Mkuu umechambua vizuri, kuna wakati kama namuona Damushin ndani yako
Back to the point
Sijui kwanini watu tafsiri ya vipaji vya soka, ni visigino, kuendesha baiskeli, kupiga pasi kulia huku unaangalia kushoto, na mbwembwe za kila aina.
Kwa tafsiri hii, Paul Scholes, Frank Lampard, Steve G., Mark Hughes, Andre Cole, pengine hata Waza wanaonwa kama hawana vipaji halisi. Kwa tafsiri ya wadau wenye mtazamo huo mtu kama Joe Cole au Ricardo Quaresma are more talented [emoji23] kuliko hao niliowataja. Naamini dribbling is a talent, scoring is a talent, defending is a talent, passing is talent. Tunaweza kuwaona wachezaji wa beach soccer wanavyowazidi talent akina Scholes[emoji1] (kwa mtazamo ule)
United ninayoijua imejengwa na Waingereza wa kutosha kwa kuchanganya na vipaji kutoka nje ya nchi. Kuanzia United ya akina Bob Charlton, George Best, Mark Hughes, Scholes, Waza mpaka ya akina Rashford na Greenwood zote zimejengwa kwa mfumo huo.
Watu wa nje ambao wamesaidia kuweka United kwenye ramani ni akina Cantona, CR 7,wachache sana. Hata ile Greatest United of all times kwa kigezo cha mafanikio, Treble Winners ilijengwa na hawa hawa Waingereza (Uingereza means, UK in this respect wakuu). Hivi tunaamini kabisa out there kuna akina Bruno weeeeengi [emoji23], tuache kujidanganya.
Nadhani tumeipenda United kwa sababu, ndio maana hatuipendi Flamengo, Boca Juniour, Sporting Lisbon, Barca, pengine hata Arsenal ya Wenger (najua baadhi yetu waliipenda United kipindi Guners ya Wenger inaupiga mwingi sana)
Wakati huo huo timu za EPL zinalazimishwa kuwa na wachezaji angalau 8 waliokulia Uingereza (ambao majority ni Waingereza) kati ya 25 kwenye kikosi kizima. Je tunataka kutii hiyo sheria kwa kuwa na akina Lingardinho, Phil Jones, sidhani kama hilo ni sahihi, nadhani tunahitaji wachezaji kama Grealish, namuona Grealish ni Creative sana, anapaswa kupunguza kukaa na mpira bila sababu, basi.
Grealish hawezi kuuzwa United kwa hiyo bei ya £80m, na United ya sasa sio ya kumwaga mapesa, kwanza kutokana na sera mpya (marufuku kulipa zaidi ya thamani halisi), pili kwa kuwa Villa wanashuka daraja na tatu sababu ya Corona. Ed akilipa hata £60m kwa Grealish nitamshangaa sana labda iwe kwa mfumo wa add ons.
Jambo la mwisho, wakuu tusibweteke, City wananyanyasa pale uingereza kwa sababu hawajabweteka. City yenye Sane, D. Silva, B. Silva, Sterling, bado ikamuongeza Mahrez, hapo walikuwa wanajua wana kijana anayekuja kwa kasi anayeitwa Foden.
Sisi tuna Bruno, tusione tumemaliza wakuu. Juzi kati nilisikia watu wanasema eti hamna haja ya United kununua striker eti yupo Greenwood, nikacheeka sana. HIZI TIMU KUBWA ZINAFANIKIWA KWAKUWA HAZIOGOPI KUSAJIRI ILI KUMFANYA MCHEZAJI ALIOPO AJISIKIE VIZURI. Katika kiwango cha juu alichokuwa nacho Berbatov, lakini UCL final ya mwaka 2008 hakuwepo hata benchi, sababu ya kuwa na squad iliyosheheni vipaji.
Bavaria,
Una mtizamo sawa na mimi. Vipaji vya kiingereza huwa sina imani navyo kabisa, hawa mimi ktk recruitment model yetu ninge-wawekea red flag unless wawe highly recommended na technical team ndo nawasajili. Nje ya hapo ningekuwa nawapandisha kupitia academy system kama Mason Greenwood na Marcus Rashford.
Tunapaswa tutafute vipaji nje ya hawa waingereza kama tulivyofanya kwa Bruno. Binafsi naona waingereza wanakuzwa mno kuliko thamani yao na uwezo wao halisi pia. Mfano halisi ni huyu huyu Jack Grealish ana thamani kubwa kuliko hata Bruno Fernandes,
Comparisons;
| Jina | Grealish | Bruno |
| Umri | 24 | 25 |
| Nafasi | Kiungo Mshambuliaji | Kiungo Mshambuliaji |
| Msimu huu | Mechi 33 Magoli 7 Assists 6 | Mechi 10 Magoli 7 Assists 6
Mchezaji bora wa mwezi (Feb, June) |
| Tuzo | 0 | Mchezaji bora ligi kuu ya Ureno(2018,2019)
Mchezaji bora wa Ureno, 2019 |
| Timu ya taifa | Hajawahi kucheza | Mechi 19 Goli 2 |
Sasa jiulize inakuwaje mchezaji mwenye uwezo mdogo kama Grealish kumlinganisha na Bruno, thamani yake iwe Pound 80M na Bruno Pound 67M? Nimeona watu wanasema ni backup ya Bruno, C'mon buddies! Kwa maamuzi haya sioni busara ya matumizi ya pesa. Huwezi kununua mchezaji wa backup kwa pesa nyingi kuliko mchezaji wa kikosi cha kwanza. Hii Pound 80M ni kheri tuwape scouts wetu assignment watuletee kipaji kinachoendana na hiyo thamani.
Kama Bruno tumempata kwa Pound 67M, vipi kuhusu Pound 80M (Aston Villa wanayotaka tuwape)? Hii assignment wanapaswa kupewa hao hao scouts walio-file report Bruno watuletee mtu mwenye thamani halisi ya P80M. Hata Jadon Sancho Burussia wame-inflate thamani yake halisi. Hata James Maddison same WhatsApp group, they are all inflated.