Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Welcome to the gang! I can imagine what it feels like. We at LFC have said this for 29 years now. ManUtd fans had a good laugh at us. And now, for 7 yrs we seem to be in the same boat. Our 29 was aslo 7 once, you'll find out soon.

Have a good luck
 
Hizi mech 2 mfululizo anazocheza Chelsea na hawa waliopanda daraja zisikudanganyeni mkaona mna timu,

Nilishawafanyia uchambuzi makini ,ikaonekana mtamaliza nafas ya 10,

Astonvilla kasajiri kuliko wenzake , ana wachezaji wazuri ,sina hakika kama kwa villa atashinda kirahis ikiwa Norwich & shefflied wanamuhenyesha , niliwaambia mtachukua point 4-6 kwa hawa wawili ,ila wolves ,Leicester , Everton, Watford , westaham ,mtagawana point au mpigwe,

Top 6 sion mtakayemfunga .
Usinihusishe na genge la watoto wa Lampard. Mimi ni mhenga wa namba 5-7 tokea msimu wa 2014/15 kasoro msimu wa 2017/18 nilipokamata nafasi ya 2. By the way, mpaka sasa wapo 2 - 2(Chelsea Vs Sheffield United).
 
Rashford sio mshambuliaji wa kutegemea mkuu,mimi nilikuwa nadhani labda Ole ameuza Lukaku bila kusajili akimtegemea hata Sanchez, kumbe tegemeo lake ni Martial na Rashford

Huyo Rashford msimu huu anaweza kuzidiwa magoli hata na dogo James, Rashford amekuzwa sana inafika muda anajiona kama Ronaldo vile. Ni mchezaji wa kawaida sana. Hana uhakika wa namba katika timu nyingi sana katika EPL. Ila kinachombaba ni uingereza wake.
hamna kitu na kichwa chake kama mchele uyo
 
Apo sawa lakini ukweli ni kwamba Chelsea tuna vijana ambao wanaingia moja kwa moja tena bila kupingwa kwenye first XI ya Ole ...

Mcheki Mount, ata Rashid anapigwa bench apa jpo yeye ana uzoefu na ligi.

Mcheki Kova apo ata Pogba anaeza pigwa benchi.

Mcheki Tammy ..Marshal apa anaeza kaa bench

Kwa upande Beki muko vizuri ..ila Magwaya anakalishwa vizuri tu na Zouma

Apo kati ndo usiseme Joghihno, Kante nani wa kuwaweka benchi apo Man u? Jibu ni hatuna..

Kepa anaeza mkompiti vizuri tu De gea na soon anachukua kipa namba moja Uspain..

Kila la kheri Chelsea
Mkuu kuna taarifa zimenifikia hapa. Inasemekana yule beki wetu maridadi mwenye kiwango cha kumuweka Harry bench amemtandika Kepa booonge la goli.

Zouma moja
Maguire hajapata kitu.
 
Niliwahi sema humu Man United iuze wachezaji wote ila si Herrera na Lukaku.

Ole akunisikiliza nikamwambia tena uza uyo Pogba Nununua Verrat wa psg akunisikiliza.

Kwenye dimba angesimama Matic na Herrera, Verrati anasogea mbele hawa watu wawili Herrera na Verrat wanauwezo waku offer vitu vingi zaidi ya Pogba kwanza wanakaba wanauwezo wa kupiga pasi za mwisho, kufungua pia wanaweza.

Nilimuandikia tweets akupuuzia, nikamuandikia email akapuuzia basi matokeo yake ndio haya.
 
Niliwahi sema humu Man United iuze wachezaji wote ila si Herrera na Lukaku.

Ole akunisikiliza nikamwambia tena uza uyo Pogba Nununua Verrat wa psg akunisikiliza.

Kwenye dimba angesimama Matic na Herrera, Verrati anasogea mbele hawa watu wawili Herrera na Verrat wanauwezo waku offer vitu vingi zaidi ya Pogba kwanza wanakaba wanauwezo wa kupiga pasi za mwisho, kufungua pia wanaweza.

Nilimuandikia tweets akupuuzia, nikamuandikia email akapuuzia basi matokeo yake ndio haya.
utabaki kuwa shabiki daima
 
Tumeshacheza mechi 4 kati ya 38 tayari Man City wameshatuzidi point 5 ,Kama Liverpool akishinda atakuwa ametuzidi pointi 7,Imagine baada ya mechi 38 tutakuwa tumezidiwa pointi ngapi ?
Kama mwendo utakuwa hivi, mwisho wa msimu tutapoteza au kudraw zaidi ya mechi 19.
 
Formation imebuma, bado anaendelea kuitumia.

Unampango wa kuuza wachezaji, hununui wachezaji.

Unategemea uchukue ubingwa na Rashford.
 
Back
Top Bottom