Tusishangae tukapata mshangazo wa Patrice Evra kupewa hiki kiti, sidhani kama ile kuonekana na ed woodward kila game wako pamoja ilikua ni kwa ajili ya kuangalia mpira tuu, nadhani Evra kuna nafasi anatafutiwa pale OT, na huenda ikawa ndio hii,
Ikumbukwe SAF kabla hajastaafu alimsifia sana Evra kuwa anajua kuongoza wengine na alimtabiria kuwa kocha mzuri baadae kama akiamua kuwa kocha kuliko giggs, akasema giggs ni mkimya sana, kocha anahitaji mtu aliechangamka kidogo,
Pia, nilikuwa nasoma makala moja jana,
Wakasema, lengo la kumrudisha OGS, ilikua ni kuirudisha utd katika njia zake, ndio maana akarudi OGS, akarudishwa na Mike Phelan, na SAF amesogea karibu na timu kuliko nyakati zote tangu alivyostaafu,
Inasemekana nafasi ya director of football position inaenda kushikwa na SAF mwenyewe kupitia kioo cha mtu mwingine anaeifahamu united, ndio maana hapa mtu kama Evra anaingia kwenye picha.
Sent using
Jamii Forums mobile app