Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Story huwa zinaanza hivi hivi, na bodi huwa inatoa hakikisho hivyo hivyo.... Hata kipindi cha Jose ilikuwa hivyo hivyo
skysports___B7qIVhdg5ZY___.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana na mimi naona huyu jamaa ni tatizo zaidi

Anapenda sana kuwa kocha wa United kiasi cha kwamba yupo tayari kuongea ujinga ili asiwauzi wakubwa. Haka kajamaa wakati Glazer ana take over United kalikuwa very critical, sasa hivi unaweza dhani ni mtu mwingine kabisa, kumbe unafiki sio bongo tu hata wazungu wapo

Hawezi kuwaambia ukweli kwamba kuna mapungufu hapa na hapa, kanapiga siasa tu ili kaendelee kuwepo kwenye timu , sina uhakika kama atafikisha hata mechi 100 huyu jamaa

Lakini hata mbinu zake nimekuwa na mashaka nazo, too predictable, too rigid, too boring

Sent using Jamii Forums mobile app
Ole haongelei mambo ya ufundi kwenye press zake kitu ambacho indirectly kingekuwa kinawaanika akina ed na glazers wakafanya mambo. Kila wakati anaongelea positive moments ambazo kiuhalisia ni chache na hazishabihiani na matokeo. Kuna haja ya kumfanya Haji Manara (msemaji) wetu kuliko mkuu wa benchi la ufundi.
 
Ndio maana na mimi naona huyu jamaa ni tatizo zaidi

Anapenda sana kuwa kocha wa United kiasi cha kwamba yupo tayari kuongea ujinga ili asiwauzi wakubwa. Haka kajamaa wakati Glazer ana take over United kalikuwa very critical, sasa hivi unaweza dhani ni mtu mwingine kabisa, kumbe unafiki sio bongo tu hata wazungu wapo

Hawezi kuwaambia ukweli kwamba kuna mapungufu hapa na hapa, kanapiga siasa tu ili kaendelee kuwepo kwenye timu , sina uhakika kama atafikisha hata mechi 100 huyu jamaa

Lakini hata mbinu zake nimekuwa na mashaka nazo, too predictable, too rigid, too boring

Sent using Jamii Forums mobile app

Ole n tactiless hana mbinu yoyote no game plan united hatuna pattern on how tunacheza

Ukiachana n ki uchezaji na legacy yake ole ki ukocha n mdogo sana kwa man u ndo mana bado anaendlea kuwa puppet wa edwood n glazer

Tunafeli kusajili cause anashindwa kumshinikiza edwoord kusajili wachezaj wametoka wachezaj with only 3 replacement

ana tumia mda mwng kwe press conference kutoongelea madhaifu anaishia kum boycot edwood kulinda kibarua chake hakisahau klabu ndo inazid ku sink.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
OLE GUNNAR AISHIWA MBINU SASA AOMBA MSAADA KWA WATAALAMU




KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer anatafuta mtaalamu wa saikolojia kwenye michezo kwenda kutibu vichwa vya wachezaji wake kutokana na matokeo ya hovyo wanapokabiliana na timu ndogo.
Solskjaer anaamini kuna tatizo sehemu linalowakabili wachezaji wake wanapocheza na timu ndogo kwa sababu viwango vyao vinakuwa tofauti na wanaposhuka uwanjani kuzikabili timu vigogo.
Jambo hilo linamtia shaka kocha huyo akisema kwenye mechi kubwa, mastaa wake wanawasha moto kwelikweli, lakini wanapocheza na timu zinazopambana zisishuke daraja, wanakuwa hovyo uwanjani na kupoteza kirahisi sana.
Jana Jumatano usiku, Man United ilitarajia kumenyana na Burnley kwenye Ligi Kuu England na kocha Solskjaer anatafuta mtu wa saikolojia kuwatibu wachezaji wake ili kutokuwa na tabia hiyo ya kubagua mechi.
Man United ndiyo timu pekee iliyogawana pointi na Liverpool msimu huu huku wakiwachapa pia Manchester City uwanjani kwao Etihad. Wamezichapa timu ngumu pia za Leicester City, Chelsea mara mbili — 4-0 kwenye Ligi Kuu England na 2-1 kwenye Kombe la Ligi na wakiwachapa pia wasumbufu Wolves. Lakini, utashangaa imechapwa na Watford, Bournemouth, West Ham, Newcastle na Crystal Palace — wakitoka sare pia na Aston Villa.
Jambo hilo linamfanya kocha Solskjaer kushindwa kuielewa timu yake na hivyo sasa anahitaji msaada wa nje kuja kurekebisha mambo.
Man United waliichapa Burnley 2-0 uwanjani Turf Moor mwezi uliopita, lakini walihitaji mabao mawili ya dakika za mwisho kupata sare nyumbani msimu uliopita.
Solskjaer alisema: “Kila wakati tunapocheza na Burnley shughuli inakuwa pevu. Wanakuwa wasumbufu uwanjani utashani wameshinda mechi tano mfululizo.”

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Just imagine man u wanafika 2040 hawajabeba league watu wanaanza kuandika : last time man u wanabeba ubingwa VAR haikuwepo madogo wanashangaa, sijui ooh ikulu ilikuwa Dar , mara ooh daraja la kigamboni halikuwepo mda huo yapo matatu sijui salenda , jangwani mpaka kisiju .... Mara oooh chama kikuu cha upinzani kilikuwa chadema mda huo chauma ndio watawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
POCHETTINO NA MAN UTD WAPO MEZANI.





Lisemwalo ni kwamba Mauricio Pochettino yupo kwenye mazungumzo na mabosi wa Manchester United kwa ajili ya kwenda kumbadili kocha Ole Gunnar Solskjaer huko Old Trafford.
Muargentina huyo amekuwa akihusishwa na kwenda kukalia kiti cha moto huko Old Trafford baada ya kufutwa kazi Tottenham Hotspur, Novemba mwaka jana.
Iliaminika pia angeenda kuchukua mikoba ya kuinoa Manchester United wakati Jose Mourinho alipofutwa kazi Desemba 2018, lakini wababe hao wa Manchester waliamua kumchukua jumla Solskjaer baada ya kuwaonyesha kiwango bora kwenye mechi zake za kwanza alipokuwa kocha wa muda.
Lakini, sasa mabosi wa Man United wanafikiria kufanya uamuzi sahihi baada ya timu kutokuwa na matokeo yanayoeleweka. Taarifa za kutoka Italia zinadai kwamba Man United wameshaanza mazungumzo na Pochettino, ambaye pia yupo tayari kwenda kupiga mzigo huko Old Trafford.
Man United ya Solskjaer imekuwa haeleweki kiwango chake cha uwanjani na jambo hilo ndilo linalodaiwa kuwafanya mabosi wa miamba hiyo kufikiria kumleta mtu atakayekuja kuleta mambo matamu.
Kocha mwingine anayedaiwa kwamba anaweza kufikiriwa kwa haraka kwenda kumbadili Solskjaer ni Mtaliano, Max Allegri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAN UTD YAPIGWA BAO JINGINE




MAISHA ndivyo yalivyo, mwenye kisu kikali ndiye anayekula nyama.
Si unajua kwamba Manchester United kwa muda mrefu wanatajwatajwa kwenye mpango wa kumsajili beki wa kati wa Napoli, Kalidou Koulibaly?
Basi sasa mpango huo unaweza kukwama kwa sababu kuna watu na pesa zao wameingilia kati na wanahitaji saini ya beki huyo wa kimataifa wa Senegal. Ni Paris Saint-Germain buana, ndio wanaomtaka beki huyo mwenye umri wa miaka 28.
Taarifa za huko Italia zinaweka wazi kwamba beki huyo kwa sasa yupo tayari kuachana na Serie A baada ya kukerwa na Napoli kumfuta kazo kocha Carlo Ancelotti.
Na sasa La Gazzetta dello Sport linaripoti kwamba Paris Saint-Germain wameibuka mstari wa mbele kwenye vita ya kunasa huduma ya beki huyo, wakimwaandalia mkataba wa miaka minne wenye thamani ya Pauni 10.2 milioni kwa mwaka.
Kinachoelezwa ni kwamba mkurugenzi wa michezo wa PSG, Leonardo ameshaanza mazungumzo na wakala wa Koulibaly na kwamba wameshaweka mezani mkwanja wa Pauni 41 milioni na kwamba kwa mwaka unaweza kuongezeka kwa Pauni 4.2 milioni kutokana na kile timu itakachofanikiwa ndani ya uwanja.
Lakini, inaripotiwa Napoli wao wanataka Pauni 100 milioni kwenye mauzo ya mchezaji huyo jambo linalozifanya timu nyingi kukwama kwenye kumsajili kutokana na mkwanja huo mrefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JE NI WAKATI WA GLAZZER KUIUZA MANCHESTER UNITED AMA OLE GUNNAR KUONDOLEWA?




Manchester United walizomewa na mashabiki wao baada ya Burnley kuweka ushindi wa kwanza katika uwanja wa mechi ya ligi ya Uingereza katika uwanja wa Old Trafford jana Jumatano usiku.Burnley walichukua uongozi kabla ya kipindi cha kwanza baada ya Chris Wood kufunga akiwa maguu sita.Jay Rodriguez aliongeza bao la pili na kuwapatia The Clarets fursa wakati aliposhirkikana na Wood katika nipe nikupe kabla ya kupiga kombora kali kutoka kona ya upande wa kushoto lililomwacha kipa Davdi de Gea bila jibu.Ni msimu wa tatu mfululizo kwa Burnley kuwa mbele 2-0 katika uwanja wa Old Trafford, lakini ni mara ya kwanza ambapo walizuia na kutoka na ushindi wa pointi zote tatu.United waliokosa huduma za mshambuliaji nyota Marcus Rashford , walikuwa na bahati mbaya katika kipindi kirefu na hakuwakuweza kumtishia kipa wa Burnley Nick Pope.Walisomewa katika kipindi cha mapumziko na baada ya mechi kukamilika na mashabiki wengi walitoka katika uwanja huo katika kipindi cha dakika tano za mwisho.Mazungumzo mengi yalikuwa jinsi Man United itakavyocheza bila Rashford ambaye anauguza jeraha kwa kipindi cha wiki sita.Hiyo ilimpatia fursa Anthony martial kuonyesha umahiri wake kama mshambuliaji wa nyota wa United, akini mshambuliaji huyo alishindwa kufurukuta katika kipindi chote na alikosa nafasi nzuri katika kipindi cha kwanza kupitia pasi za Wan -Bissaka na Nemaja Matic.Solskjaer alimuingiza kinda mason Greenwood katika kipindi cha kwanza na kijana huyo alionyesha umahiri wake baada ya kumchenga Charlie Taylor na kupiga nje. Hatahivyo hmatokoe hayo ynaweza kuishinikiza United kununua wachezaji wapya katika dirisha dogo la uhamisho la mwezi Januari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • sheffield anashika nafasi ya 8 na amezidiwa kwa alama 1 na manchester united wanaoshika nafasi ya 5
  • southampton anashika nafasi ya 9 na amezidiwa kwa alama 3 na manchester united wanaoshika nafasi ya 5 (mechi 10 za mwisho wamepoteza mechi mbili na draw 1)
  • newcastle anashika nafasi ya 14 na amezidiwa kwa alama 4 na manchester united wanaoshika nafasi ya 5.
  • brighton wanashika nafasi ya 15 na amezidiwa kwa alama 9 na manchester united wanaoshika nafasi ya 5
  • wattford anashika nafasi ya 19 na amezidiwa kwa alama 11 na manchester united wanaoshika nafasi ya 5.
  • norwich anashika mkia amezidiwa kwa alama 17 na manchester united
01/02 = tunacheza nyumbani dhidi ya wolves
17/02 = tunacheza ugenini dhidi ya chelsea
23/02 = tunacheza nyumbani dhidi ya watford
01/03 = tunacheza ugenini dhidhi ya everton
07/03 = tunacheza nyumbani dhidi ya ma city
14/03 = tunacheza ugenini dhidi ya tottenham
Hizo fixtures zilivyokuwa nasikia harufu ya kutimuliwa mtu hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom