Dean Henderson zaidi ya De gea aisee hata gharama naona ndogo ukilinganisha na kazi hiyo
sidhani kama ameshafikia level ya kulinganishwa na david degea hata kama tutaamua kutumia kigezo cha kuangalia performance dhaifu ya david kwa miaka hii miwili (2019 and 2020).
namhurumia sana dean henderson pamoja na familia nzima ya kiengereza ilio nyuma yake (waingereza wanatamani kikosi chao kizima kijengwe na timu kubwa na si everton na wengineo), dean ana ndoto ya kuona siku moja anasimama kwenye milango ya old trafford kabla ya world cup ila sidhani kama itawezekana kwa sasa.
asikwambie mtu unahitaji kuwa na roho mbaya kama bolo yeong, roho ya kijinga kama arturito pindi unapochukua uamuzi wa kumfanyia mabadiliko ya kudumu goalkeeper wa kikosi cha kwanza.
kabla ya kumuangalia kwanza dean unapaswa ugeuze jicho lako kwa david, je ataelekea wapi kwa sasa pindi utakapomfanyia mabadiliko?
PSG, Real Madrid, Juventus, Newcastle?
david ana mkataba wa takribani miaka 3 na kwa mshahara anaolipwa haitokuwa rahisi kumweka benchi kwa miaka mitatu.
wafanyiwe match rotation?
hmmmm! ukitaka kujua madhara yake basi muulize manuel neur pale bayern munich, huyo mzee ameweka mkwala mzito baada ya bayern kumsajili goal keeper wa schalke 04.
============
halafu kuna balaa hili:
fred + scott + matic
corona imemuokoa paul pogba