Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mkuu kwani ule mpira si ulimgonga Maguire ndio ukaingia? So lingekuwa own goal.

Sasa hata mimi sijaelewa offside imetoka wapi pale.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu imagine ile ni free kick, then mchezaji pinzani kaenda kumziba de gea, ingekuwa ni offside ama sio offside?

Ule mpira ulishakuwa offside hata kabla haujamgusa maguire, kitendo tu cha yule jamaa kumziba kipa anahesabika tayari yupo mchezoni na ni offiside.

Na kama ile sio offside basi free kick kipa angekuwa anakabwa na timu pinzani then ikipigwa free kick wale wanaokaba wanalala na mpira uingie nyavuni.
 
Nachompendea OGS kuwalinda wachezaji wake dhidi ya vyombo vya habari, sishangai kuiteka dressing room

GGMU
Screenshot_20200302-182123.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata yule kipa wa liverpool aliyewachoma kwenye fainal na madrid alilindwa na Klopp.

Nafikiri ni Managerial skills ambazo managers lazima wawenazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawezi kwenda kwenye press na kusema"De Gea ni mjinga wa mwisho kabisa"..

Kuna watu wanampenda mourinho kwa kuwa mwatukaji kwenye Press zake,kitu ambacho naona sio sahii..Ukiwa kama kocha na una ishu na mchezaji inabidi umchane yeye mwenyewe na sio kutumia press kumchana
 
Bado naamini kwa mwelekeo tunaoenda sasa tuko kwenye right track tuendelee kula mtori nyama tutazifikia hivi karibuni.

Ole anafanya kazi nzuri tuendelee kuheshimu maamuzi yake na rebuild anayofanya.
baada ya kufanya operation safisha mji (darmian, valencia, young, sanchez, fellaini, smalling) pamoja na kuleta wachezaji wengine wanne (ambao ni wan bissaka japokuwa sifurahishwi na style yake ya kiuchezaji kwenye ulimwengu huu wa kisasa, maguire amekuwa kiongozi mzuri sana kwa wachezaji, daniel james huyu natumai kilio changu cha mwanzoni wa msimu kitafanyiwa kazi na ole msimu ujao ambapo sikupendelea huyu dogo awe mchezaji wa kikosi cha kwanza, bila ya kumsahau bruno fernandez) hao wote kwa pamoja wameweza kuleta utofauti mkubwa kwenye kikosi chetu kwa muda mfupi zaidi.

ni matumaini yangu dirisha la tatu la usajili chini ya ole gunnar (tutamaliza biashara ya rebuilding kwa kutafuta wachezaji wengine sahihi hususani eneo la winga wa kulia) ila tatizo kubwa litakalobaki ni ubora wa mwalimu mwenyewe kututhibitishia ubora wake kimbinu, kiupande wangu bado namuona ole hajapevuka kimbinu ukimlinganisha na makocha wengineo wanaofundisha timu pinzani mfano jurgen klopp, carlo ancelotti, josep guardiola isala.

kuna nyakati sir alex alikuwa na kundi bora la wachezaji na hatimaye akafanikiwa kulitawala soka la england (1999, 2008-2009 na wapinzani wake wakasema anabebwa na timu bora pamoja na bajeti), vile vile kuna nyakati sir alex alikuwa na kundi la wachezaji wenye viwango vinavyotabirika (2010.-2012) kabla ya kuingia uwanjani ila pia alifanikiwa kulitawala soka la england na cha ajabu zaidi aliweza kucheza robo fainali ya ligi ya mabingwa takribani mara tatu ndani ya miaka minne kama nitakuwa nipo sahihi.

Hivyo basi ubora wa rebuilding unaofanywa na mwalimu hautoshi kuthibitisha ubora wake katika kuongoza timu kubwa kama manchester united (ole gunnar anapaswa kupevuka zaidi kama anahitaji kudumu man utd kwa muda mrefu zaidi, mfano mdogo tumeshacheza na wolves takribani mechi sita kwa siku za karibuni lakini mpaka leo tumeshindwa kupata tiba ya kimbinu dhidi yao).

sote hatufahamu anachokiwaza ed woodward (mzee wa suprise) kwenye mtindio wa ubongo wake, tukumbuke mara nyingi amekuwa akitamka hadharani ya kwamba klabu itaendelea kufanya kazi na ole msimu ujao kwa sababu ya kuvutiwa na mipango yake ndani ya klabu, hata nyakati za louis van gaal alimpaka mafuta kwa mgongo wa chupa na mwisho wa msimu akavunja mkataba wake licha ya kubeba ubingwa wa FA dhidi ya crystal palace na sababu kubwa anayoiangalia zaidi ni tiketi ya UEFA.

kivyovyote itakavyokuwa mwalimu yeyote atakayekuwepo msimu ujao atakuwa amebakiwa na kazi ndogo sana ya kukamilisha rebuilding ya kikosi chetu ambayo imeanza kufanywa na ole gunnar solskjaer...... ni mwendawazimu pekee ndiye atakayekuja na mkakati mpya wa kujenga timu na kuutelekeza huu uliopo.

  1. david degea au dean henderson
  2. wan bissaka + ( dalot au Ethan Laird )
  3. luke shaw + brandon williams
  4. eric bailly + lindeloff + tuanzebe
  5. harry maguire
  6. scott mctominay + nemanja matic (man of the match wa mechi yetu dhidi ya everton kwa mtazamo wangu)
  7. fred + paul pogba
  8. bruno fernandez
  9. marcus rashford
  10. anthony martial
  11. daniel james + greenwood + juan mata
 
Tatizo Sigurdsson aliyekuwa katika offside position alifanya movement ambazo kwa namna moja ama nyingine ziliingilia mchezo mkuu

Ili mchezo uhesabiwe kuwa offside, sio lazima mchezaji aliye offside auguse mpira, aki influence goli kuingia kwa namna yoyote hiyo inahesabiwa kama offside

Kuna watu wanasema ule mpira ulimgonga Maguire kwahiyo sio offside. Ukweli ni ndio huo ule mpira ULIPIGWA na Lewin na Maguire ulimbabatitiza tu. Ingekuwa Maguire ndio kaupiga ule mpira goli lingesimama

Mkuu kwani ule mpira si ulimgonga Maguire ndio ukaingia? So lingekuwa own goal.

Sasa hata mimi sijaelewa offside imetoka wapi pale.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DE GEA AKALIA KUTI KAVU KISA MAGOLI YA UZEMBE

Maisha ya David De Gea ndani ya Manchester United yako shakani na huenda akapoteza namba katika kikosi cha kwanza.
Baada ya kufanya makosa ya mara kwa mara, Man United ipo njiani kufanya mazungumzo ya kumsajili kwa mkopo kipa Dean Henderson akitokea Sheffield United.
De Gea ameigharimu Man United mabao saba ambayo yametia doa ubora wake tangu alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2011 akitokea Atletico.
Kosa la kutoa zawadi ya bao kwa mchezaji wa Everton Dominic Dominic Calvert-Lewin limemuweka katika mazingira magumu De Gea.
Ingawa kocha Ole Gunnar Solskjaer anamtaja De Gea ni kipa bora duniani licha ya kufanya makosa ambayo yameigharimu Man United katika baadhi ya mechi.
Henderson (21) anatajwa ni mmoja wa makipa bora katika Ligi Kuu England. Pia kipa huyo ni mchezaji wa timu ya taifa ya vijana England.
Man United inatarajiwa kuzungumza na wawakilishi wa kipa huyo mapema mwezi huu. Henderson alisajiliwa na Man United mwaka 2015 kabla ya kutolewa kwa mkopo Sheffield.
Kipa namba mbili Sergio Romero anatarajiwa kucheza mechi ya Kombe la FA dhidi ya Derby.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NASIKIA Paul Pogba amepona. Nasikia kuna uwezekano akarudi kwenye mechi ya Manchester Derby.
Hajarudi na tayari ameshaanza kuandikwa. Mchezaji wa kwenye vyombo vya habari. Hapo kati, Man United ilipocheza bila ya huduma yake, hakuna mengi yaliyokuwa yakiandikwa kuhusu Man United. Ikishinda, ikifungwa au kutoka sare, ripoti zinakuwa za kawaida tu.
Lakini, shida ni kama matokeo hayo ingeyapata wakiwa na huduma ya Pogba uwanjani. Habari zingekuwa tofauti zaidi kama Man United ingepoteza au kutoka sare ikiwa na Pogba uwanjani. Vyombo vya habari vingeizungumzia Man United kidogo, lakini vingehamishia mjadala mkubwa kwa Pogba. Sasa yanini kuwa na mchezaji wa hivyo? Mchezaji wa vyombo vya habari?
Sawa, wachezaji wa aina hiyo kuna wakati mwingine wana umuhimu wake kuwapo kwenye timu, lakini wakati mwingine unahitaji kuwakwepa. Sasa hivi, kocha Ole Gunnar Solskjaer amekuwa akipanga mambo yake bila ya presha kwa sababu vyombo vya habari ni kama vimemsahau kimtindo. Hilo ni kwamba hakuna mchezaji kivutio kwenye vyombo vya habari. Makosa ya David de Gea yangekuwa yamefanywa na Pogba, habari ingekuwa kubwa zaidi na pengine wiki nzima ingekuwa mjadala. Lakini, kwa sasa mambo yanakwisha siku ya pili tu.
Hili linamfanya Solskjaer kuwa na muda wa kuandaa kikosi chake kwa utulivu na kuepuka presha ya vyombo vya habari. Wachezaji wote wa hivyo walikosekana kwenye kikosi hicho kwa siku za karibuni. Pogba amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu na Romelu Lukaku amepigwa bei tangu mwaka jana. Vyombo vya habari vimekuwa vikilazimisha kuandika kuhusu Anthony Martial. Lakini, hailipi sana. Kwa sasa wamehamia kwa Bruno Fernandes. Hata hivyo, bado hajaanza kukiki sana na soko lao. Sasa mtu wao, Pogba yupo njiani kurejea kwenye kikosi. Kwa sasa tochi zote zitamulikwa kwao, atafanya nini kwenye kurejea kwake katika kumalizia siku zilizobaki kwenye msimu. Si muda mrefu, vyombo vya habari vitaibuka na taarifa za kwamba Solskjaer anapasuka kichwa, hajui Pogba ampange wapi. Utasikia Fred hafai, utasikia Bruno hawezi kucheza pamoja na Pogba. Chanzo kikuu kitakuwa mchezaji wa vyombo vya habari, Pogba. Sasa mchezaji wa hivyo wa nini? Ningekuwa Solskjaer nisingefikiria mara mbili uamuzi wa kumuuza Pogba, hasa kwa kipindi hiki ambacho timu imekuwa kwenye utulivu mkubwa wakati yeye alipokosekana kwenye kikosi. Uamuzi ni wake Ole, kama atakubali kuendelea kufuatwafuatwa na vyombo vya habari kujadiliwa mambo yake kwa ajili ya mchezaji huyo mmoja, au kumwondoa na kuepukana na presha ya timu yake kumulikwa kila uchao. Ukweli ni kwamba kama kuna mchezaji ambaye amekuwa akiifanya Man United kutotulia kwa sababu zisizokuwa za maana basi ni Pogba. Leo utasikia anasema kwenye vyombo vya habari anafurahia kocha akimpanga upande wa kushoto, kesho utasikia anasema kocha amempa majukumu ya kukaba, yeye sio soka lake, lakini keshokutwa utasikia anasema anataka kwenda kukabiliana na changamoto mpya kwingineko. Ni presha tu kwenye timu. Vitu kama hivyo vinapendwa na vyombo vya habari.
Ni kitu kinachopendwa pia na wakala wa mchezaji huyo, Mino Raiola. Wakala Raiola anataka kila wakati mchezaji wake huyo awe kwenye vyombo vya habari hata kwa sababu zisizokuwa na maana. Hivi karibuni alivurugana na Ole kwa kumzungumzia mchezaji ambaye hata kucheza hachezi. Anawachimba mkwara kwamba wasipomaliza ndani ya Top Four na kufuzu kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, basi wasijiamini kwamba wataendelea kuwa na huduma ya mteja wake msimu ujao. Sasa mchezaji wa hivyo wa nini?
Jambo la kujiuliza, je Pogba tangu aliporudi Man United kuna kitu kikubwa amekifanya? Hakuna cha maana, zaidi ya kutokea tu kwenye vyombo vya habari na kubadili mitindo yake ya nywele kila mechi. Bruno anatamba kwa sasa amekuta utulivu mkubwa kwenye timu. Pogba atakaporejea, sasa hivi ataanza kujadiliwa hata nafasi yake anayocheza ndani ya uwanja. Litakuwa tatizo na kila kitu kitatibuka.
Uamuzi ni wake mwenyewe Ole kwa sababu yeye ndiye mtu wa karibu anayefanya kazi na Pogba na ndiye anayefahamu usumbufu wa wakala Raiola. Lakini, ukiniuliza mimi kuhusu Pogba, nitakwambia aendee tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe na ujinga mko sambamba....

Sijajua kwanini Ole anamprefer zaidi chong kuliko Gomez ,mimi naona chong bado sana hajatulia na anapapara sana bora Gomez anaonyesha ana kitu fulani natamani kumuona benchi zaidi kuliko huko under 23.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Chong ni winga na Gomez ni playmaker, tuna uhaba sana wa mawinga ndio maana Chong anapata muda zaidi wa kucheza.

Na wote wawili wana matatizo kwenye mikataba yao wanaweza kuondoka muda wowote, pengine msimu ujao wasiwe man utd.
 
Yaani Man united imnunue Dean Henderson kwa mkopo wakati ni mchezaji wa united yupo kwa mkopo huko Shelfield !!!?

Back
Top Bottom