Nina uhakika Lingard kwa sasa anakula bakora nyingi kwa kuwa timu haipati matokeo mazuri
Nina uhakika timu ikijakupata matokea Lingard ataonekana kama Iniesta wa Man Utd
Na kupata matokeo mazuri yanasababishwa na timu nzima kucheza vizuri
Nina uhakika Man City ingekuwa haipati matokeo kuna wachezaji tungewaona wa kawaida sana (akina Zichenko, akina Otamendi, akina Rodri labda abadilike mbele ya safari)
Kwa sasa kuna vitu naona Lingard inabidi aongeze ili a improve game yake, lakini haimaanishi ni mbovu kama watu wanavyomsemasema
Nina uhakika matokeo ya mechi zilizopita yametu dis appoint sana, lakini pia nina uhakika kuna mambo madogo madogo ambayo yangetokea/yasingetokea kwenye mechi zilizopita hasa ya Cristal Palace leo hii tungekuwa tunaongea mengine
Martial kuangushwa na Garry Cahil kwenye penalt box, ingetolewa penati na Garry Cahil angepewa kadi ya pili ya njano sidhani kama matokeo yangekuwa yale tuliyopata
Rashford kukosa penalt. Ni jambo linalotokea kwenye soka mchezaji kukosa penalt lakini ni nafasi rahisi ya kufunga kuliko nafasi nyingine yoyote uwanjani hivyo Rashford angetumia nafasi ile leo tungeongea mambo mengine
Martial kuumia dakika za mwishoni na kufanya United inayohitaji goli la kuongeza kubaki na watu 9 uwanjani
Kuna watu watasema ndio mpira ulivyo, nakubaliana nao. Lakini kwa mechi iliyopita ni kwamba hatukuwa na bahati na si kuzidiwa kiwango