Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kizuri ni kwamba pamoja na ugumu wote Tottenham wamekuwa akifanya biashara na Man united.

Michael Carrick na Dimitar Berbatov wote hawa walitokea

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa Glazers wa sasa asee wakitajiwa 150 au 200 wanatoka nduki. Kama Bruno tu hyo 67 waliahirisha kabisa na usajili wake kabla hawajarudi tena January hayo ya 100+ watayaweza mkuu? Bale pia ilishindikana, Modric pia. Labda carick mana Berbatov ilikuwa ni njia nyingine sijui hadi Leo kilichofanyika hadi tukamnyakua mana levy alishakataa kutuuzia
 
Kwa bruno ilikuwa plan nzur sana kumbuka rekod zote za usajili zimewekwa na hao jamaa di maria,paul pogba, harry maguire, tony martial so naona timu inataka kurudi kwenye misingi yake
 
Tukijifua kidogo
 
Attachments

  • We can't stop watching this _scream_⁣ ⁣ _movie_camera__ @PaulPogba ( 800 X 640 ).mp4
    1.7 MB
Kwa bruno ilikuwa plan nzur sana kumbuka rekod zote za usajili zimewekwa na hao jamaa di maria,paul pogba, harry maguire, tony martial so naona timu inataka kurudi kwenye misingi yake
N way muda utaongea
 
Ni ngumu sana kupambana na Real Madrid kwenye soko la usajili.

Wametupiga kwa wachezaji wengi sana.
1 Modric
2 Bale
3 Toni Kroos
4 James Rodriguez

Hao wenyewe huwa wanatoa hela kwa mchezaji bila kujali hata faida watarudishaje.
Hawa Glazers wa sasa asee wakitajiwa 150 au 200 wanatoka nduki. Kama Bruno tu hyo 67 waliahirisha kabisa na usajili wake kabla hawajarudi tena January hayo ya 100+ watayaweza mkuu? Bale pia ilishindikana, Modric pia. Labda carick mana Berbatov ilikuwa ni njia nyingine sijui hadi Leo kilichofanyika hadi tukamnyakua mana levy alishakataa kutuuzia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
STRAKA kinda wa Birmingham City, Jude Bellingham ameripotiwa kuikacha Manchester United na kutaka kutimkia Borussia Dortmund. Straika huyo (16) alikuwa anahusishwa klabu hizi mbili na kuna wakati alionekana kuwa karibu kabisa kujiunga na United, lakini taarifa za hivi karibuni zinadai kinda huyo ameamua kuichagua Dortmund.
Hata hivyo, kutokana na ugonjwa wa corona dili lake linaonekana kukwama huku pia Dortmund wakihofia uchumi wao kuyumba kutokana na virusi hivi vya covid19, ingawa wapo karibu kabisa kuipata saini yake na kuipiku United.
Kwa sasa United imeripotiwa kuhamishia nguvu zake kwa kinda raia wa England, Jadon Sancho anayeichezea Dortmund na taarifa za klabu hiyo zinadai kamwe hawawezi kumuuza kwa pesa ya madafu, hivyo United ijipange kufungua pochi.
 
Hivi kumbe Jude Bellingham ni STRAKA?

Klabu ya Shanghai Shenhua ya hapa China imetoa ofa ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wake Odion Ighalo (30) ambaye anacheza kwa mkopo Manchester United. Mkataba wa sasa ulikuwa unamalizika mwaka 2022, lakini Shanghai baada ya kuridhika na kiwango chake cha hivi karibuni, wanataka kuendelea kummiliki Mnigeria huyo hadi mwaka 2024, kwa malipo ya paundi 400,000 kwa wiki. Kwa upande wake Ighalo anachusubiri ni ofa itakayotolewa na Man United baada ya mkopo wake kumalizika mwezi Juni mwaka huu kwani imekuwa ni ndoto yake ya maisha kukipiga kwa mashetani hao wekundu wa Jiji la Manchester.
Uyu Ighalo hamna akili mule..anaacha paundi zote izo kicha ichi kikundi cha wacheza ngoma??

Kama ni drimu Si keshatimiza!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mashabiki wa man U hatuipendi liverpool mfn hakuna!

Hakuna timu inayochukiwa na manchester united kama liverpool!
Kwa Tz mashabiki wa man u hawaipendi arsenal na co Liverpool ila kwa England Mashariki wa man u hawaipendi Liverpool
 
STRAKA kinda wa Birmingham City, Jude Bellingham ameripotiwa kuikacha Manchester United na kutaka kutimkia Borussia Dortmund. Straika huyo (16) alikuwa anahusishwa klabu hizi mbili na kuna wakati alionekana kuwa karibu kabisa kujiunga na United, lakini taarifa za hivi karibuni zinadai kinda huyo ameamua kuichagua Dortmund.
Hata hivyo, kutokana na ugonjwa wa corona dili lake linaonekana kukwama huku pia Dortmund wakihofia uchumi wao kuyumba kutokana na virusi hivi vya covid19, ingawa wapo karibu kabisa kuipata saini yake na kuipiku United.
Kwa sasa United imeripotiwa kuhamishia nguvu zake kwa kinda raia wa England, Jadon Sancho anayeichezea Dortmund na taarifa za klabu hiyo zinadai kamwe hawawezi kumuuza kwa pesa ya madafu, hivyo United ijipange kufungua pochi.
Huyu dogo ameanza lini kuwa straika,jana au?
 
BOSI WA MAN UNITED HAPATI USINGIZI KISA WACHEZAJI HAWA

KABLA ya Ligi Kuu England kusimama kwa dharura kutokana na kusambaa kwa virusi vya corona, Manchester United ilikuwa imeshika kasi kufukuzia nafasi nne za juu kwenye msimamo.
Walikuwa wameshinda mechi 10 za mashindano yote, ambapo rekodi inaonyesha kuwa mara ya mwisho kufungwa ilikuwa ni Januari 22. Kutua kwa kiungo fundi wa Ureno, Bruno Fernandes aliyesajiliwa kwenye dirisha la Januari kuliongeza ubora wa kikosi cha Kocha Ole Gunnar Solskjaer.
Hata hivyo, bado bosi kubwa wa wababe hao wa Old Trafford, Ed Woodward hapati usingizi kutokana na kupambana kuwashusha kikosini mastaa ambao anaamini watairejesha Manchester United kwenye enzi zake.
Hawa hapa nyota watano ambao Ed anapambana kuhakikisha wanatua Manchester United kama si wote, basi hata wawili.

JADON SANCHO
Kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa huko Old Trafford, jina la winga wa Borussia Dortmund ya Bundesliga, Jadon Sancho, lipo. Mwaka 2017 alikuwa mmoja wa makinda hatari kwenye kikosi cha Manchester City.
Pep Guardiola na mabosi wa City walipambana kuhakikisha anabaki Etihad, lakini Sancho alikuwa na mipango mingine na kwenda kutua zake Borussia Dortmund ambako sasa amekuwa staa mkubwa na mwenye thamani kubwa.
Manchester United imejaribu mara kadhaa kwenye dirisha la usajili lililopita, lakini harakati hizo hazikukamilika. Thamani ya Sancho inatajwa kufikia Pauni 120 milioni na Woodward amepania kumshusha Old Trafford.
Hata hivyo, Manchester United itakuwa na shughuli ya kupambana na Chelsea, Liverpool na Arsenal ambazo nazo zinawania huduma ya winga huyo wa Kiingereza.

KALIDOU KOULIBALY
Kabla ya Manchester United kuvunja akaunti na kulipa Pauni 80 milioni kwa Harry Maguire, macho na mipango yote ilikuwa kwa beki wa kati wa Senegal anayekipiga Napoli, Kalidou Koulibaly.
Kwa sasa inaelezwa kuwa kwenye orodha ya mabeki wa kati bora duniani kwa yumo ukiacha Virjil van Dijk wa Liverpool basi anayefuata ni Koulibaly.
Woodward anataka kumleta Msenegali huyo Old Trafford ili kusuka ukuta wa chuma akicheza sambamba na Maguire, Victor Lindelof au Eric Bailly. Hata hivyo, Napoli ambao wanaweza kufikia makubaliano ya kumweka sokoni beki huyo hawatakuwa tayari kuanza mazungumzo bila kuwekwa Pauni 100 milioni mezani.

ERLING HAALAND
Kwenye dirisha dogo la Januari, mwaka huu, Manchester United walipewa nafasi kubwa ya kumsajili kinda wa miaka 19 Erling Haaland. Hata hivyo, mambo yakawa tofauti kabisa na mwisho kukaibuka mgogoro mzito baina ya mabosi wa Man United na wakala Mino Raiola ambaye anamsimamia kinda huyo.
Inaelezwa kuwa Raiola aliweka vipengele vya kumnufaisha zaidi kwenye mkataba wa kinda huyo jambo ambalo Man United hawakukubaliana nalo na kusitisha mpango huo, na Haaland akaelekea zake Signal Iduna Park tena kwa pesa ndogo tu.
Kwa sasa thamani ya Haaland imepanda hadi kufikia Pauni 100 milioni huku wababe kibao wa Ulaya wakiwemo Real Madrid, Barcelona na Liverpool wakifuatilia kwa karibu maendeleo ya kinda huyo aliyeanza kwa kasi ya kupachika mabao.

JAMES MADDISON
Pale Kings Power kuna dogo mmoja anaitwa James Maddison ambaye rada zake zinasoma kuwa kama siyo sasa, basi baadaye atakuwa amevaa jezi ya Manchester United.
Mara kadhaa Man United wamekuwa wakiulizia mkataba wa Maddison, lakini usajili wa hivi karibuni wa Fernandez unaweza kuzima dili hilo.
Hata hivyo, mvutano wa kiungo Paul Pogba wa kutaka kuondoka Old Trafford unaweza kufufua matumaini ya Maddison kukipiga Man United, kwani ni aina ya mchezaji ambaye Ole anataka kuwa nao klabuni kwake.

JACK GREALISH
Nahodha wa Aston Villa ambayo kwa sasa inapambana na hali yake huko chini ya msimamo wa Ligi Kuu England.
Staili ya uchezaji ya Maddison inafanana kabisa na supastaa huyo wa Aston Villa, Jack Grealish.
Viungo hawa wote wanafiti kwenye mfumo wa Ole huku suala la umri mdogo likiwaongezea sifa ya kukipiga Old Trafford.
Jack anapatikana kwa dau la Pauni 60 milioni, na kama Aston Villa itashuka daraja basi kuondoka kwake hakuna mjadala na thamani yake huenda ikashuka zaidi.
 
Back
Top Bottom