Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Endapo mchezaji akicheza miaka 16 kwa kiwango cha juu, miaka nane kwa klabu moja na mingine nane kwa klabu nyingine. Mchezaji huyo azipe mafanikio klabu zote mbili, anakua sio lijendi simply kwa sababu amechezea vilabu viwili tofauti ?
Kwaiyo kwa maana hiyo ulijendi ni kutokuhama... ?
Au niulize kwa mujibu wako, muda mrefu ni kuanzia miaka mingapi ?
Tolea mfano wa mchezaji wa namna hyo
 
Kwahiyo
David Beckham
Jap Stam
Ronaldo na Owen Hagreaves siyo legends ila Phil Jones na Chris Smalling ni legends right ,?
Hili swala inabidi liwe subjective..na ndo maana kila mtu ana mtazamo wake

Kigezo changu ni kifupi tu..Kucheza kwenye kiwango cha juu na kujituma sana no matter what kwa muda mrefu kwenye klabu moja na kuiletea mafanikio..na naamini mchezaji hawezi kuwa legend wa klabu mbili tofauti..that's me

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si ndio Ronaldo mkuu... Tunataka mfano gani mwingine ?
CR amechukua vikombe kama 8 au 9 hivi ikiwepo UEFA CL 1 akiwa Man U ila amechukua vikombe 17 au 18 hivi yakiwemo makombe 4 ya UCL akiwa Madrid. Amekuwa ballon d'or winner Mara moja akiwa Man U lakini amekuwa balon d'or winner Mara 4 akiwa Madrid. Kwetu amecheza misimu 6, Madrid misimu 9 kama sikosei. Amewafungia real Madrid magoli kama 450 hivi, na Man U magoli 118 au 119 hivi. Bado sisi tunaona huyu kijana ni true legend wetu kuliko Madrid?
 
Niwe mkweli tu toka yupo united hajawahi niingia moyoni

Na bado akatufunga tulipocheza na juventus na akashangilia vizuri tu utadhani alizwa kwa lazima na klabu wakati yeye ndio alilazimisha kuondoka. Hata El Clasico ya mwisho hapa alienda kuitazama ila sijawahi ona amesafiri toka Madrid au Turin kwenda OT kutazama derby yoyote, hii ni wazi anaipenda na kuithamini R. Madrid kuliko Man U. Yawezekana CR7 anaipenda R. Madrid siyo Manchester United, ila anampenda Ferguson kuliko kocha yeyote aliyewahi mfundisha
 
Kweli toka aondoke ot hajawahi kanyaga tena kutazama hata mechi ya kirafiki
Na bado akatufunga tulipocheza na juventus na akashangilia vizuri tu utadhani alizwa kwa lazima na klabu wakati yeye ndio alilazimisha kuondoka. Hata El Clasico ya mwisho hapa alienda kuitazama ila sijawahi ona amesafiri toka Madrid au Turin kwenda OT kutazama derby yoyote, hii ni wazi anaipenda na kuithamini R. Madrid kuliko Man U. Yawezekana CR7 anaipenda R. Madrid siyo Manchester United, ila anampenda Ferguson kuliko kocha yeyote aliyewahi mfundisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi huwezi kuwa legend kwa team zaidi ya moja
  • labda tukisema sir alex ferguson ni legend wa Aberdeen na man utd itakuwa si sahihi, au aberdeen hawana haki ya kumshukuru sir alex ferguson kwa mafanikio aliowapatia?
  • tukisema kenny daglish ni legend wa blackburn rover, celtic na liverpool tutakuwa tunakosea?
  • hivyo hivyo kwa ronaldo
kama tunaiangalia tafsiri ya legend kwa kigezo cha umri na kuhudumu klabu kwa muda mrefu basi ronaldo hawezi kuwa legend kwa sababu ameondoka man utd akiwa na miaka 24 (amedumu klabuni miaka 6, miaka mitatu ya mwishoni akiwa kwenye ubora, nguvu kubwa zaidi aliitumia real madrid ndio maana si ajabu alikwenda kubeba tuzo lukuki huko spain), tofauti na wayne rooney aliyeondoka klabuni akiwa na miaka takribani 30, miaka yake 12 akicheza soka la kiwango cha juu tofauti na CR7 tuliyemvumilia kwa miaka takribani miwili hadi mitatu

kama tunauangalia mchango wa mchezaji husika basi ronaldo anaingia katika kundi la wachezaji muhimu zaidi kuwahi kutokezea ndani ya klabu kama wengineo (tulishinda makombe matatu mfululizo ya ligi kuu huku yeye akiwa ni tegemezi, tumecheza mara tatu mfululizo nusu ya fainali ya champions league na kubeba ubingwa mara moja)

kuhusu ishu ya nidhamu hata hao wengineo mfano paul scholes, rooney, giggs, cantona, roy keane, david beckham kwa nyakati tofauti waliwahi kuonyesha matendo maovu dhidi ya klabu kwa sababu zao binafsi kama vile ishu ya mkataba, kulinda heshima zao (ego).

turejee mgogoro wa rooney na man utd kuhusiana na mustakabali wake na klabu (rooney alifika kuponda sera za uendeshaji wa klabu hadharanu hususani kwenye ishu ya usajili, kumbe kelele zote alitaka ongezeko kubwa la mshahara wake, hivi tusema na yeye hakuwa na mapenzi ya ukweli na united?)

paul scholes aliwahi kugoma kuingia uwanjani mnamo mwaka 2001 kwa sababu ya hoja ya kikosi dhaifu kilichochaguliwa kucheza dhidi ya arsenal, hatimaye akapigwa faini, ndipo kipindi hicho tetesi za kuelekea Inter milan zikaanza kuzagaa , pia ujio wa sebastian veron ulipelekea achezeshwe nafasi isiyompendeza(namba 10) na jambo hilo likazidi kumkosesha amani, ndio maana sven goran erikson alikuwa anamtumia paul scholes left winger kama ilivyokuwa man utd, kwa kuwa mzee alikosa bahati mzigo wa matusi ukamuangukia yeye na si ferguson aliyeanzisha tabia ya kumbadilisha nafasi paul scholes tokea mwanzoni.

rejea sakata la cantona na kung fu zake
rejea sakata la roy keane (mpaka leo anamchukia fergie)
rejea sakata la beckham na fergie
rejea sakata la nistelrooy​

cristiano ronaldo tokea mwanzoni alishaweka wazi dhamira yake ya kutaka kuichezea real madrid kabla hata hajawa nyota muhimu ndani ya kikosi chetu, halafu ile ishu yake ya usajili kipindi kile ilichafuliwa zaidi na sepp blatter (aliwahi kusema kuna timu zinawafanya wachezaji kuwa ni watumwa na haikuwa kauli yenye kupendeza masikioni mwa united ila ni kauli yenye kupendezwa masikioni mwa ronaldo kwa sababu aliona amepata mtetezi atakayemsaidia kutimiza ndoto zake za muda mrefu za kuichezea real madrid kwani hakuna mtu aliyekuwa tayari ndani ya united kumpoteza ronaldo kijinga jinga)

I am a slave, says Ronaldo as he pushes for Madrid move
 
Hata mim naungana na haya mawazo, Cr7 akiwa na 23 years old alimuomba Sir Alex amruhusu ajiunge na timu yake ya ndoto Real Madrid, Giggs akiwa ktk peak alitakiwa na timu kubwa duniani ila aligoma also fundi Paul Scholes

Sent using Jamii Forums mobile app
Cr7 ndo mchezaji pekee aliyetoka Man u anayetamba adi leo ..wengine wote wamepoteana ..ivyo Ronaldo ni muchezaji bora wa muda wote apo Man United..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na bado akatufunga tulipocheza na juventus na akashangilia vizuri tu utadhani alizwa kwa lazima na klabu wakati yeye ndio alilazimisha kuondoka. Hata El Clasico ya mwisho hapa alienda kuitazama ila sijawahi ona amesafiri toka Madrid au Turin kwenda OT kutazama derby yoyote, hii ni wazi anaipenda na kuithamini R. Madrid kuliko Man U. Yawezekana CR7 anaipenda R. Madrid siyo Manchester United, ila anampenda Ferguson kuliko kocha yeyote aliyewahi mfundisha

Msamehe bro, derby ya Madrid na Barca yenye either Ronaldo au Messi au wote ni kama premier ya movie kubwa sana duniani, kila mwanamichezo anataka kuiona. Tena hata wasio wanamichezo watataka kuiona.

Kiuhalisia zile timu mbili za Barca na Madrid ziko branded kama namba 1 na 2 duniani kwa kipindi kirefu sana, binafsi ukiacha Liverpool vs Man Utd, derby nyingine niliyoangalia sana ni hiyo. Tokea kipindi cha Figo anahama kutoka Barca kwenda Madrid.

Sasa mtu kama Ronaldo ambaye ni juzi tu katoka kuchezea Madrid na bado anatambulika pale, si ajabu kwenda hiyo game, na unaweza kukuta aliitwa na timu kwa ajili ya kuwapa motivation vijana, ndiyo maana aliingia mpaka locker room.

Binafsi siyo mshabiki wa Man Utd, lakini Ronaldo namwelewa sana toka yuko Man Utd, na nilipunguza kuangalia game za Man Utd baada ya Ronaldo kuondoka.
 
Back
Top Bottom