manchester united,
tusisahu watoto wa kiengereza wanakupa ulinzi