Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Naona kitendo cha yule mchezaji kutoa mguu maana yake alikuwa part of the game.

Ila hizi game tatu kuanzia game ya Wtaford, Club Brugge na hii tunacheza vibaya sana defensively, tumecommit error nyingi sana ambazo kwa timu makini tungeweza kuadhibiwa.

By the way kwanini Solkjaer aliopt kendra na 3 defence midfielders ?

Sent using Jamii Forums mobile app
bila james na rashford inamake sense zaidi kucheza na midfield wengi kuliko kuforce mtu kama Perreira ama mata awe winga wa kulia. still tunamuhitaji sana Sancho, japo midfield inaonekana kidogo ina uhai tunatakiwa kama timu kubwa tusiwe tunatabirika, sasa hivi timu pinzani zitaanza kupanga wachezaji wawili wawili wamkabe bruno.
 
ANKO BRUNO PIGA KAZI, OLD TRAFFORD ILIKUWA INAKUSUBIRI WEWE TU.

KAMA bando kwenye simu yako lipo la kutosha hebu ingia ‘Google’ halafu tafuta kitu hiki; ‘George Best, Bobby Charlton, Denis Law statue’.
Itazame vizuri hiyo picha watakayokuletea. Ni kitu fulani hivi kipo nje ya uwanja wa Old Trafford, maskani ya Manchester United.
Ewaaa! Umekiona ee? Bila shaka ni sanamu hiyo. Ina hao watu watatu niliokutajia. Kwa heshima yao, maelfu ya mashabiki wa Man Utd walikubaliana kwamba wachezaji hao wa zamani wajengewe sanamu.
Walikuwa ni waburudishaji wa macho ya mashabiki zaidi ya 70,000 waliokuwa wanafurika katika dimba la Old Trafford na mamilioni ya wengine duniani kote kwa mabao waliyokuwa wanafunga.
Chini ya kocha mwenye heshima zake pale Man United, Sir Matt Busby, utatu wa mastaa hao wa zamani uliipa klabu hiyo heshima na mafanikio makubwa.
Siku hizi huwapati wachezaji wa namna hiyo, Man Utd ina Bruno Fernandes, fundi haswa. Mtaalam wa soka kutoka kule Ureno. Bahati mbaya ni kwamba ataikosa heshima ya kujengewa sanamu.
Kwanini? Kwa soka la sasa linaloendeshwa na fedha, Fernandes huenda asidumu Manchester na kupata mafanikio kwa muda mrefu.
Lakini, ni mashabiki wachache wa Man Utd wanaojali suala hilo, kwa sasa wanafurahia upako wa soka unaotembezwa pale Old Trafford. Fernandes ameiteka Manchester United.
Hizi kelele unazozisikia mjini hapa ni kwa hisani ya Anko Bruno. Kwanini usimfurahie mtu anayepiga penalti akiwa angani? Mtu mwenye uhakika wa kutoa asisti kila mechi. Kwanini usimfurahie?
Fernandes ameipa Man Utd uhakika wa mabao ya kila aina. Yeye mwenyewe ana uwezo wa kutumia vizuri mipira iliyokufa, achilia tu hizo penalti zake zinazotibu kisukari.
Ukitaka akutengenezee bao kupitia kona, muamini yeye. Ukitaka mabao ya mbali, pia, muamini Anko Bruno. Kingine kinachofurahisha kuhusu kiungo huyo raia wa Ureno, ni uwezo wake wa kuusoma mchezo.
Juzi, wakati Man United ikiibamiza Club Bruges mabao 5-0, Fernandes alionyesha utofauti mkubwa mno katika kikosi cha mashetani wekundu hao. Ni zaidi ya wachezaji wengi waliokuwa tegemeo kabla ya ujio wake msimu huu.
Ndani ya dakika tisa tu za mchezo huo alifanya mambo yote ya msingi tena kwa ubora wa hali ya juu. Alidhihirisha jinsi gani alivyokuwa hatari wakati anaitumikia Sporting Lisbon.
Ikumbukwe wakati akiwa nchini Ureno, Fernandes aliweza kufunga mabao 48 ndani ya miezi 18 ya mwisho kuitumikia klabu hiyo. Ni aina ya mchezaji ambaye alisubiriwa pale Old Trafford.
Amecheza dakika chache kuliko viungo washambuliaji aliowakuta katika klabu ya Man Utd, lakini ameanza kutishia umaarufu wao. Si Jesse Lingard, Andreas Pereira ambao wanaweza kuufikia uwezo alionao Anko Bruno. Angalau, Juan Mata.
Anko Bruno amemkuta Pereira akiwa na bao moja, asisti tatu kwenye mechi za Ligi Kuu England. Amemkuta Mata akiwa na asisti mbili tu, bila bao. Yeye hadi sasa amesha ameshafunga mara moja na asisti mbili.
Unajua kwanini sijazitaja takwimu za Lingard? Ni kwa sababu hana bao wala asisti kwenye Ligi Kuu England tangu 2018. Sasa kwanini mashabiki wa United wasimfurahie Anko Bruno?
Ilikuwa ni ngumu mno kwa mashabiki hao kufurahi wakiwaona Lingard, Mata na Pereira wakicheza zaidi ya dakika 3,000 kwenye Ligi Kuu England bila mchango wa maana.
Anko Bruno hajafikisha hata dakika 400 kwenye ligi hiyo, lakini wastani wa kuchangia bao unasomeka kila dakika 90 anazocheza. Kwa viungo washambuliaji, ni Kevin de Bruyne tu ambaye ana ubora huo.
Bila shaka zile pauni milioni 47 zilizotumika kumtoa Sporting zilikuwa ni ndogo mno. Kwa jinsi alivyoifanya Man Utd kuwa imara katika safu ya viungo, ni haki yao Sporting kuongezwa fedha.

Umesomeka vzr. Jana vs Everton bruno alikuwa pekeake, alitafuta nafasi.

Wkt mchezo ule ukiendelea kuna wachezaji wawili ama watatu wqlikuwa walisongamana eneo la middle, wanaonekana wanakimbia kama nguruwe.

Ninachoendelea kujifunza bado timu haina kiungo uzuiaji. Roy Keane hakupata mrithi.
 
Roy Keane hataki kumsamehe De Gea, anasema endapo angekua kocha angemuua kwa ule uzembe

Duuuh
Screenshot_20200302-093104.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom