Matic na Fred wanacheza tofauti sana mkuu
Matic ni more holding mid, anamzunguka zunguka mbele ya namba 4 na 5 na mara chache hufika mbele ya upande wa namba 3 na namba 2
Matic ni more stationary. Ni disciplined mid. Ni aina ya viungo ambao ni bora kwenye ku intercept kuliko kupokonya mpira kwenye man to man batle. Kazi kubwa ya jamaa ni ku control tempo ya game na kulinda ukuta wake usifikiwe kirahisi na timu pinzani.
Ni mid (kwenye 3 ya kati) anayecheza vizuri akiwa na viungo 2 wa juu wanaoweza ku possess mpira zaidi
Fred hata na Scot ni aina ya viungo wazururaji. Ni viungo wenye uwezo wa kukaba lakini ni box to box mids, sekundi ya 16 anaokoa kwenye penati box yake, sekunde ya 26 unamkuta kwenye timu pinzani akijaribu kufunga au akitoa assist.
Fred na Scoty ni aina ya viungo ambao ukiwapa kazi ya kumbughuzi star wa timu pinzani, hufanikiwa sana. Hawa huwa ni less disciplined kwenye positioning. Unaweza kupata magoli mengi kutoka kwa mids wa aina hii kuliko mid ya aina ya Nemanja.
Viungo sampuli ya akina Fred sio wasomaji wazuri sana wa mchezo lakini flexibility yao na agility yao inakupa dimension tofauti kwenye game katika kukaba na kushambulia. Akina Fred na Scoty wanakupa pass nyingi za mbele kuliko square na back passes.
Naona kila kiungo na kazi yake pale United, kutegemea na aina ya matokeo tunayotaka, mpinzani tunayekutana naye na individual quality ya timu pinzani.
✓Bruno Fernandes inabidi arelax muda mwingine,..anafanya mambo kwa papara sana yanayopelekea kuwa na sloppy result
✓Nadhani mtakuwa mmeelewa ni kwa nini nilisema Matic ana kitu ambacho Fred na Scot wamenyimwa
✓Lingard,Dalot,Mata,Jones,Perreira...Hawa inabidi waondoke tuchukue replacement za bei rahisi zenye uhai kushinda wao..Cantwell,Grealish type of things