Kwa sasa game yoyote kwa United ni ngumu, hata dhidi ya Newcastle.... Ni siri iliyo wazi kuwa United hawapo kwenye good form na wana wachezaji majeruhi ambao ni muhimu
Lakini ni kosa kubwa kuidharau United itakapokuwa inacheza na timu kubwa (top six) kwani hizi timu zinafunguka na kuacha nafasi inayoweza kuruhusu game ya United/OGS (counter attacking football)
Kuna watu wanajiuliza Chelsea walipigwaje na United hii, nashindwa kuelewa wanashindwaje kupata majibu
United ina creative players wachache na inacheza zaidi counter attacking football. Aina hii ya mchezo inawatesa sana wanapokutana na timu ndogo zinazocheza "kwa ku pack bus" kwa kuwa wanashindwa kutengeneza nafasi na kufunga magoli
Tatizo la United la kuwa na washambuliaji butu halijaisha, tatizo la kuwa na majeruhi bado lipo, tatizo la United kuwa na kiwango kibaya bado lipo lakini watu wanafanya makosa sana kuidharau United mbele ya Gunners wenye washambuliaji wazuri, midfield ya kawaida na beki isiyoridhisha.
Kuna watu watasubiri kesho tufungwe halafu waje wa quote huu Uzi, ninawaambia NO PROBLEM, ninawasubiri. Lakini kuweka kumbukumbu sawa Sijasema United ana 100% ya kushinda, ila ninampa asilimia kubwa ya kushinda