Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Schmeichel kuhusu DDG na Dean .

Ni mapema sana kwa Manchester United kufikiria kumbadili kwenye jezi namba moja Davidi De Gea kwa ajili ya Golikipa wao aliye kwa mkopo katika klabu ya Sheffield United, Dean Henderson, kwa mujibu wa Peter Schmeichel .

Huku kiwango cha De Gea kikionekana kuyumba katika misimu miwili ya hivi karibu na Henderson akionesha kiwango kizuri kumekuwa na hoja za Muingereza huyo kuchukua nafasi ya Muhispania .

Peter Schmeichel hana hofu kuhusu uwezo wa Henderson lakini uhalisia wa kuwa namba moja wa Man United kuna vigezo vingine lazima viangaliwe .
.
. “ Kuna mtu yoyote anafikiria kutokuwa na David De Gea golini na nafasi yake achukue Dean Henderson sasa hivi ? Hakuna shaka kuhusu uwezo wa Henderson lakini amecheza msimu mmoja katika klabu ambayo imekuwa na msimu mzuri ndani ya Ligi ya Uingereza “ .
.
. “ Henderson atahitaji kuonesha msimu mwingine kama huu ambao ameibuka, halafu na mwingine na mwingine tena , ili kumshawishi kila mtu kwamba ni kipa sahihi . “ .
.
. “ Kuna utofauti mkubwa sana baina ya kuwa namba moja katika dimba la Bramall Lane na kuwa namba moja Old Trafford , tofauti kubwa sana. Hata kuwa mchezaji tu wa ndani kuna tofauti ya hivyo vilabu viwili “ .
.
. “ Nimeona watu wengi sana ambao wamekuja Old Trafford na rekodi zao , wafungaji magoli lakini wakashindwa kufanya kile walichoahidi kufanya kwa kuangalia viwango na vipaji vyao . Hiyo ni kwasababu presha ya Old Trafford ni tofauti , ni kubwa sana unajua “ .
.
. “ Kwa mfano kama Henderson akifanya kosa - naweza kukumbuka lile kosa dhidi ya Liverpool , itakuwa aaah sawa , bado mdogo na blah blah blah nyingi kwasababu anacheza Sheffield . Kama akifanya kosa Old Trafford akiwa na Manchester United basi itakuwa kichwa cha Habari hiyo , na itakuwa wiki nzima mpaka itakapokuja mechi nyingine , ambapo watu watakuwa wanahoji kuhusu uwezo wake . “ .
.
. “ Kwahiyo swali , De Gea au Henderson ? Kuna jibu moja tu hapa sasa hivi “
 
Nilikuwepo nimeisahau hii ahsante kwa kunikumbusha mkuu.
Man United vs Real Madrid Ronaldo aliwafunga United robo finally UEFA Champions League.

Kocha wa Man United alikuwa Sir Alex Ferguson Madrid alikuwa Jose Mourinho.

Mwamuzi wa mechi hii alikuwa Cuynet Cakir.

Madrid alifunga magoli yake baada ya Luis Nani kutolewa kwa red card ya hovyo kabisa kuwahi kutokea kwa kumchezea Faulo Alvaro Albeloa.

Real Madrid wakawa knocked out kwenye Semi final na Borussia Dortmund.

Ronaldo hakushangilia lile goli.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ili uwe Legend kwenye Timu flani unataka kusema sababu Moja wapo haitakiwi kuifunga Timu ulotoka na Ukashangilia???
Afu tukichukua Records zake CRISTIAN RONALDO Kuifunga Manchester United almost ni 2 times kushangilia 1 time kwanini Sababu moja ifute Mazuri ya mtu aloyatenda kwa kipindi kirefu tena Mazuri ya Kufurahisha Juu yetu na Team Pia.
Mimi namuona ni mtu aliyekuwa hana loyalty kwa ile timu. Alipotufunga akiwa Madrid hakushangilia nadhani alifanya vile kwa kuwa alijua hafahamu kesho yake, ila alipotufunga akiwa Juventus naamini alishangilia sana kwa sababu ashajua uwezekano wa kesho yake kuwa Man U ni kama Mdogo au hakuna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wadau,
Naona baada ya ligi kusimama mada zimekuwa chache sana na zinachukua muda mrefu kubadilika,omba uwe na uwezo wa kuitetea mada yako hadi mwisho.
Kuhusu hii habari ya ulejendari,kunakuwa na vigezo vingi vinavyotumika kumpa mtu hii hadhi. Ni kama alivyo ainisha mkuu Daemusin kwenye kigezo cha muda wa kuitumikia klabu,mchango wa mchezaji wakati yuko klabuni,uaminifu wake kwa klabu tangu anacheza na hata anapokuwa amehama au kustaafu lakini la msingi zaidi ni namna mchezaji anavyowakaa mashabiki mioyoni.
Kwa mtizamo wangu mimi simchukulii cr7 kama lejendari wetu kutokana na namna alivyofosi kuondoka utd kuelekea madrid maana alikuwa anaionyesha dunia kuwa utd si kitu mbele ya madrid.
 
Mtazamo wako ukoje kuhusu nani zaidi kati ya hizi timu mbili?
Inategemeana na wakati.
Kwa miaka mingi sana tumekuwa tukimpumulia madrid kwenye suala la mapato.
Na kwa upande wa mafanikio ya uwanjani united ilikuwa juu ya madrid kipindi cr7 anaelekea kule,
Madrid alisotea champions league kama liverpool na epl tu.
 
Rejea records zako bosi.

Au uniambie kuanzia kipindi hiki mpaka hiki Man Utd alikuwa juu ya Madrid, na kuanzia hapa mpaka hapa Madrid alikuwa juu.
 
Rejea records zako bosi.

Au uniambie kuanzia kipindi hiki mpaka hiki Man Utd alikuwa juu ya Madrid, na kuanzia hapa mpaka hapa Madrid alikuwa juu.
Kuanzia 2008-2011 utd alikuwa juu ya madrid na ndicho kipindi ambacho ronaldo anakomalia kwenda madrid
Na kwenye habari ya makombe tangu 2002 hadi 2009 man utd alikuwa amebeba mara moja na mshindi wa pili mara 2 wakati madrid alikuwa amebeba mara moja tu na hakucheza fainali yeyote hadi 2014.
Kimsingi Ronaldo aliyetengenezwa na man utd ya fergie ndiye alienda kufufua uhai wa madrid kwenye champions league.
Tulimuuzia adui silaha.
 
Ni 4 years span, na vipi Madrid amekuwa juu lini mpaka lini?
Don Clericuzio nilikuwa najibu hoja yako kuwa kwa kuangalia kipindi ambacho ronaldo anakomalia kwenda madrid kwa kuiona ni klabu bora zaidi ya united kwa kipindi hicho kama ulivyoniuliza awali.
Hata hivyo 2015,2017 na 2018 united alikuwa anatawala kwa utajiri ingawa sio kipindi tunachokijadili kwa sasa.
 
Kwa mtazamo wako, unadhani kama Ronaldo angebaki Man Utd angeweza kupata mafanikio sawa na aliyoyapata akiwa Real Madrid? Hapa nazungumzia mafanikio ya timu na mafanikio binafsi.

Kwa mtu ambaye ana mtazamo wa kuwa mchezaji bora duaniani kwa kipindi kirefu, lazima angewaza zaidi kwenda Madrid au Barca kwa sababu malengo ya hizo timu ni pamoja na kuwa on top kila wakati, hivyo zitafanya kila linalowezekana kuhakikisha zinakuwa na world class players na coaches as well. Hivyo Ronaldo aliliona hilo.

Man Utd ya 2008 ilikuwa inabebwa na philosophy za Fergie, na muda wowote ambao Fergie angestaafu Man Utd ingekuwa average team (nazungumzia kidunia in terms of performance). Na Man Utd pamoja na kuwa juu, haikuwa na utaratibu wa kusajili wachezaji wakubwa kutoka team zingine, hivyo Ronaldo aliona aende mahali ambapo atapata wasaidizi wengi kurahisisha kazi yake na kufikia malengo yake kirahisi.

Mind you, hakuna timu EPL inaweza kumnyanganya Barca au Real mchezaji wake bora, ila wao wanaweza kuja kubeba mchezaji yeyote wanayemtaka. Na hii imekuwa hivyo toka nimeanza kufatilia mpira (more than 25 years).

Sasa hapo niambie, mafanikio ya timu kifedha unayatafsiri vipi?
 
Don hii mada ni ndefu mno maana tukimaliza kipengele hiki,tutahamia kingine.
Ninachoweza kusema tu,usajili wa galacticos ndio ulikuwa unaamua hatima ya chaguzi za marais wa vilabu vya madrid na barca hivyo basi ilikuwa hata ikitumika michezo michafu kulifanikisha hilo.
 
Ili uwe Legend kwenye Timu flani unataka kusema sababu Moja wapo haitakiwi kuifunga Timu ulotoka na Ukashangilia???
Afu tukichukua Records zake CRISTIAN RONALDO Kuifunga Manchester United almost ni 2 times kushangilia 1 time kwanini Sababu moja ifute Mazuri ya mtu aloyatenda kwa kipindi kirefu tena Mazuri ya Kufurahisha Juu yetu na Team Pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ronaldo aliishi vema OT na hadi anaondoka aliendelea kupendwa, hilo alipaswa kuliheshimu,kuwaheshimu mashabiki na kuiheshimu timu. Hakuwa na haja ya kushangilia,labda kama angeondoka kwa matatizo na labda mashabiki kumtukana n.k lakini haikuwa hivyo. Huwa naamini kwamba CR hakushangilia tulipocheza na Madrid kwa sababu hizi mbili, 1. Hakuwa na uhakika na future yake mana umri ulikuwa bado, hivyo alijua professional ly lolote lingetokea mbeleni pengine kuna siku angerudi kuwa mchezaji wa Man U
2. Ronaldo anamheshimu sana Fergie na si Man U

Na huwa naamini alishangilia akiwa Juve kwa sababu alijua uwezekano wa kucheza tena Man U ni Mdogo sana au haupo mana umri ushakuwa jioni. Hivyo hii inaonyesha wazi kwamba kati ya C. Ronaldo na washabiki wa Man U kuna upendo wa kinafiki ambapo upande mmoja washabiki wanampenda CR kwa kuamini anawapenda na kuipenda timu yao ilihali CR yeye anajua Man U alipita tu,destination yake ilikuwa R. Madrid na upendo Mkubwa upo huko
 
True legends ni wale ambao hata baada ya maisha yao ya soka bado wapo connected na sisi..Huyu Ronaldo IMO sio our true legend..Paul Scholes,Roy Keane,Ferdinand,Evra n.k hawa ndo wamba ambao ukisema ni malegend atleast una make sense..

Huu ni mtazamo wangu
Paul Scholes,Patrice Evra,Roy Keane,Evra wote walishastaafu kucheza football na wengi bado wanafukuzia kazi kwa Woodward Christiano Ronaldo alikuwa professional player Real Madrid now yupo Juventus hawezi kuanza kuizungumzia timu ambayo haijamuajiri kwa sasa lazima aheshimu mkataba alio nao
 
Ronaldo aliishi vema OT na hadi anaondoka aliendelea kupendwa, hilo alipaswa kuliheshimu,kuwaheshimu mashabiki na kuiheshimu timu. Hakuwa na haja ya kushangilia,labda kama angeondoka kwa matatizo na labda mashabiki kumtukana n.k lakini haikuwa hivyo. Huwa naamini kwamba CR hakushangilia tulipocheza na Madrid kwa sababu hizi mbili, 1. Hakuwa na uhakika na future yake mana umri ulikuwa bado, hivyo alijua professional ly lolote lingetokea mbeleni pengine kuna siku angerudi kuwa mchezaji wa Man U
2. Ronaldo anamheshimu sana Fergie na si Man U

Na huwa naamini alishangilia akiwa Juve kwa sababu alijua uwezekano wa kucheza tena Man U ni Mdogo sana au haupo mana umri ushakuwa jioni. Hivyo hii inaonyesha wazi kwamba kati ya C. Ronaldo na washabiki wa Man U kuna upendo wa kinafiki ambapo upande mmoja washabiki wanampenda CR kwa kuamini anawapenda na kuipenda timu yao ilihali CR yeye anajua Man U alipita tu,destination yake ilikuwa R. Madrid na upendo Mkubwa upo huko

Huwezi kuitengenisha Manchester United na Sir Alex Ferguson ,SAF ameplay part kubwa sana kwenye mafanikio ya Manchester United ndio maana baada ya kustaafu timu inazidi kupotea
 
Hata Evra alihama akaenda Juve,Hata Rooney alihama akarudi Evertoon..

Hili ni swala subjective..kila mtu abaki na anachokiamini

Mimi naamini Legend akitajwa,jina la klabu moja linajitokeza automatically

i.e Ukisema Lampard-Watu wataiona Chelsea

Ukisema Gerald-Watu wataiona Liverpool

Ukisema Drogba-Watu wataiona Chelsea

Ukisema Company-Watu wataiona Man.City

Ukisema Giggs-Watu wataiona United

Hivyo ndo inavyopaswa iwe in my opinion
Nakupa list ya baadhi ya wachezaji/makocha ni legends kwenye klabu zaidi ya moja

Edwin Van der Sar-Ajax,Manchester United
Marco Van Basten -Ajax,AC Milan
Dennis Bergkamp-Ajax,Arsenal
Frank Rijkaard-Ajax ,AC Milan
Ronaldo de Lima-Barcelona,Inter Milan
Zinedine Zidane-Juventus,Real Madrid
Jose Mourinho-FC Porto,Chelsea
Johan Cruyff-Ajax,Barcelona
Jurgen Klopp-Dortmund,Liverpool
 
Nimesema ninachokiamini mimi..

Sababu hakuna formula ya kusema let say straika akifunga goli mia anakuwa ndo legend
 
Huwezi kuitengenisha Manchester United na Sir Alex Ferguson ,SAF ameplay part kubwa sana kwenye mafanikio ya Manchester United ndio maana baada ya kustaafu timu inazidi kupotea
Basi mimi ninachoamini ni kwamba CR alikitenganisha hiki kitu Man U na mtu Sir Alex Ferguson! Na inawezekana kabisa mtu akamheshimu Ferg na asiiheshimu timu. Na ninachoamini CR asingeshangilia kamwe goli la kuifunga United kama timu ingekuwa chini ya Fergie na yote hiyo nini kwa sababu anamheshimu zaidi.
 
Back
Top Bottom