Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Timu ya ovyooo kupata kutokeaa...!!
 
Umefanana na mimi shabiki kindakindaki wa Chelsea nilikuwa napiga zangu zoezi tu sababu najua kabisa timu yangu ndiyo inajengwa upya so nilishajiandaa na lolote kuliko hawa ndugu zangu wanaojitesa bure tu hapa
Hahaha,mkuu mbona timu yako ni nzuri tu, uhakika wa kumaliza juu ya MUFC upo. Una wachezaji wa kazi na sio mabishoo tulionao sisi.
 
Tusiposhuka daraja basi shetan la united linafanya kazi maana mech za away huyu bwana mdogo hana ujanja nazo kabisa yaani
Hahaaa...we Jamaa ulivyokuwa unateseka na Mourinho sikupatii picha kabisa kuwa sasa hivi uko ktk hali gani kwa hasira
 
Wewe unajua mwanangu
 
Hahaha,mkuu mbona timu yako ni nzuri tu, uhakika wa kumaliza juu ya MUFC upo. Una wachezaji wa kazi na sio mabishoo tulionao sisi.
Lakini bado hawajawa na consistency ya uhakika kama Man City au Liverpool, so sikuwa na haja ya kujipa presha niliona ni vyema nikapunguze sumu kwa mazoezi
 
Unamaanisha kocha wa namna gani, maana tulikuwa na LVG
Kufeli kwa LVG haimanishi makocha wengine pia watafeli. Hata hivyo LVG, alikuwa Old school, kuna makocha wazuri wanafundisha modern football, kama

Ten Hag
Jardim
Kuna yule aliyeko RB leipzig, Naingelsman
Hata Allegri sio mbaya
Luis enrique.

Atleast hao wameprove wanaweza kusuka kikosi na kikacheza mpira unaeleweka na kucompete kwenye top level,

Napenda sana OLE afanikiwe tena afanikiwe akiwa kocha wa Man u. But........
 
MkuuDaemusin Ole alikosea sana kuamini kuwa kikosi chake kingeweza kumpa matokeo ya kufikia malengo aliyojiwekea ya top four hili lilikuwa kosa kubwa sana.

Epl ni ligi yenye ushindani mkubwa sana team hizi ndogo hutengeneza nafasi chache sana za kufunga lakini huzitumia effectively wakipata mbili moja lazima wafunge hiki kitu kitamtesa sana Ole.

Team nyingi za epl sasa hivi zinaifahamu Man u ni dhaifu kwenye idara ya ushambuliaji hivyo zinacheza bila pressure ya kuadhibiwa.

Naona Ole akipoteza mechi nyingi sana msimu huu kama Woodward ataendelea kumvumilia mpaka Christmas.
 
Nachokiona Ole ni mwanafunzi wa Ferguson lakini ana ubongo wa Arsene Wenger
 
Nachokiona Ole ni mwanafunzi wa Ferguson lakini ana ubongo wa Arsene Wenger
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…