Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kumbuka Maguire ni £80

Fred £60m

Wachezaji ghali hao
Ni wachezaji ghali lakini kiuhalisia hawana thamani hiyo, fred ana uwezo mdogo kuliko Wjinaldum wa Liverpool aliyenunuliwa kwa £25m.

Kuhusu Maguire sishangai kwa wachezaji wa kiingereza kuuzwa bei mbaya refer bei ya Andy Carrol kwa wakati ule, subiri bei ya bwana mdogo wa Leicester James Maddison itakavyokuwa kubwa.
 
Abraham anaweza vipi?

Management mambo ya mpira ni zero huwez uza lukaku na herrera kwa mpigo bila replacement kupata
Unaloongea ni kweli Management pia ni tatizo, brand ya Man u ni kubwa sana ukilinganisha na wachezaji waliopo, united inahitaji world class players kama 4 hivi angalau iweze kushindana na Liver pamoja na city
 
kama solskjaer ataendelea kuwepo nakuhakikishia atamsajili mmoja kati ya hao ndugu wawili, unadhani kwa sajili za ovyo kama hizo zitatutoa kwenye dimbwi la dhoruba?
never ever​
kuna muingereza mmoja tu ndiye mwenye uwezo wa kuichezea manchester united na si mwengine ni james maddison.
sijamtaja harry kane kwa sababu bei yake ni ghali sana

Huyu james Maddison ni mchezi hatari sana. Pia bado umri wake mdogo natamani aje aichezeee chelsea aisee
 
Unaloongea ni kweli Management pia ni tatizo, brand ya Man u ni kubwa sana ukilinganisha na wachezaji waliopo, united inahitaji world class players kama 4 hivi angalau iweze kushindana na Liver pamoja na city
Mkuu man u inahitaji DIRECTOR OF FOOTBALL, kama world class wameshakuja hapo man u lkn hakuna kitu,

Huyo Fred ametoka shaktar akiwa moto

Maguire huyu sio muda mtamkataa

DOF ni muhimu kuliko chochote hapo man u ,huyo ndiye atasimamia Recruit nzima ya wachezaji , Kuleta world class sio suluhisho .

DIRECTOR OF FOOTBALL NI NANI? ANAFANYA NINI NDANI YA KLABU?

MICHAEL Zorc. Anatajwa kama 'director of football' bora zaidi duniani. Amekua akiifanya kazi hii kwa zaidi ya miaka 20 sasa akiwa Borussia Dortmund. Klabu yake ya maisha. Ndio. Borrusia Dortmund ni klabu ya maisha yake. Misimu 17. Mechi zaidi ya 500 kama mchezaji. Misimu 21 sasa kama 'director of football'.

Alianza kuitumikia Dortmund tangu akiwa na miaka 16, akastaafu mwaka 1998. Muda mfupi baada ya kuachana na soka, alianza majukumu mapya kama 'director of football' wa Dortmund. Amekua akiifanya kazi hii kwa mafanikio makubwa. Ndio maana amekua akitajwa kuwa bora.

Dortmund inasifika kwa kutengeneza wachezaji wengi mahiri na bora. Inasifika pia kwa kuwa na mfumo bora wa uongozi kuanzia kwa wachezaji, makocha hadi bodi ya klabu. Mfumo wa utendaji kazi ndani ya klabu upo chini ya Michael Zorc.

Wakati anacheza soka, alifahamika zaidi kwa jina la utani la 'Susi'. Jina lililotokana na staili yake ya kuachia nywele ndefu kichwani. Alishawahi kuwa nahodha wa Dortmund kwa kipindi kirefu. Anakumbukwa pia kwa uwezo wake mkubwa wa kufunga mabao kwa penati.

Mwanzoni mwa mwaka 2017 alihusishwa kujiunga na Arsenal. Ili aifanye kazi yake ya 'director of football'. Kwenye kipindi hiki, Arsenal haikuwa na mtu kwenye nafasi ya 'director of football'. Shughuli zote zinazoihusu klabu zilikua chini ya Sir Chips Keswick kama mwenyekiti wa klabu na Arsene Wenger kama kocha.

Mzee Arsene Wenger alishangazwa sana na habari hii. Aliiona ni habari isiyokua na ukweli. Tangu aanze kuifundisha Arsenal hakuwahi kuwa na mtu kwenye nafasi ya 'director of football'. Hakuamini na hakuwa akiifahamu kazi ya mtu wa aina hiyo ndani ya klabu.

"Director of football? Ni nani mtu huyu? Siijui kazi yake. Au ni mtu anayesimama na kuawaelekeza wachezaji huku ni kulia na huku ni kushoto?". Haya yalikua ni majibu yake baada ya kuulizwa kuhusu habari za Arsenal kutaka kumuajiri Michael Zorc.

Wenger aliendelea kusimama kwenye kile alichokiamini. Hakuwa anaiona kazi ya 'director of football' ndani ya klabu. Aliamini yeye ni kocha na maneja wa Arsenal. Ataamua mambo yote ndani ya uwanja. Yeye ndiye bosi wa Arsenal, maswala yote ya kiufundi yapo chini yake. Atahusika na mipango yote ya klabu.

Siku chache zilizopita Ed Woodward ambaye ni makamu-mtendaji wa Manchester United aliulizwa swali kuhusu uwezekano wa klabu yake kuajiri mtu akayefanya kazi kama 'director of football'.

Alijibu,

"tutaendelea kufanya uwekezaji muhimu kwenye kikosi chetu cha kwanza, akademi yetu na kwenye kitengo chetu cha kusaka vipaji. Huu ni mpango wa muda mrefu wa kukijenga kikosi chetu na ni mpango sahihi".

Maneno yake yalimaanisha kwamba, Manchester United haina mpango wa kuongeza mtu mwingine kwenye nafasi ya uongozi wa klabu. Hii ina maana kwamba klabu haijaona umuhimu wa 'director of football' ndani ya klabu. Kwamba mfumo wa utendaji kazi ndani ya klabu ni 'sahihi'.

Sikushangazwa na kauli hii. England ni moja kati ya nchi barani Ulaya ambayo klabu zake zilichelewa sana kuajiri mtu kwenye nafasi ya 'director of football'. Nafasi na kazi yake ndani ya klabu ilikua haifamiki au imekua ikileta mgawanyiko mkubwa.

Swali la msingi la kujiuliza. 'Director of football' ni nani? Ana kazi gani ndani ya klabu? Ukimuuliza Michael Zorc swali hili, atabasamu kidogo kabla ya kulijibu. Hii ni kwa sababu amekua akiifanya kazi hii kwa miaka mingi. Anajua kila kitu kuihusu kazi hii. Huwa anatamani kazi yake ifahamike zaidi kwa watu wengi. Kama vile kazi ya kocha inavyofahamika.

Kwa miaka mingi, kocha amekua na majukumu ya kuhakikisha anakisimamia kikosi cha kwanza, akademi na vikosi vya vijana kama bosi. Anafundisha falsafa zake ambazo anaamini ni bora kwenye kupata ushindi. Anakua na kazi ya kusimamia uhamisho wa wachezaji. Kuuza na kununua.

Anasimamia vitengo vyote ndani ya klabu. Kuanzia kile cha kutafuta wachezaji vijana hadi kitengo cha madaktari. Kocha anakua na kazi ya kutengeneza na kusimamia mipango ya muda mrefu ya klabu. Ndio maana kocha hakutambulika kama kocha pekee. Alitambulika kama meneja wa klabu. Alikua na majukumu mengi.

Kocha si mtu aliye na uhakika wa kudumu kwenye nafasi yake kwa muda mrefu. Ikaonekana kwamba, si busara kocha kupewa majukumu yote makubwa ndani ya klabu. Ni vyema kuwe na mtu mwingine atakayehakikisha anaisimamia mipango ya klabu. Halafu kocha awe na jukumu la kusimamia na kuifundisha timu.

Hapo ndipo nafasi ya 'director of football' ilipoanzishwa na klabu mbalimbali kuanza kuajiri watu kwenye nafasi hii. Kazi yake ndani ya klabu ikawa ni kusimamia vitengo vyote ndani ya klabu.

Kusimamia upatikanaji wa wachezaji vijana, wachezaji wa kikosi cha kwanza na kusimamia upatikanaji wa kocha mpya. Yaani 'director of football' ndiye anayetafuta na kupendekeza jina la kocha mpya kama yule wa zamani ataondoka.

Anakua na kazi ya kuanzisha na kusimamia falsafa ya klabu. Falsafa ya klabu inajumuisha mambo mengi ikiwemo namna timu inavyocheza. Falsafa hii hufundishwa zaidi kwenye akademi na vikosi vya vijana.

Huku kwenye kikosi cha kwanza kocha anakua na uhuru wa kufundisha soka lake ingawa ni vyema kama kocha huyu ataindeleza falsafa na tamaduni ya klabu. Ndio maana jukumu la kutafuta kocha linakua chini ya 'director of football'. Yaani kocha atakayeajiriwa ni yule aliyeaminika mbele ya 'director of football' kuendeleza falsafa ya klabu.

'director of football' anakua na kazi ya kuhakikisha wachezaji waliopendekezwa na kocha wanapatikana. Yaani 'ana-negotiate' bei na gharama ya usajili na kusimamia mikataba yao. Hapa anakua na kazi ya kujadiliana na kocha kwanza kabla ya kumsajili mchezaji aliyependekezwa.

Ndio maana kazi hii inahitaji mtu ambaye alishawahi kucheza soka zamani. Huyu ni mtu anayefahamu zaidi jinsi soka lilivyo. Anafahamu mchezaji gani atakua muhimu na ataleta faida ndani ya klabu kulingana na falsafa ya klabu ilivyo.

'director of football' anasimama kama daraja kati ya kocha na bodi ya klabu. Mabosi, wakurugenzi na wamiliki wa klabu. Mapendekezo yote ya klabu kutoka kwa kocha yanapitia kwake kwanza kabla ya kufika kwa viongozi wa juu wa klabu.

Anakua na kazi ya kusimamia shughuli zote za klabu zinazokihusu kikosi. Wakati mwingine analazimika kuhudhuria mazoezi kila 'session' na kuhudhuria mechi zote za klabu. Kwa kufanya hivi, atatambua makosa na mapungufu ya kikosi kwa undani zaidi.

Cheo cha 'director of football' wakati mwingine hujulikana kwa majina tofauti. Anaweza kuitwa 'sporting director' au 'technical director'. Hapa huleta mgawanyiko na kuwafanya wengi wasielewe. Hii ni kwa sababu majukumu hubadilika na kuwa tofauti kati ya klabu na klabu au nchi na nchi.

Mfano, muda mfupi kabla ya Arsenal na Arsene Wenger kutengana, kulikua na mabadiliko makubwa ya kiungozi ndani ya klabu. Aliajiriwa Bwana Raúl Sanllehí kuwa 'director of football'. Arsenal waliona Sanllehí pekee hatoshi. Wakamuajili Edu kuwa 'technical director'.

Kimsingi 'director of football' hufanya kazi za 'technical director' ingawa kuna utofauti wa majukumu kati yao. 'Technical director' ana kazi ya kusimamia na 'ku-organise' shughuli zote za kikosi cha kwanza na akademi ya klabu. Ana kazi ya kutafuta wachezaji watakaendana na falsafa ya klabu. Majukumu yake ni machache ukilinganisha na yale ya 'director of football'.

Mwishoni mwa mwaka 2016, kwa mara ya kwanza Liverpool walimuajiri bwana'mdogo Michael Edwards. Huyu aliajiriwa kama 'sporting director' yaani kama 'director of football' ingawa majukumu yake ni tofauti na ya 'ma-football director' wengine.

Kazi ya Michael Edwards ni kuisimamia Liverpool kwenye maswala ya kifedha, mauzo na maendeleo ya klabu kwa ujumla. Majukumu ya ufundi na majukumu mengine ya kikosi na wachezaji yanabaki kuwa chini ya watu wengine.

Chelsea wao baada ya kuachana na Michael Emenalo ambaye alikua kama 'technical director' aliajiriwa mwanamama Marina Granovskaia ambaye anafanya kazi kama 'director' wa klabu. Inasemekana hana uelewa mzuri kuhusiana na mambo ya kiufundi 'technical' kama alivyokua Emelano.

Mhipaniola Txiki Begiristain anafanya kazi kama 'director of football' pale Manchester City. Huyu ni mtu bora sana kwenye kazi hii. Alishawahi kuifanya kazi hii akiwa Barcelona. Ni mbobezi kwenye kazi hii. Yeye ndiye aliyesimamia usajili wa Pep Guardiola na wachezaji wengi pale City.

Manchester United wao bado hawaelewi kama kuna umuhimu wa kuajiri 'director of football', 'technical director' au 'sporting director'. Kama alivyosema Ed Woodward siku chache zilizopita, bado wanaona mfumo wao wa uongozi ni 'sahihi'. Hawana shida na mtu wa aina hiyo. Mpira una njia zake.
 
bahatisha kila kitu lakini sio kocha. liverpool alipooandoka Rafael Benitez timu alipewa Roy Hogson akasajili watu wake mizigo hali ilikuwa tete sana.
akaondoshwa timu akapewa Kenny Dalgish huyu ndio alisajili Suarez, Andy Carrol, Downing, Charlie Adam heka heka tupu.
Akaletwa Brendan Rodgers yeye alianza vizuri lakini alipoondoka Suarez na kusajili Balotelli, Benteke hali tete ndipo akaajiliwa KLOPP.

huyu mjerumani kairudisha timu relini, kikubwa mazee kocha maana kocha ndio anaamua amuuze Lukaku ili ampandishe Rashford, Herera kaondoka free.

maamuzi pekee ni kufukuza kocha lkn baada ya kujua anakuja nani, msije leta Giggs
 
kama siyo giggs watamleta rio ferdinand

Aiseeehhh ingekuwa vizuri kama bwana Eddy angekuwa humu jf akasoma hii nondo ili aruhusu ujio wa DoF ili kunusuru watu kujinyonga na kupata vidonda vya tumbo...

Hahahahahahaaaaa
 
bahatisha kila kitu lakini sio kocha. liverpool alipooandoka Rafael Benitez timu alipewa Roy Hogson akasajili watu wake mizigo hali ilikuwa tete sana.
akaondoshwa timu akapewa Kenny Dalgish huyu ndio alisajili Suarez, Andy Carrol, Downing, Charlie Adam heka heka tupu.
Akaletwa Brendan Rodgers yeye alianza vizuri lakini alipoondoka Suarez na kusajili Balotelli, Benteke hali tete ndipo akaajiliwa KLOPP.

huyu mjerumani kairudisha timu relini, kikubwa mazee kocha maana kocha ndio anaamua amuuze Lukaku ili ampandishe Rashford, Herera kaondoka free.

maamuzi pekee ni kufukuza kocha lkn baada ya kujua anakuja nani, msije leta Giggs
Mimi ningependekeza G.NEVILLE apewe timu wadau mnasemaje?
 
Manchester United are interested in signing Mohamed Elneny for a fee around £17.6m. Player identified by Solskjær and seen as ideal option to 'add bite and creativity' to United's midfield. [Various]
Aiseeeeh
 
Back
Top Bottom