Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

kabla ya kufikia makubaliano ya kumpa mkataba jose mourinho:
  • je bodi walikuwa hawafahamu ya kwamba huyu jamaa (mourinho) ni mtumiaji wa pesa sana kama alivyofanya chelsea na real madrid?
  • walikuwa hawafahamu ya kwamba jose mourinho huwa hapendelei sana kuangalia umri wa mchezaji pindi anapohitaji huduma yake ( rejea usajili wa ibrahimovic, samuel etoo, michael ballack, diego millito, carvalho ricardo kuelekea real madrid)
  • je! bodi ya klabu walipokuwa wanampa mkataba jose mourinho walikuwa hawafahamu ya kwamba huyu jamaa hana tabia ya kuwavumilia wachezaji wake pindi wanapokuwa ovyo au asipowahitaji (kwa mfano pendekezo la kutafutwa mchezaji wa kuziba nafasi ya mkhitaryan aliyeshuka kiwango, pia rejea usajili wa ashley cole kwenda chelsea na william gallas kwenda arsenal)
bila ya shaka walikuwa wanayafahamu yote na ndio maana walifikia makubaliano pande zote mbili ya kufanya kazi kwa pamoja.

namnukuu ed woodward
===== tuko vizuri sana kwenye eneo la kibiashara kuliko timu yoyote duniani na matokeo ya ndani ya uwanja hayaleti athari kubwa sana kwenye biashara zetu.
===== manchester united ndiyo timu pekee yenye uwezo wa kumsajili mchezaji yoyote kwenye soko la usajili bila ya kupata athari yoyote na kwa hilo namuahidi kocha nitayafanyia kazi mapendekezo yake

kwa nini manchester united walishindwa kumtimizia baadhi mahitaji yake haliyakuwa ed woodward ameshajisifu mara nyingi sana ya kwamba klabu ina uwezo wa kumsajili mchezaji yoyote anayetakiwa na mwalimu?

kuhusu kushindwa kuwatumia ipasavyo wachezaji wake aliowasajili nalo pia si geni kwa jose mourinho kwani huko nyuma alishawahi kufanya vimbwanga kama hivyo (rejea usajili wa asiel del horno,lassana diarra, shevchenko, mateja kezman) na ndio maana nikauliza hapo juu kuhusiana na utambuzi wa bodi juu ya suala hili kabla hawajampa kandarasi jose mourinho.

pia mourinho si kocha pekee mwenye tabia mbovu kama hiyo ya kushindwa kuwavumilia wachezaji wake pindi wanapocheza chini ya kiwango hata josep guardiola pia anayo tabia hiyo na bado ameendelea kuwa nayo tabia hiyo (kwa kuwa ni guardiola basi hakuna anayehoji)
  • wakati guardiola anamuondoa nolito ambaye alimsajili yeye mwenyewe kwa kutokuendana na falsafa yake msimu wake wa pili alionekana malaika lakini mourinho alipomuondoa mkhitaryan kwa kushindwa kuwa kwenye kiwango msimu wake wa pili alionekana ni mwanadamu asiyekuwa na chembe ya uvumilivu.
  • guardiola alimsajili claudio bravo akashindwa kufikia matarajio yake na hatimaye msimu wa pili akatumia tena fedha nyingi kwa usajili ederson (ndani ya misimu miwili josep guardiola alitumia takribani paundi millioni 70 kwa usajili wa magoal keeper)
  • wakati guardiola anasajili walinzi wawili wa kushoto (benjamin mendy na laporte) huku akimuondoa mlinzi mwengine mahiri ambaye ni kolarov alionekana ni malaika lakini mourinho alipoomba apewe fungu la usajili kwa ajili ya alex sandro alionekana ni shetani asiye na uvumilivu, unabaki kujiuliza kama ni guardiola je angeliendelea kumtumia luke shaw na ashley young kama walinzi wake haliyakuwa amemuondoa alexandre kolarov na gael clichy?
  • guardiola alimsajili zlatan ibrahimovic na msimu uliofuata alimuondoa na nafasi yake ilizibwa na david villa kama nitakuwa nipo sahihi.
  • kama guardiola aliweza kuwandoa wachezaji kama joe hart, bacary sagna, gael clichy, zabaleta pablo, alexander kolarov, samir nasri, jesus navas, wilfried bony, mangala, martin demicheliss na kelechi iheanacho ndani ya misimu miwili je. kama angelikuwepo manchester united angeliendelea kufanya kazi na wachezaji kama smalling na phil jones kwa moyo mkunjufu.?
yaliopita si ndwele na tunapaswa tugange yajayo
twende na Ole gunnar solskjaer japo kishingo upande huenda akatufikisha kwenye safari yetu ya matumaini.
nafasi ya nne bado ipo wazi
Sawa mkuu nimekuelewa, leo vijana wajitaidi watupe furaha dhidi ya everton

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vita nafasi ya 4

Wapinzani wanaofuata kwa Man Utd na Chelsea

Man Utd VS Everton, Watford, Newcastle & Burnley

Chelsea Vs Tottenham, Southampton, Arsenal & Brightom

Kaugonjwa ka mechi ndogo kasiturudie

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunapocheza na timu ndogo kipind cha kwnza uwa tunapotea sana, uwa tunaamka 2nd half, OGS alifanyie kazi hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Liverpool wanaanza kumnyatia Takumi Minamino January, wakati huo United haina playmaker wa kueleweka na imetulia tu.
Hakuna maana kusajili mtu wakuja kujaribu kama ataweza, unasajili mtu wa uhakika kiufupi mtu amesha onyesha kudumu kwenye kiwango kwa misimu kadhaa. Vijana wakujaribu wapo wengi kwenye academy yetu tunaweza wapandisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mkuu nimekuelewa, leo vijana wajitaidi watupe furaha dhidi ya everton

Sent using Jamii Forums mobile app
swadkata brother
ushindi dhidi ya everton ndio jambo muhimu zaidi kwa nyakati hizi (ole anazihitaji zaidi hizi mechi nne zijazo kwa lengo la kututhibitishia uwezo wake dhidi ya timu ndogo, vile vile ushindi dhidi ya everton utatupelekea kupunguza utofauti wa alama kutoka nane zilizokuwepo takribani wiki mbili zilizopita hadi alama 2 dhidi ya chelsea).

si vibaya kuyajadili mambo yaliopita kama tutakuwa na lengo la kujisahihisha na si kumtafuta mchawi aliyepelekea anguko letu, kama tutaamua kumtafuta mchawi basi hakuna atakayebaki salama kuanzia fergie mwenyewe aliyetuletea david moyes a.k.a the choosen one hadi ole mwenyewe aliyetuondolea romelu lukaku

adui yetu mkubwa ambaye ni chelsea kwa sasa hali yake imeshakuwa dhoofu, tunahitaji kumsukuma kutoka kwenye kilele cha mlima
================================
When Manchester United take on Everton on 15 December, it will be the 4000th senior match in succession in which at least one youth graduate is represented in the Reds’ first-team or matchday squad.
 
Nadhani kuna wakati Magazeti yanatafuta habari za kuuza, Haya Magazeti ya Mirror, Dail Mail, The Sun n.k. hayaaminiki kiivyo mkuu

Usajili wa Sancho January ni impossible, hakuna timu makini (Dortmund ni makini) ambayo itakuwa tayari kuuza mchezaji wake muhimu katikati ya msimu ambapo wana kampeni ya UCL, wana kampeni muhimu kwenye ligi yao

Na usajili wa Sancho July unategemea sana kama tutamaliza top 4 au lah, jambo ambalo mpaka sasa ni kitendawili kwetu

kuna taarifa fulani nimeiona jana inadai ya kwamba matt judge amekutana na wawakilishi wa jadon sancho... kuna ukweli wowote kuhusiana na taarifa hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
It is a matchday...uuuuuuuuhuuu

C'mon United!!!

Aisee naomba sana Daniel James(DJ) afunge goli..it's been a while..nitakuwa more than happy

Ole inabidi aingie kwa kasi ya ajabu..Toffies inabidi walale mapema sana,ili tuwe 2 clear points from Top Four

Tukikosa point tatu leo,tunarudi tena hatua kumi nyuma

GGMU
 
Mzee mimi shauku yangu ni Martial aondoke na mpira
It is a matchday...uuuuuuuuhuuu

C'mon United!!!

Aisee naomba sana Daniel James(DJ) afunge goli..it's been a while..nitakuwa more than happy

Ole inabidi aingie kwa kasi ya ajabu..Toffies inabidi walale mapema sana,ili tuwe 2 clear point from Top Four

Tukikosa point tatu leo,tunarudi tena hatua kumi nyuma

GGMU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee mimi shauku yangu ni Martial aondoke na mpira

Sent using Jamii Forums mobile app
Unamkubali sana nini??...au unaona tu kwamba anadeserve??

Maana mimi nimesema hivyo kwa Daniel James maana dogo anapambana sana,anatoa pasi za mwisho nyingi nzuri lakini wanashindwa kumalizia..natamani sana afunge,

Na leo nahisi atatupia..let's wait
 
Mzee mimi shauku yangu ni Martial aondoke na mpira
robin van persie ndiye mchezaji wa mwisho wa man utd kufunga hatrick na ilikuwa dhidi ya aston villa takribani miaka saba iliopita.
1576409143047.png
 
Back
Top Bottom