Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

umenikumbusha mbali sana, hivi yule fala belotti amepotelea wapi?

niliangalia video yake mara moja tu nikawaambia mashabiki wa chelsea munakwenda kununua kenge, jamaa anajua kutumia kichwa tu kama nyoka
Upo sahihi aisee, mm nilimuangalia nikasema atakayemchukua anaenda kula hasara.

Lakin Chelsea kwa tamaa zao wakaangukia kwa kilema morata

'When you’ve been an Arsenal fan as a kid, you will be one your whole life in some way.” David Alaba
 
tamaa ziliwaponza torino pamoja na wakala wake, nimeangalia rekodi yake msimu huu ameshafunga magoli 10 SERIE A.
kutoka kutakiwa na chelsea kwa paundi millioni 60 hadi kutakiwa na west ham.
kweli hakuna aijuae kesho yake itakuwaje.​
Perez alifika Euro 100 milioni akapigwa chini na bosi wa Torino msimu uliyofata kila mtu anayo habari yake
 
LONDON, ENGLAND
OLE Gunnar Solskjaer ametimiza lengo lake la kwanza kwa kuinasa ajira ya kudumu ya ukocha wa Manchester United, lakini mengi ya kufanya yanamsubiri Mnorway huyo, yakianza na kuwakaribisha Watford Old Trafford Jumamosi hii.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka
46 ndiyo aliyekuwa chaguo la wengi katika kurithi kiti kilichoachwa na Jose Mourinho baada ya kuwa na mwanzo mzuri madarakani kama kocha wa muda katika kipindi ambacho United walishinda mechi 14 katika mechi 19 alizoiongoza timu.
Hapa tunaangalia nini kinafuata na mitihani inayomsubiri
Solskjaer.
Kumaliza Top-4
Tangu kuwasili kwa Solskjaer, United imepunguza pengo la pointi kati yake na timu za Top 4 kwenye msimamo wa Ligi Kuu hadi kufikia pointi mbili, lakini kumaliza vyema kunahitaji ili kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Wakiifunga Watford Old Trafford, United watakuwa pointi sana na timu inayoshika nafasi ya tatu Spurs, ambao wameambulia pointi moja tu kutoka kati mechi zao nne zilizopita za ligi na wanasafiri kwenda kuivaa timu inayofukuzia ubingwa ya Liverpool Jumapili hii.
"Sasa tumejipa nafasi nzuri ya kukaa katika Top 4, au hata Top 3," alisema Solskjaer Alhamisi. "Hilo ndilo lengo letu la muda mfupi."
Kuimarisha kikosi
Bila ya kujali kwamba United wako katika Ligi ya Mabingwa ama Ligi ya Europa msimu ujao, Solskjaer anakabiliwa na mtihani mkubwa wa kuijenga upya timu hiyo.
"Sasa ni rahisi kutambua tunachokitaka kwa sababu tutaingia sokoni katika dirisha la usajili linalokuja," alisema Ole.
Kinda mwenye kipaji wa England, Jadon Sancho wa Borussia Dortmund amekuwa akitajwa kama mchezaji chaguo la kwanza anayewindwa kwa dau litakaloweka rekodi ya uhamisho kwa klabu hiyo, lakini ni kwenye eneo la ulinzi ambako mchezaji mwenzake wa zamani Solskjaer na nahodha wa zamani wa United, Gary Neville, anaamini ndilo linalohitaji mabadiliko makubwa.
"Ulinzi ndiyo eneo namba moja nikimaanisha kupata pacha sahihi ya mabeki wa kati kwa sababu kumekuwa na mabadiliko mengi," aliiambia Sky Sports.
"Solskjaer hawezi kupata mafanikio Man United isipokuwa kama atapata watu sahihi wa kumzunguka katika usajili na kupata wachezaji sahihi. Hilo ndilo muhimu kabisa."
Sanchez tupa kule?
Kutakiwa kwa Sancho kunachochea shaka katika hatima ya Alexis Sanchez.
Mshambuliaji huyo wa Chile alikuwa mchezaji anayelupwa pesa nyinmgi Zaidi klabuni hapo aliposajiliwa Januari 2018, lakini amefunga magoli matano tu United, na mawili tu kati ya hayo ameyafunga katika mechi 23 zilizopita msimu huu.
Solskjaer alipata kusema kuwa ni Sanchez mwenyewe tu anayeweza kurejesha kiwango alichokionyesha Arsenal na Barcelona lakini kwa aumri wake wa miaka 30 zama zake bora zimeshampita.
Isipokuwa kama Ole ataweza kufufua kiwango cha Sanchez, United watalazimika kupunguza mzigo wa mshahara wake wa mwaka unaosemekana kuwa ni Pauni 14 milioni kwa kumuuza.
De Gea pasua kichwa
Dili la Sanchez siyo tu linaleta shida kutokana na kiwango chake kibovu, bali pia linafanya bajeti ya mshahara United kuwa kubwa sana.
Mkataba wa David de Gea unamalizika 2020 na kipa huyo wa Mhispaniola, ambaye amshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu wa United mara nne katika misimu mitano iliyopita, ameripotiwa kutaka alipwe mshahara sawa na wa Sanchez.
Katika kipindi cha klabu kuyumba chini ya makocha watatu waliopita, De Gea alikuwa ni kati ya wachache waliokuwa waking’aa na kubakisha moja ya vipaji vyao vya kiwango cha dunia ni jambo muhimu sana.
"Kujua nani kocha wa klabu msimu ujao inasaidia kuamua wapi anataka kucheza," alisema Solskjaer.
"Tuna wachezaji wengi tuko katika mazungumzo nao na natumai watasaini mikataba mipya."
Vita kali ya utawala baina ya mahasimu
Mbio za ubingwa zinachukuliwa kama ndiyo maisha kwa mashabiki wa United kihistoria na mahasimu wa jadi Liverpool na Manchester City wameingia kwa kishindo.
Solskjaer ameweka lengo kuu kwamba ni kumaliza ukame wa makombe uliotawala tangu Alex Ferguson alipostaafu 2013 lakini pia ni lazima akubali ukweli kwamba tofauti kati yake na wapinzani wake hao kubwa.
"Kuna kazi kubwa bado ya kufanya katika miezi na miaka ijayo kuirejesha Man United kule ilikokuwa zamani," alionya Neville.
 
Leaked jezi msimu ujao

Man-Utd-1598911.jpg
 
Back
Top Bottom