Hizi picha zimenikumbusha ugomvi uliokua ukizuka kati ya Keane na Vieira.Ugomvi usioisha
Roy Alikuwa Mtata sana,Baada ya Eric Cantona Kuondoka Jamaa akawa zaiidi ya Mtata,Anakemea Uzembe na uvivu dimbabi kwa kila njia iwe ngumi au Mateke na sentensi za Makaripio lukuki.
Ferguson aliwahi kuelezea njisi alivyo Muondoa Old Trafford,Ilifika kipindi Roy aliingia Mutv kisha akawapa Makavu/Maneno mazito karibia kila Mchezaji,
Mfano Fletcher aliambiwa kurukaruka kwakwe uwanjani tayari kashajiona superstar akirudi Taifa basi bichwa hilo.
Wachezaji waliokuwa na uwezo walau kidogo wa kusimama naye hata kwa kujibu vijineno viwili vitatu walikuwa Van N & Edwin Van D,Wengine Wote kama kondoo.
Ferguson alivyoona hivyo akamuita kisha akamwambia shukrani kwa kazi iliyofanya klabuni,Nadhani ni Wakati wa Kuagana kwa Amani.
Roy Akasema Mzee hukuwa hivi Umebadilika haya si maneno yako,Mzee akijibu haya mabadoliko ndio yanifanya niwepo hapa..
Roy Keane alikuwa anamgwaya sana Eric Cantona,Eric alikuwa ni chuma cha Pua mbaya zaiidi Jamaa alikuwa msomaji mzuri wa vitabu na Falsafa lukuki za akina Hegel mpaka Kwa mbabe wa Alexander The Great bwaana Diogenes of snope..
Kuna picha nimeiweka ya Eric Cantona akitoka Uwanjani akiwa na polisi huko Uturuki mechi ilikuwa ya vurugu Uefa,Walivyoingia vyumbani wachezaji Wote Jamaa akataka arudi uwanjani amtafute moja wa askari aliyemzongazonga amgawie dozi kamili,
Wachezaji Wote, wengine wakipiga magoti wakimuomba asirudi uwanjani itakuwa balaaaa sana,Jamaa Mzuka Ukopoa.
Roy & Vieira Wameacha Alama na burudani Epl.....Great Captains.