Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kwenye safu ya ushambuliaji kwa umri wa Ighalo sioni kama atapewa permanent Contract lakini sokoni hakuna watu watakaoweza kununulika kwa dau dogo, kilichowazi ni kwamba Harry Kane kama Tottenham hawatafika top four huenda akaondoka Tottenham dau lake Daniel Levy anajua.
khofu yangu ipo kwa timu zitakazohitaji huduma ya harry kane sidhani kama wataweza kuhimili gharama zake za usajili (amebakisha miaka 4 kwenye mkataba wake) pamoja na mshahara wake (bila ya kusahau ugumu wa kufanya biashara na daniel levy ukimuongezea na jose mourinho anayehitaji kujenga timu ya ushindani)

mauricio pochettino endapo atafanikiwa kupata offer ya kufanya kazi kwenye timu kubwa (kati ya man city, psg au man utd) basi upo uwezekano wa kumshawishi harry kane ajiunge naye kwenye timu, kinyume chake si guardiola. thomas tuchel, zidane, bayern munich watakaokuwa tayari kulipa zaidi ya paundi millioni 130 kupata huduma ya harry kane.

kinyume chake

== bayern munich - robert lewandowski bado wataendelea kumtegemea kwa misimu mengine miwili
== psg - mauricio icardi (wanaweza kumsajili rasmi baada ya kumalizika kwa mkopo, amewafungia magoli 20 kwenye mechi 31)
== josep guardiola-sergio aguero ataendelea kuwepo chini yake, bila ya kusahau zimwi la financial fair play bado linawatafuna
== barcelona - ni kweli wanahitaji mrithi wa luis suarez ila sidhani kama harry anaweza kuvutiwa na offer ya kucheza barcelona japokuwa ni ndoto ya kila mchezaji kucheza pamoja na mtakatifu messi lionel, jambo baya zaidi kwa miaka hii ya karibuni barcelona wamefanya usajili kwa kuleta wachezaji kwa kutumia gharama kubwa lakini bado wameshindwa kukiepuka kivuli cha messi kiutegemezi (watakuwa makini sana kufanya usajili msimu ujao)
== real madrid - sikio la kufa kwa kylian mbappe (zidane anamuhitaji sana mbappe kuliko paul pogba ndivyo ninavyoamini), ni rahisi kulipa paundi millioni 150 kupata huduma ya mbappe kuliko hela hiyo kuielekeza kwa harry kane, bila ya kusahau real madrid wanaweza kuvunja kikwazo (release clause) kilichowekwa na wakala wa erling haarland ili kupata huduma yake kuliko kutumia mara mbili ya fedha kupata huduma ya harry kane.

ukiziangalia timu zote tajwa hapo juu utagundua takribani zote zinasumbuliwa na matatizo yasiozidi mawili (maeneo watakayoyafanyia kazi kwenye usajili) tofauti na manchester united ambao kwa akili ya haraka haraka tungelipendelea kushuhudia usajili wa wachezaji watatu wenye viwango vikubwa, kivyovyote harry kane ni mchezaji muhimu sana tunayemuhitaji nyakati hizi tunazojiandaa kurudisha ubora wetu wa kiushindani barani ulaya, kikwazo kikubwa itakuwa ni bajeti ya usajili sidhani kama inatosheleza kuelekeza nguvu sehemu nyenginezo kama tutaweka kipaombele kwa harry kane.

pia tumekuwa tukiimba wimbo wa kuhitaji winga wa kulia (kiitikio chetu ni jadon sancho), kwa hesabu za haraka haraka utahitaji takribani paundi millioni 250 kufanya usajili wa wachezaji hao wawili (jadon sancho, harry kane), bila ya kusahau hadithi za kumhitaji kiungo mshambuliaji mwengine atakayeziba nafasi ya jesse lingard, andreas perreira (hapa kwa kiasi kikubwa tunamuangalia jack grealish au james maddison)

harry ni mshambuliaji mwenye uhakika wa kukupa magoli 25 kwa msimu mmoja pindi anapokuwa fiti ( 181 goals and 30 assists in 278 games for Spurs ), lakini tatizo kubwa ninaloliona ukiachana na gharama za usajili ni kuhusu afya yake (injury prone), ukiangalia takwimu zake kiwango chake cha ufungaji wa magoli kimekuwa kikipungua kila msimu kutokana na kukosa muda wa kutosha wa kucheza.

59 League goals in 67 games in 16/17 season and 17/18 season (0,88 goals per game)
28 League goals in 48 games in 18/19 season and 19/20 season (0,58 goals per game)

16/17 (0.96 goals per game) = amecheza mechi 30
17/18 (0.81 goals per game) = amecheza mechi 37
18/19 (0.60 goals per game) =amecheza mechi 28
19/20 (0.55 goals per game) = msimu huu amecheza mechi 20

ninachokiona mimi klabu itatafuta cheap option (labda ighalo, joshua king) then fedha nyengine zitaelekezwa kwenye usajili wa jadon sancho (haijalishi tumepata tiketi ya UEFA au kinyume chake), unajua tunaelekea mwaka wa 10 tumeshindwa kupata winga atakayekata kiu ya hitaji letu.

usajili wa harry kane na jadon sancho unahitaji maamuzi ya kibabe kwa sababu wote tunawahitaji kama ubongo na uti wa mgongo, wengi wetu hatufurahishwi na safu yetu ya ushambuliaji kuongozwa na anthony martial, pia wengi wetu hatufurahishwi kuona eneo letu la winga wa kulia linaongozwa na juan mata, jesse lingard na daniel james.

1585480017473.png
 
JUVENTUS wanajipanga kuhakikisha wanatimiza ndoto zao za kumsajili kiungo wa Manchester United, Paul Pogba kwenye dirisha lijalo la usajili.
Kwenye mpango huo, miamba hiyo ya soka ya Italia imepanga ama kumtumia mshambuliaji Paulo Dybala au kiungo Miralem Pjanic kwenye dili la kuwashawishi Man United.
Pogba anaonekana kuwa kwenye nyakati zake za mwisho za maisha huko Old Trafford na huenda akaachana na timu hiyo kwenye dirisha lijalo la usajili huku Juventus wakimtaka mchezaji wao wa zamani arudi kwenye kikosi.
Real Madrid nao wanatajwa kuhitaji saini ya mchezaji huyo na hapo ndipo panapowafanya Juventus kutaka kuwapa Man United ofa ya mchezaji ili kushinda kwenye vita hiyo.
Man United wapo tayari kuachana na Pogba kama tu kutawekwa mezani Pauni 100 milioni huku mchezaji mwenyewe akidai kwamba atakasirika kama klabu hiyo itatumia kipengele kilichowekwa kwenye mkataba wake cha kuongeza mwaka mmoja zaidi wa kuendelea kubaki kwenye kikosi hicho. Mkataba wa sasa wa Pogba utafika tamati mwakani, lakini ndani yake kuna kipengele kinachowaruhusu Man United kumwongezea mwaka mmoja. Juventus wao wanamtaka na wapo tayari kuachana na mmoja wa wachezaji wao Pjanic na Dybala.

Rudi Nyumbani Kumenoga.
Watupe hao wachezaji na hela itakuwa dili nzuri japo juve siyo wapumbavu hivyo
 
khofu yangu ipo kwa timu zitakazohitaji huduma ya harry kane sidhani kama wataweza kuhimili gharama zake za usajili (amebakisha miaka 4 kwenye mkataba wake) pamoja na mshahara wake (bila ya kusahau ugumu wa kufanya biashara na daniel levy ukimuongezea na jose mourinho anayehitaji kujenga timu ya ushindani)

mauricio pochettino endapo atafanikiwa kupata offer ya kufanya kazi kwenye timu kubwa (kati ya man city, psg au man utd) basi upo uwezekano wa kumshawishi harry kane ajiunge naye kwenye timu, kinyume chake si guardiola. thomas tuchel, zidane, bayern munich watakaokuwa tayari kulipa zaidi ya paundi millioni 130 kupata huduma ya harry kane.

kinyume chake

== bayern munich - robert lewandowski bado wataendelea kumtegemea kwa misimu mengine miwili
== psg - mauricio icardi (wanaweza kumsajili rasmi baada ya kumalizika kwa mkopo, amewafungia magoli 20 kwenye mechi 31)
== josep guardiola-sergio aguero ataendelea kuwepo chini yake, bila ya kusahau zimwi la financial fair play bado linawatafuna
== barcelona - ni kweli wanahitaji mrithi wa luis suarez ila sidhani kama harry anaweza kuvutiwa na offer ya kucheza barcelona japokuwa ni ndoto ya kila mchezaji kucheza pamoja na mtakatifu messi lionel, jambo baya zaidi kwa miaka hii ya karibuni barcelona wamefanya usajili kwa kuleta wachezaji kwa kutumia gharama kubwa lakini bado wameshindwa kukiepuka kivuli cha messi kiutegemezi (watakuwa makini sana kufanya usajili msimu ujao)
== real madrid - sikio la kufa kwa kylian mbappe (zidane anamuhitaji sana mbappe kuliko paul pogba ndivyo ninavyoamini), ni rahisi kulipa paundi millioni 150 kupata huduma ya mbappe kuliko hela hiyo kuielekeza kwa harry kane, bila ya kusahau real madrid wanaweza kuvunja kikwazo (release clause) kilichowekwa na wakala wa erling haarland ili kupata huduma yake kuliko kutumia mara mbili ya fedha kupata huduma ya harry kane.

ukiziangalia timu zote tajwa hapo juu utagundua takribani zote zinasumbuliwa na matatizo yasiozidi mawili (maeneo watakayoyafanyia kazi kwenye usajili) tofauti na manchester united ambao kwa akili ya haraka haraka tungelipendelea kushuhudia usajili wa wachezaji watatu wenye viwango vikubwa, kivyovyote harry kane ni mchezaji muhimu sana tunayemuhitaji nyakati hizi tunazojiandaa kurudisha ubora wetu wa kiushindani barani ulaya, kikwazo kikubwa itakuwa ni bajeti ya usajili sidhani kama inatosheleza kuelekeza nguvu sehemu nyenginezo kama tutaweka kipaombele kwa harry kane.

pia tumekuwa tukiimba wimbo wa kuhitaji winga wa kulia (kiitikio chetu ni jadon sancho), kwa hesabu za haraka haraka utahitaji takribani paundi millioni 250 kufanya usajili wa wachezaji hao wawili (jadon sancho, harry kane), bila ya kusahau hadithi za kumhitaji kiungo mshambuliaji mwengine atakayeziba nafasi ya jesse lingard, andreas perreira (hapa kwa kiasi kikubwa tunamuangalia jack grealish au james maddison)

harry ni mshambuliaji mwenye uhakika wa kukupa magoli 25 kwa msimu mmoja pindi anapokuwa fiti ( 181 goals and 30 assists in 278 games for Spurs ), lakini tatizo kubwa ninaloliona ukiachana na gharama za usajili ni kuhusu afya yake (injury prone), ukiangalia takwimu zake kiwango chake cha ufungaji wa magoli kimekuwa kikipungua kila msimu kutokana na kukosa muda wa kutosha wa kucheza.

59 League goals in 67 games in 16/17 season and 17/18 season (0,88 goals per game)
28 League goals in 48 games in 18/19 season and 19/20 season (0,58 goals per game)

16/17 (0.96 goals per game) = amecheza mechi 30
17/18 (0.81 goals per game) = amecheza mechi 37
18/19 (0.60 goals per game) =amecheza mechi 28
19/20 (0.55 goals per game) = msimu huu amecheza mechi 20

ninachokiona mimi klabu itatafuta cheap option (labda ighalo, joshua king) then fedha nyengine zitaelekezwa kwenye usajili wa jadon sancho (haijalishi tumepata tiketi ya UEFA au kinyume chake), unajua tunaelekea mwaka wa 10 tumeshindwa kupata winga atakayekata kiu ya hitaji letu.

usajili wa harry kane na jadon sancho unahitaji maamuzi ya kibabe kwa sababu wote tunawahitaji kama ubongo na uti wa mgongo, wengi wetu hatufurahishwi na safu yetu ya ushambuliaji kuongozwa na anthony martial, pia wengi wetu hatufurahishwi kuona eneo letu la winga wa kulia linaongozwa na juan mata, jesse lingard na daniel james.

View attachment 1402951
Mkuu nafasi ya kiungo mshambuliaji kuna Pogba kama ataendelea kuwa mmoja wetu msimu ujao au la pesa tutakayomuuza ndio hiyo tutatumia kumnunua Grealish au Madders. Hivyo tutabaki tukihitaji bajeti kwa ajili ya wing wa kulia (Sancho) na mshambuliaji aina ya Kane.
Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa man utd wanamtaka Auba wa Arsenal,jamaa ni world class lakini kwenye list yako sijaona ukimuhusisha na giant yeyote. Vipi hapo bro.
 
Kama tunahitaji cheap option kuwa mbadala wa Harry Kane bora kumsajili Raul Jimenez wa Wolves kuliko huyu Joshua King.

Lakini hivi Jack Grealish akisajiliwa Man united bado Jadon Sancho atakuwa anahitajika tena United ?

Kama tutashindwa kumsajili Harry Kane je Timo Werner hawezi kuwa mbadala mzuri zaidi? Wasi was wangu Werner anacheza akitokea kushoto sasa sijui wataweza kucheza vipi na Marcus Rshford ambaye kwangu ni bora kuacha kusajili mchezaji mwingine ili Rashford aendeleze makali yake kushoto.

Lakini Solkjaer amekuwa akimpa nafasi sana Tahith Chong huenda ni maandalizi pia kama atashindwa kusajili winger wa kulia.

Mkuu credit kwa andiko zuri.
Watupe hao wachezaji na hela itakuwa dili nzuri japo juve siyo wapumbavu hivyo
Daemusin

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Confidence ndiyo kinachokosekana, sema kwa mechi za hivi karibuni ameanza kujiamini na kuimarika sana.

Let's hope for the best aendelee kuimprove.
Huyu dogo nilikuwa namkubali sana kwenye timu ya watoto..

ila kila akipewa nafasi kwenye first team lazima anikere..sijui hana nguvu au stamina..Yaani ni kudondoka dondoka tu..

Muda upo wa yeye kuimarika zaidi lakini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NYUMA YA PAZIA: ANATAMBA BRUNO FERNANDES, ANACHEKA MINO RAIOLA

NI mchezo wa Chesi. Kete zipo hadharani lakini akili ipo kichwani. Zamani tulikuwa tunawatazama Warusi wawili wakichuana. Garry Kasparov na Anatoly Karpov. Mechi inakuwa kali kiasi cha kuahirishwa. Wanarudi tena kesho na akili inazidi kutumika.
Jaribu kufikiri wakati mteja wako anapopata upinzani mkali lakini unashangilia. Ndivyo akili ya mtu anayeitwa Mino Raiola ilivyo. Wakala huyu. Mtoto wa Kiitaliano aliyelelewa Haarlem Uholanzi. Ana akili kama mchwa. Anaongea lugha za Kiitaliano, Kiingereza, Kijerumani, Kihispaniola, Kifaransa na Kireno.
Atatumia moja kati ya lugha hizo kuwasiliana na wateja wake katika dirisha kubwa lijalo la majira ya joto akijaribu kumuuza mchezaji anayeitwa Paul Pogba kwenda katika klabu kubwa za Ulaya. Haikuwa kazi rahisi katika dirisha kubwa lililopita la majira ya joto lakini ugumu wa kazi unaweza kupungua mwishoni mwa msimu.
Kuna sababu nyingine imekuja. Bruno Miguel Borges Fernandes. Ndio, huyu mtu atamrahisishia kazi Raiola mwisho wa msimu huu. Tangu jioni ile aliyocheza pambano lake la kwanza la Ligi Kuu akiwa na jezi ya Manchester United katika pambano dhidi ya Wolves Bruno hakamatiki.
Bruno anakupa mambo mengi katika soka. Umiliki wa mpira, pasi za mwisho, mashuti, mabao na kila kitu. Bruno tayari ana pasi mbili za mwisho katika mechi tatu tu za Ligi Kuu ya England, wakati huo huo tujikumbushe kuwa Mesut Ozil ana pasi moja ya bao katika mechi 17 alizoichezea Arsenal msimu huu.
Tayari mashabiki wa United washamchoka Paul Pogba. Washamchoka wakala wake, Raiola. Washachoka na uvumi wa Pogba kuhama. Mchezaji mwenyewe ambaye kila siku anawasumbua akili ana mchango mdogo uwanjani msimu huu. Amekaa zaidi katika kitanda cha hospitali kuliko uwanja wa soka.
Kwa chochote ambacho Bruno anakifanya, Raiola anacheka. Anajua kwamba uchungu wa United kumpoteza Pogba utapungua mwishoni mwa msimu endapo Bruno ataendeleza moto huu huu. Tayari Bruno ameziba mashimo mengi ambayo Pogba angeyaacha.
Mwishoni mwa msimu hata United yenyewe inaweza ikashusha bei ya Pogba kwa sababu watataka aondoke kupisha utawala wa Bruno. Lakini pia watataka aondoke kwa ajili ya kuachana na jinamizi la wakala anayewasumbua kupita kiasi, Raiola.
Hizi ni hesabu za chesi. Hesabu za kuchungulia karata ya mwenzako na kuicheza vema. Kwa sasa United haina cha kupoteza, Raiola hana cha kupoteza, Pogba hana cha kupoteza. Mwisho wa msimu wanaweza kukubaliana kuachana na kila mtu akashika mkono wa mwenzie na kushika njia yake.
Kwa sasa pindi Pogba atakaporudi uwanjani utasikia kauli nyingi mpaka mwisho wa msimu. United watasema ‘hatuna mpango wa kumuuza Pogba’. Ole Solskjaer atasema ‘Nataka kutengeneza kombinesheni ya Pogba na Bruno’. Mwisho wa siku ni katika kujaribu tu kutoishusha bei ya Pogba lakini mioyoni watafahamu kwamba Pogba anaondoka.
Raiola kwa sasa atakuwa anaongea kwa unafuu kidogo na watu wa Barcelona. Kesho yake atanyanyua simu yake na kuongea na watu wa PSG. Keshokutwa yake ataongea vema na watu wa Juventus. Maisha yake yatarahisishwa na Bruno.
Kama ingekuwa Pogba ana miaka 31 Raiola angeingiwa na hofu. Kwamba mteja wake anasukumwa nje ya kikosi huku labda soko lake litakuwa dogo nje ya Old Trafford. Lakini Pogba ndio kwanza anatimiza miaka 27 wiki ijayo.
Timu kubwa zinajua kwamba Pogba ana matatizo ya mguu na ana matatizo na Manchester United. Wanajua ni kitu gani anaweza kukupa pindi akiyaweka matatizo hayo kisogoni. Akicheza mechi tatu tu hata kuanzia Aprili mwishoni hadi Mei katikati bado soko lake lipo pale pale. Tukiachana na ukweli huo, kinachonishangaza kuhusu Bruno ni uhamisho wake.

Je ni maandalizi ya kuondoka kwa Pogba?
 
Huyu dogo nilikuwa namkubali sana kwenye timu ya watoto..

ila kila akipewa nafasi kwenye first team lazima anikere..sijui hana nguvu au stamina..Yaani ni kudondoka dondoka tu..

Muda upo wa yeye kuimarika zaidi lakini
Na nywele zile anyoe, mana mwili Mdogo bado anajitwisha na limzigo la minywele. Gomes angekuwa anapewa hiyo nafasi
 
Back
Top Bottom