Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mkuu, kuna watu wanaamini mfumo wa ATM hauendani na kipaji cha Joao Felix

Lakini mbona Griezman ame shine pale ATM kwa mfumo ule uliopo

Na Joao alikuwa ni like to like replacement ya Griezman

Kuna tatizo sehemu zaidi ya mfumo wa uchezaji wa ATM
baadhi ya nyakati wachezaji wa ulaya ambao tunawafahamu kama ni professional (wa tabia, matendo na fikra) hufanya maamuzi ambayo hayatofautiani na yale yanayochukuliwa na wachezaji wa kiswahili (unampongeza samatta kwa kucheza aston villa ila wewe unakataa ofa ya tp mazembe, unakimbia sweden na unaikataa al ahly ya sudan kwa sababu ya hamida)

diego simeone ameshafundisha atletico madrid kwa takribani miaka mitano na falsafa yake ya ufundishaji haijabadilika hata kwa sekunde moja (ni mtu anayeamini team work kuliko kutegemea miujiza ya mchezaji mmoja).

huyo felix alikuwa halifahamu jambo hili pamoja na washauri wake?

ndio yale ya alexander hleb (fundi) anaondoka arsenal akiwa ni mchezaji muhimu sana na hatimaye anaelekea barcelona akiamini kwa uwezo aliojaaliwa hatoweza kuwekwa nje, kwa akili ya kawaida ina maana alexander alikuwa hafahamu ya kwamba kwa uwezo aliokuwa nao na style yake ya uchezaji hatoweza kumweka nje andreas iniesta pamoja na thiery henry kwenye mfumo wa 4-3-3?

pia rejea ishu ya:
alexander song na barcelona ya sergio bosquet
mascherano na barcelona ya sergio bosquet
cesc fabregas dhidi ya xavi hernandez

sipingani na sera au tabia ya mchezaji kwenda kutafuta changamoto mpya ya kazi yake bali napingana na tabia ya mchezaji husika kuhama sehemu ambayo inaweza kumhudumia mahitaji yake yote na kuelekea sehemu ambayo haitoweza kumhudumia kimahitaji (wengi wao hufikiria mahitaji muhimu ni ongezeko la mshahara na makombe).

joao felix alihitaji timu mfano wa borussia dortmund ila kwa mazingira ya usajili wake isingeliwezekana kwa sababu kila upande ulishaonyesha tamaa ya kuvuna fedha haramu bila ya kuangalia mustakabali wa felix kikazi.

atletico wamelipa takribani paundi millioni 100 kupata huduma yake, ni vigumu sana kumpata mjinga wa kulipa zaidi ya kiwango kama hicho au asilimia 70 ya kiwango hicho (kumuuza kwa bei ya hasara).

labda vichaa wanaoitwa barcelona wanaweza kulipa fedha kama hiyo, kama waliweza kulipa kwa dembele, coutinho, griezman, (paulinho na malcom) kwa nini wasilipe haliyakuwa wanatafuta mbadala wa lionel messi.

kinyume chake itakapomaliza corona miaka miwili ijayo huenda tukamuona joao felix kwenye ardhi ya china au japan akicheza soka pamoja na iniesta, hulk, ramirez, oscar n.k

----------------------------------------------------------
Alexander Hleb has admitted that he “made a mistake” leaving Arsenal for Barcelona in 2008. The Belorussian moved to Spain for a fee in the region of €15 million but failed to make an impact, being loaned out after just one season before finally leaving the club on a permanent basis in 2012.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Man united ya sasa bado inamhitaji Sergej Millinkovic Savic?

Hivi Man united ya sasa bado inamhitaji Milan Skinniar ?

Hivi Man united ya sasa bado inamhitaji Khalidou Koulibally ?

Hivi Man united ya sasa bado inamhitaji Mauricio Pochetino ?

Hivi Man united ya sasa bado inamhitaji Masmilliano Allegry ?

Najaribu kujiuliza tu

Sent using Jamii Forums mobile app
ukimuondoa yule jamaa anayeitwa Chusa ndani ya thread hii takribani wachangiaji wote humu ndani tumekuwa tuna tabia ya kubadilika kutokana na mdundo wa spika kwangu mimi ni jambo zuri sana kubadilika kifikra...... ila sielewi yule mdau anawezaje kuwa na msimamo usioyumba (acha nikupe hongera brother kwa msimamo wako wa kibabe) na pia acha niendelee kubakiwa na mshangao dhidi yako (timu ikicheza vizuri upo freshi na timu inapocheza vibaya upo fresh tu kimtazamo)
-----------------------------------------------------------
ole gunnar solskjaer....
  1. tokea aondoke sir alex naweza kusema yeye ndiye mwalimu pekee aliyeweza kufanya kazi na wachezaji wote huku wakionyesha bidii na nidhamu wakati wote wa safari (nyakati za shida na raha wachezaji wote wamekuwa wakijitolea kwa ajili yake) bila ya kusikia fununu yoyote yenye kuleta mgawanyo kwenye timu (hakuna tena anti mourinho wala pro mourinho) na sasa tumekuwa familia moja.
  2. game plan zake zimetupa faida kubwa sana ya kimatokeo pindi tunapokutana na timu zinazotuzidi kwa kuwa na kundi kubwa lenye wachezaji wenye vipaji.... ukiniuliza ni mechi ngapi ambazo sir alex amemfunga guardiola nitakutajia mechi ileeee tuliocheza marekani, ila ndani ya msimu mmoja ole ameshafanikiwa kumfunga guardiola mechi 3 kwa mfumo ule ule (3-4-3)...... guardiola kumfunga ole mechi moja si jambo geni kwenye ulimwengu wa wapenda soka.
  3. mimi ni mmoja ya wachangiaji wenye tabia ya kubadilika kimsimamo humu ndani na sina tabia za wapiga kura wa afrika (kama ni ccm au chadema basi ni hao hao) .... tokea tupoteze mechi dhidi ya burnley kwa sababu ya wachezaji wachache na ubishi wa mwalimu wa kuamini ya kwamba yupo sahihi kimaamuzi, baada ya hapo timu imeonyesha dalili ya kuimarika kila eneo (wapo wengine wanasema sababu ni ujio wa bruno, ighalo, kurudi kwa matic, bailly)...... ok, kila mtu anabaki na sababu zake anazoziona kupitia jicho lake pindi anapokaa kwenye televisheni kufuatilia mechi zetu........ kwa muda huu sioni umuhimu wa kutafuta mwalimu mwengine.
  4. naweza kusema ole amekuwa kama catepillar, tunahitaji kuwa na uvumilivu na huyu catepillar ili baadae tupate kumshuhudia kipepeo mwenye mbawa nzuri zinazovutia machoni mwetu.
 
Mkuu, kuna watu wanaamini mfumo wa ATM hauendani na kipaji cha Joao Felix

Lakini mbona Griezman ame shine pale ATM kwa mfumo ule uliopo

Na Joao alikuwa ni like to like replacement ya Griezman

Kuna tatizo sehemu zaidi ya mfumo wa uchezaji wa ATM
upo sahihi
inawezekana tatizo ni yeye mwenyewe joao felix ameshindwa kuendana na kasi ya LA LIGA au pengine bwana mdogo ni overrated.
nawalaumu washauri wake pamoja na benfica waliojawa na tamaa ya kifedha.
 
Kwamba bora mwakani tuwe Europa League lakini wale jamaa wakose ubingwa? Kumbuka hata sisi tutaumia

Kuna wachambuzi feki walikuwa wanafananisha hicho kikosi chao na kile chetu cha 1999, treble winning team
Kuna watu itakuwa imewauma sio kidogo.
Waliandaa hadi nguo za kwenda kwenye parade ya mabingwa wapya!
Ligi ya msimu huu ingeishia hapo tuanze upya tu mwezi wa nane.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwangu mimi bado namuona JOAO FELIX kuwa ni kipaji na wala sio overrated kihivyo.
Tunatambua na tumeshuhudia kuwa ni wachezaji wachache na wenye bahati ndio huwa wanaweza kutoka timu A iliyo ligi B na kufanikiwa kung'ara timu C inayoshiriki ligi D mkuu Daemusin
Sababu zinaweza kuwa ni nyingi zinazopelekea dogo asiwike sana pale wanda,lakini kubwa kuliko yote ni ameingia pale akiikuta ATM inachechemea kimatokeo (naweza kusema msimu wake mbovu kati ya mingi niliyoishuhudia hii timu). Sio kwamba haina vipaji la,ila nadhani ule muunganiko kati ya wachezaji haujazaa matunda chanya kwa wakati huu.

Pili dogo ameenda pale akitegemewa kutoa matokeo chanya kama kipindi cha Griezmann bila kujali ugeni wake kwenye ligi pamoja na umri.
N pia angalia striking force yao inatengenezwa na morata pamoja na Costa waliokuwa wote ni magarasa ya chelsea.
ATM wanacheza vizuri sana kuanzia nyuma hadi sehemu ya kiungo halafu mwisho ndio shida inapokuja.
 
Kwamba bora mwakani tuwe Europa League lakini wale jamaa wakose ubingwa? Kumbuka hata sisi tutaumia

Kuna wachambuzi feki walikuwa wanafananisha hicho kikosi chao na kile chetu cha 1999, treble winning team

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu wa mpira (kama kweli yupo) alikuwa upande wa liverpool kwa msimu huu.
Hata sisi kuingia top 4 bado ni bahati nasibu pia.
 
Mkuu Daemusin credit kwa andiko lako.

Unadhani ni maeneo gani sasa ambayo tunapaswa kuweka kipaumbele ili kuimarisha kikosi chetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tukipata wachezaji angalau 3 wengine,

sidhani kama bajeti yetu itavuka paundi millioni 200
  1. kipaombele chetu kiwe ni winga mfano wa jadon sancho kama alivyoelezea chief mkwawa hapo juu, unajua hata hao wachezaji mfano wa silvester, wes brown, phil neville, john oshea na hata gary neville kiupande fulani hawakuwa ni fullback wenye miujiza mikubwa sana kama walivyo jamii ya dani alves, jordi alba na wengineo lakini udhaifu wao ulizibwa na ubora wa winga wetu( giggs, beckham, ronaldo, nani na hata Andrei Kanchelskis)...... possibilities ya kusaini fullback mwengine haipo ila uwezekano wa kusajili winga aliyejaaliwa ufundi wa kufunga na kupika nafasi za magoli mfano wa sancho naamini ndio dira ya mwalimu na kila mdau wa machester united.
  2. mshambuliaji: kwa kuangalia bajeti yetu na huu mdundo wa tetesi unavyokwenda nitakuwa mwanadamu wa mwisho kuamini ya kwamba tutasajili mshambuliaji wa kiwango cha juu mfano wa harry kane, kwa sasa hatupo vizuri sana kimapato yatakayotuwezesha kulipa paundi millioni 80-100 kwa wachezaji wawili tofauti na hali hii ikichangiwa zaidi na madeni ya wamarekani...... hata ukiangalia soko la usajili itakuwa ni vigumu sana kupata mshambuliaji mwengine kwa bei ya afadhali........huenda backup yetu atakuwa ni ighalo ambaye ameshafunga magoli manne kwenye takribani mechi 8 alizopewa...... pia uwepo wa mason greenwood ambaye mpaka sasa ameshafunga magoli 11 kwenye mechi takribani mechi 30 alizocheza kutazidisha kufifisha kampeni ya kusajili mshambuliaji mwengine mwenye nguvu (misimu miwili inayofuata huenda tukasajili mshambuliaji mwengine kama greenwood na martial watakaposhindwa kufikia malengo yetu)
  3. mustakabali wa paul pogba ndio utakaoamua ni mchezaji wa aina gani anayepaswa kusajiliwa ili kuziba nafasi yake kama ataamua kuondoka msimu ujao.
  4. nemanja matic huenda akapewa kandarasi mpya hivyo basi uwezekano wa kusajili kiungo mwengine wa ulinzi mwenye uzoefu utakuwa ni mdogo sana (labda tukawekeze kwa yule dogo wa birmingham city)
  • kuondoka kwa pogba ndio ujio wa jack grealish ndivyo ninavyoamini.
  • pia kushindwa kumsajili jadon sancho ndio ujio wa james maddison au yule dogo wa real sociedad anayeitwa martin odegaard.
jadon sancho atatibu ugonjwa wetu unaotusumbua na martial atakuwa ndiye mshambuliaji wetu wa uhakika huku marcus rashford akiwa winga wetu wa kushoto msimu ujao.

David degea + wan bissaka + Maguire + luke shaw + victor Lindelof
Jadon Sancho + mc'tominay + fred / bruno + rashford
pogba + martial
backup: (ighalo, greenwood, matic, perreira, williams (atakuwa kiraka kama ashley young), juan mata, bailly, tuanzebe, daniel james, romero)

1584101591510.png
 
Kwangu mimi bado namuona JOAO FELIX kuwa ni kipaji na wala sio overrated kihivyo.
Tunatambua na tumeshuhudia kuwa ni wachezaji wachache na wenye bahati ndio huwa wanaweza kutoka timu A iliyo ligi B na kufanikiwa kung'ara timu C inayoshiriki ligi D mkuu Daemusin
Sababu zinaweza kuwa ni nyingi zinazopelekea dogo asiwike sana pale wanda,lakini kubwa kuliko yote ni ameingia pale akiikuta ATM inachechemea kimatokeo (naweza kusema msimu wake mbovu kati ya mingi niliyoishuhudia hii timu). Sio kwamba haina vipaji la,ila nadhani ule muunganiko kati ya wachezaji haujazaa matunda chanya kwa wakati huu.

Pili dogo ameenda pale akitegemewa kutoa matokeo chanya kama kipindi cha Griezmann bila kujali ugeni wake kwenye ligi pamoja na umri.
N pia angalia striking force yao inatengenezwa na morata pamoja na Costa waliokuwa wote ni magarasa ya chelsea.
ATM wanacheza vizuri sana kuanzia nyuma hadi sehemu ya kiungo halafu mwisho ndio shida inapokuja.
yote uliyoelezea yana ukweli brother na siwezi kupingana na wewe kwa sababu kwanza nimeangalia mechi moja tu ya atletico madrid msimu huu (mechi yao ya kwanza dhidi ya liverpool)

nilichojifunza kupitia hilo andiko lako ni kwamba unaomba au unaamini huyo dogo kama atapewa muda hadi msimu ujao atarudisha thamani na ubora wake uliozoeleka na si vyema kumhukumu kwa kuangalia performance yake ya msimu mmoja.

ahsante sana brother.
 
The FA, Premier League, EFL and Barclays FA Women’s Super League and FA Women’s Championship have collectively agreed to postpone the professional game in England until 3 April at the earliest.

The postponements include all matches in the Premier League, Championship, League One and League Two, as well as all Academy and youth team fixtures.
 
Chances Created per 90 since Bruno Fernandes has played as an attacking midfielder for United:

3.91 – Fernandes
3.87 – L. Alberto
3.66 – Müller
3.59 – Di María
3.43 – Messi
3.21 – De Bruyne
3.15 – Neymar
3.00 – Alexander-Arnold
2.81 – A. Gómez

Aisee Corona imetuondolea starehe

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
The FA, Premier League, EFL and Barclays FA Women’s Super League and FA Women’s Championship have collectively agreed to postpone the professional game in England until 3 April at the earliest.

The postponements include all matches in the Premier League, Championship, League One and League Two, as well as all Academy and youth team fixtures.
na liverpool watapokonywa points zao kwa sababu ya corona......
hawa liverpool watakuwa na laana

teh teh teh
 
toka warudi na uwepo wa maguire na awb umetufanya tumekuwa ngome kubwa. hizi mechi 11 tulizoshinda 9 ni cleansheet
teh teh teh
kumbe wale wahuni leicester city wametuuzia harry maguire kwa bei ya kutupa na tunapaswa tuwaongeze japo asilimia 20 ya fedha tuliowalipa... jamaa amebarikiwa utulivu kama rio ferdinand na ndio maana baadhi ya nyakati nazichukia takwimu (eti anazidiwa na mustafi wa arsenal kwa kuangalia takwimu za msimu uliopita)

ningelipenda zaidi kusikia taarifa ya manchester united kuwafanyia suprise wale jamaa LASK tuliocheza nao jana bila ya mashabiki kwa kuwapa mechi ya kirafiki uwanjani kwao msimu ujao.

naamini wamepata hasara kubwa sana ya kimapato kwa kushindwa kuingiza mashabiki uwanjani kwao (licha ya kwamba hatufanyi vizuri uwanjani kwa takribani miaka 7 lakini bado tumebaki kuwa ni brand yenye mvuto kwa team nyingi sana duniani)

tuwape fair play kama tunavyowapa wamarekani mara kwa mara
 
ukimuondoa yule jamaa anayeitwa Chusa ndani ya thread hii takribani wachangiaji wote humu ndani tumekuwa tuna tabia ya kubadilika kutokana na mdundo wa spika kwangu mimi ni jambo zuri sana kubadilika kifikra...... ila sielewi yule mdau anawezaje kuwa na msimamo usioyumba (acha nikupe hongera brother kwa msimamo wako wa kibabe) na pia acha niendelee kubakiwa na mshangao dhidi yako (timu ikicheza vizuri upo freshi na timu inapocheza vibaya upo fresh tu kimtazamo)
-----------------------------------------------------------
ole gunnar solskjaer....
  1. tokea aondoke sir alex naweza kusema yeye ndiye mwalimu pekee aliyeweza kufanya kazi na wachezaji wote huku wakionyesha bidii na nidhamu wakati wote wa safari (nyakati za shida na raha wachezaji wote wamekuwa wakijitolea kwa ajili yake) bila ya kusikia fununu yoyote yenye kuleta mgawanyo kwenye timu (hakuna tena anti mourinho wala pro mourinho) na sasa tumekuwa familia moja.
  2. game plan zake zimetupa faida kubwa sana ya kimatokeo pindi tunapokutana na timu zinazotuzidi kwa kuwa na kundi kubwa lenye wachezaji wenye vipaji.... ukiniuliza ni mechi ngapi ambazo sir alex amemfunga guardiola nitakutajia mechi ileeee tuliocheza marekani, ila ndani ya msimu mmoja ole ameshafanikiwa kumfunga guardiola mechi 3 kwa mfumo ule ule (3-4-3)...... guardiola kumfunga ole mechi moja si jambo geni kwenye ulimwengu wa wapenda soka.
  3. mimi ni mmoja ya wachangiaji wenye tabia ya kubadilika kimsimamo humu ndani na sina tabia za wapiga kura wa afrika (kama ni ccm au chadema basi ni hao hao) .... tokea tupoteze mechi dhidi ya burnley kwa sababu ya wachezaji wachache na ubishi wa mwalimu wa kuamini ya kwamba yupo sahihi kimaamuzi, baada ya hapo timu imeonyesha dalili ya kuimarika kila eneo (wapo wengine wanasema sababu ni ujio wa bruno, ighalo, kurudi kwa matic, bailly)...... ok, kila mtu anabaki na sababu zake anazoziona kupitia jicho lake pindi anapokaa kwenye televisheni kufuatilia mechi zetu........ kwa muda huu sioni umuhimu wa kutafuta mwalimu mwengine.
  4. naweza kusema ole amekuwa kama catepillar, tunahitaji kuwa na uvumilivu na huyu catepillar ili baadae tupate kumshuhudia kipepeo mwenye mbawa nzuri zinazovutia machoni mwetu.
Mkuu Daemusin credits kwa andiko lako.

Nafikiri Ole kiatu cha kuwa Manchester United Manager kimeanza kumuenea vizuri sana.

Tactically naona improvement kubwa sana hasa kwenye mechi anazohitaji matokeo.

Nini kifanyike.

1 Ole ajaribu kuongeza in game management tactics kuna wakati unaona tunahitaji adjustment ya game plan yetu lakini mwalimu huoni response ya mwalimu.

2 Aanze kuwajengea vijana wake kiu ya makombe na ile big team mentality kama mentality iliyopo Bayern Munichen, Real Madrid, Juventus na Barcelona hii itatusaidia sana kuongeza Ari ya ushindani, na wachezaji kujitambua.

Mengine nimeanza kumpa credits kuwa he can do the job.

Bado naendelea kula mtori huenda nyama nikazikuta chini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona kama tukifanya signing za watu watatu huenda zikatupa squad depth tunayoihitaji.

Priorities.
1 nafikri tuwekeze kwa winger wa kulia japo mwelekeo wa Ole ni kumwamini Tahith Chong huenda akawa suluhisho la kudumu nimeshuhudia mechi kadhaa akimpa nafasi kwenye hiyo wing ya kulia. Jason Sancho ndiyo lulu inayogombaniwa sana sijui ushindani utakuwaje ili tuweze kumpata.

2 Kama Pogba ataondoka huenda Grealish, Madisson au SMS akawa mbadala japo dau la SMS siyo la kitoto sana.

3 Kwenye Defense midfield huenda tusiwe na badiliko kubwa sana kwani watu hawa watatu wameshatuonyesha kuwa wanaweza kuifanya hiyo kazi bila shaka yoyote.

4 Kwenye safu ya ushambuliaji kwa umri wa Ighalo sioni kama atapewa permanent Contract lakini sokoni hakuna watu watakaoweza kununulika kwa dau dogo, kilichowazi ni kwamba Harry Kane kama Tottenham hawatafika top four huenda akaondoka Tottenham dau lake Daniel Levy anajua.

5 Ole amuondoe Phil Jones, Lee Grant pamoja na Jesse Lingard hawa jamaa kwa ujumla wao ni wafanyakazi hewa japokuwa Lingard amekuwa akitusaidia tunapokuwa hatuna namna...

Mungu atusaidie kuondoa hii Corona itatuondolea starehe yetu.
sidhani kama bajeti yetu itavuka paundi millioni 200
  1. kipaombele chetu kiwe ni winga mfano wa jadon sancho kama alivyoelezea chief mkwawa hapo juu, unajua hata hao wachezaji mfano wa silvester, wes brown, phil neville, john oshea na hata gary neville kiupande fulani hawakuwa ni fullback wenye miujiza mikubwa sana kama walivyo jamii ya dani alves, jordi alba na wengineo lakini udhaifu wao ulizibwa na ubora wa winga wetu( giggs, beckham, ronaldo, nani na hata Andrei Kanchelskis)...... possibilities ya kusaini fullback mwengine haipo ila uwezekano wa kusajili winga aliyejaaliwa ufundi wa kufunga na kupika nafasi za magoli mfano wa sancho naamini ndio dira ya mwalimu na kila mdau wa machester united.
  2. mshambuliaji: kwa kuangalia bajeti yetu na huu mdundo wa tetesi unavyokwenda nitakuwa mwanadamu wa mwisho kuamini ya kwamba tutasajili mshambuliaji wa kiwango cha juu mfano wa harry kane, kwa sasa hatupo vizuri sana kimapato yatakayotuwezesha kulipa paundi millioni 80-100 kwa wachezaji wawili tofauti na hali hii ikichangiwa zaidi na madeni ya wamarekani...... hata ukiangalia soko la usajili itakuwa ni vigumu sana kupata mshambuliaji mwengine kwa bei ya afadhali........huenda backup yetu atakuwa ni ighalo ambaye ameshafunga magoli manne kwenye takribani mechi 8 alizopewa...... pia uwepo wa mason greenwood ambaye mpaka sasa ameshafunga magoli 11 kwenye mechi takribani mechi 30 alizocheza kutazidisha kufifisha kampeni ya kusajili mshambuliaji mwengine mwenye nguvu (misimu miwili inayofuata huenda tukasajili mshambuliaji mwengine kama greenwood na martial watakaposhindwa kufikia malengo yetu)
  3. mustakabali wa paul pogba ndio utakaoamua ni mchezaji wa aina gani anayepaswa kusajiliwa ili kuziba nafasi yake kama ataamua kuondoka msimu ujao.
  4. nemanja matic huenda akapewa kandarasi mpya hivyo basi uwezekano wa kusajili kiungo mwengine wa ulinzi mwenye uzoefu utakuwa ni mdogo sana (labda tukawekeze kwa yule dogo wa birmingham city)
  • kuondoka kwa pogba ndio ujio wa jack grealish ndivyo ninavyoamini.
  • pia kushindwa kumsajili jadon sancho ndio ujio wa james maddison au yule dogo wa real sociedad anayeitwa martin odegaard.
jadon sancho atatibu ugonjwa wetu unaotusumbua na martial atakuwa ndiye mshambuliaji wetu wa uhakika huku marcus rashford akiwa winga wetu wa kushoto msimu ujao.

David degea + wan bissaka + Maguire + luke shaw + victor Lindelof
Jadon Sancho + mc'tominay + fred / bruno + rashford
pogba + martial
backup: (ighalo, greenwood, matic, perreira, williams (atakuwa kiraka kama ashley young), juan mata, bailly, tuanzebe, daniel james, romero)

View attachment 1387001

Sent using Jamii Forums mobile app
 
So ikitokea kuna watu wa Pogba wanazungumza kauli chafu juu ya club, na Pogba kakaa kimya akiwa busy anatekeleza yanayomuhusu tu, U suggest better auzwe...!! [if I capture your point well]
Jibu ni ndio kwani hizo "Kauli chafu juu ya club" zinaweza kuchangia kushusha ari/mori ya dressing room.

Na perhaps utakuta kinachosemwa na hao kikawa kinabaraka zake nyuma ya Pazia, sasa mtu wa hivyo wa nini kuendelea nae?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom