Mkuu we ni balaa,,,
Jamaa kaandika yoote hayo af wew unaandika reply fupi hivyo!
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu we ni balaa,,,
Lakin utambue man u hawez kucheza kati au kutawala hasa kwa timu kama Barcelona,Bro mawazo mazuri.. Pia kwa taarifa zilizopo ni kwamba kuna percent kubwa dembele hatocheza..ila kwa upande wetu kikosi tutakacho kipanga ni sahihi kupambana na barca??.. Sioni sehemu ya matic kucheza ningependa
Herrera+perreira+fred/pogba yani tujiadhari kwa chochote.. Ila pia ole naamini atapanga Herrera+matic+pogba ambako sio sahihi kabisa..tukijitaidi kumkaba messi ambaye siku izi namuona kama ndo play maker wao mkubwa naamini tutaweza..
Nmeona nae messi anamsifia scott mctominay..ila nngependa tuwe na pure defensive mid wawili na mmoja acheze kma central at the same time.. Pia kma ni pogba acheze kma attacking and also akae kma CMD pia.. Tukijitaidi kuperform vizuri kati naamini tunawaweza kabisa
Sent using Jamii Forums mobile app




*Et wanasoka wenzangu*
Hiv pique anaweza riadha na rash ford?
Ter stegen atadaka chambua za martial?
Kale ka jordi alba kanaweza fukuzana na lingard?
Arthur melo amsumbue pogba,Kweli jaman?...
Alishndwa mbape ataweza Suarez kweli kwa lindelof?
Coutinho anataka kuja man u ,amfunge de gea si atakua anataka kurud brazil huyo?
Mfupa ulomshnda ronaldo makundi atauweza messi kweli?
Balaa la matic, bosquet kibabu analijua kweli?
Shaw on fire,kuna mbugira atapita kweli pale?...
Form ya ole ,yule kocha wa barca ataingia hata kdogo jaman!
*Et wana man u wenzangu ,uefa kwa nn wametupa tmu dhaifu HVO?*
Sent using Jamii Forums mobile app
Mm nashabikia Man city, kwann unataka nitafute mchezo mwingine, inamaa wewe ndo upo sahihi tu huwezi kosolewa. umekosea sasa unataka nikubali tu unachosema, mbona humu jamvin watu wanaeleweshana na wapo wanaokosea ila wanaelewana tu. ila sorry kama hupendi kukosolewa. kuna watu huwa hawapendi kukosolewa wanakuwa wakali mpaka wanasema asietaka na aondoke, ukimkosoa atasema sipangiwi.Wewe naona unataka nipotezea muda tu...Kama mpka sahv huelewi maana ya kibonde bac tafuta mchezo mwingine ushabikie
Wewe ndo ulietusemea kwamba sisi tulikuwa tumejiandaa kisaikolojia blaa blaa...lakini sisi Utd utamaduni wetu ni kuwa kila game tunayotia mguu tunajua tunaenda kushinda, kama ikitokea vinginevyo sawa, lkn mentality yetu siku zote tunajua kila game tunaenda kushinda!!Huu ndo ushujaa mkuu,Hata kama unajua mechi Fulani huwezi kushinda unajitapa kuwa unashinda ndo football hiyo
upo sahihi sana brother tunahitajika kumtafuta DIRECTOR OF FOOTBALL kama walivyofanya wapinzani wetu wakubwa barani ulaya kwa haraka, tatizo kubwa nililoliona mimi baada ya kuondoka sir alex ferguson ni kwamba klabu nayo iliamua kuivunja misingi yote ilioanzishwa na ferguson kwa miaka takribani 25, kazi aliyokuwa anaifanya ferguson ilipelekea klabu isione umuhimu wa kutafuta DOF ndio maana utamaduni wa kuajiri DOF ulikuwa ni mgeni ndani ya klabu japkuwa klabu nyengine kama barcelona, juventus, sevilla walishakuwa na utamaduni huu.Duuh aisee kweli kuna watu wapo deep humu nimefurahi sana kusoma hoja zako humu mkuu sababu mawazo yako yanendana
sana na ninachofikiria mimi...kwa ufupi tunachokosa kikubwa kwenye hii club ni "Director of Football" kwenye modern football
sahiv hyu mtu lazima uwe nae mfano City yupo,Juve Yupo,Barca Yupo, Atletico yupo etc Club kubwa karibia zote, hyu mtu kazi
yake ni kuangalia Coach anataka acheze vipi na wachezaji watakaofaa kwenye huo mfumo ni wapi na kwenda sokoni kuwa
nunua, ukiangalia tunavyofanya usajili sisi nikama hatujui tunahitaji nini na ndo maana mwisho wa siku tunaishia kununua
wachezaji wengine level za chini mfano wakina Darmian na kuendelea kuwaongeza mikataba wakina Jones,wachezaji wa
maana kama kina De jong wanaishia kwenda Barca, Ed woodward ni Banker mwanauchumi sio DoF hana uelewa wa ndani wa
mpira hvyo hana uwezo wowote wa kumpinga Coach na haelewi club inahitaji nn,mfano Moyes alivyoomba Fellaini anunuliwe na
yye akaenda kumnunua tena kwa bei mbaya,hzi timu kama Juve na City wamefanikiwa kufanya usajili mzuri ndani na kipindi
kifupi sababu ya DoF hvyo naona nasisi inabidi tufanye michakato aje mtu wa maana pale kama Dof na nimeshasikia Club
inamtafuta mtu atakae fit hyo nafasi vizuri.
Mkuu umeeleza vzr sana , hakika upo deep, kwasasa bila DOF timu itakuwa inayumba na sokon unajikuta unauziwa magarasa au wachezaj wazur ila hawaendan na mfumoupo sahihi sana brother tunahitajika kumtafuta DIRECTOR OF FOOTBALL kama walivyofanya wapinzani wetu wakubwa barani ulaya kwa haraka, tatizo kubwa nililoliona mimi baada ya kuondoka sir alex ferguson ni kwamba klabu nayo iliamua kuivunja misingi yote ilioanzishwa na ferguson kwa miaka takribani 25, kazi aliyokuwa anaifanya ferguson ilipelekea klabu isione umuhimu wa kutafuta DOF ndio maana utamaduni wa kuajiri DOF ulikuwa ni mgeni ndani ya klabu japkuwa klabu nyengine kama barcelona, juventus, sevilla walishakuwa na utamaduni huu.
kuanzia david moyes hadi jose mourinho ukiangalia sajili nyingi zilizokuwa zikifanywa zilitokana zaidi na vipaombele vya mwalimu na si falsafa ya timu ndio maana tumeshuhudia ndani ya klabu yetu tumejaza wachezaji wenye kuendana na falsafa ya manchester united na wale wasioendana falsafa.
waangalie manchester city tokea wamlete Txiki Begiristain, Ferran Soriano. na josep guardiola wamekuwa wakifanya biashara ya usajili kwa kuangalia zaidi mchezaji atakayeendana zaidi na falsafa ya timu kiuchezaji na kwa ushahidi wa hilo jaribu kurejea sajili za danilo, walker, sterling, bernardo silva, ederson, jesus, sane, gundogan hawa wote wana uwezo wa kucheza soka linalofundishwa na guardiola, hata ukiangalia umri wa wachezaji wao wanaowasajili wengi wao wana wastani wa miaka 22- 26.
hivyo basi hata kama itatokezea siku moja josep guardiola ataondoka manchester city kikubwa watakachokifanya ni kutafuta mwalimu atakayeendeleza falsafa ilioasisiwa.
lakini ukija kwetu mambo ni tofauti kuanzia sajili za makocha, sajili za wachezaji na mifumo ya makocha wote waliokuja wametelekeza misingi yetu.
director of football anafanya kazi tofauti kutegemeana na mahitaji ya klabu husika kwa mfano wanahusika zaidi na ishu za negotiations kwenye usajili wa wachezaji hivyo basi inategemea zaidi na mahitaji ya klabu ya manchester united, lakini mwisho wa siku mwenye maamuzi ya kutafuta wachezaji anaowahitaji kwenye timu ni kocha na benchi lake la ufundi, ina maana director anapaswa kufanya kazi kwa ukaribu na kocha mkuu huku akipeleka repoti kwa CEO ambaye ni ED WOODWARD.
- alipokuja david moyes kosa kubwa la kiufundi walilofanya manchester united ni kumruhusu atelekeze benchi lote la ufundi aliloliacha ferguson, hii ilikuwa ni dalili ya kwanza ilio dhahiri yenye kuonyesha anguko la klabu kiutamaduni, haitoshi klabu ikaruhusu usajili wa marouanne fellaini ambaye haendani kabisa na mfumo wetu wa kiuchezaji, barcelona wasingeliruhusu upumbavu huu aliotufanyia moyes japokuwa na wao wameanza kupoteza muelekeo kwenye usajili.
- kituko chengine ni ujio wa LVG na falsafa yake ya 3-5-2 na kumiliki mpira kwingi bila ya mipango, mpaka unafika nyakati unajiuliza tokea lini manchester united na kumiliki mpira kwa muda mrefu bila ya kufika golini?. Usajili wake pia ulikuwa ni wa ajabu ajabu ndio maana wachezaji wake wengi waliishia kufeli.
- alipokuja jose mourinho kama ni wafuatiliaji wazuri wa mahojiano yake utagundua ya kwamba jamaa alitaka klabu iachane rasmi na tamaduni yake ya matumizi, jose alitaka tuwe kama manchester city, madrid ya zamani au psg kwenye market. Alivyokuwa anataka yeye ni kwamba kama itatokezea amesajili mchezaji halafu akashindwa kuendana na matarajio yake basi atafutiwe mwengine jambo ambalo ed woodward hakuvutiwa nalo. Kiupande fulani mourinho madai yake yalikuwa ni ya msingi kwa mfano ishu ya winga wa kulia, kushoto pamoja na walinzi wa kati, lakini baadhi ya madai yake hayakuwa sahihi hususani mahojiano yake baada ya kufungwa na sevilla pale aliposema sevilla wana wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza kikosi cha kwanza cha man utd. Uwepo wa OGS unajaribu kutuonyesha madhaifu ya jose mourinho na wakati huo huo uwepo wake unajaribu kutuonyesha madai sahihi ya jose mourinho.
cha msingi ni kupata DOF mwenye uwezo wa kusaka wachezaji watakaoandikwa vizuri kwenye historia ya klabu siku za mbeleni na pia atakayekuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa ukaribu na benchi la ufundi kwa masikilizano pamoja na kushauriana juu ya mwenendo wa klabu, bila ya kusahau tupate wachezaji wanaoendana na modern game, ni bora kupata wachezaji wanaojituma lakini wawe na vipaji kuliko kuwa na wachezaji wanaojituma lakini wakakosa vipaji vya soka kama sajili zetu tulizozifanya miaka 6 iliopita.
Mwaka 2010 ndani ya klabu ya real madrid kulizuka mgogoro mkubwa wa kimaslahi kati ya jose mourinho na DOF jorge valdano. Kama kawaida yake mourinho alihitaji striker mpya wa kumuongezea nguvu na hili lilitokana na gonzalo higuain kupata majeruhi lakini pendezo lake lilikataliwa na jorge valdano, wawili hao wakawa hawazungumzi kwa muda mrefu na mwishoni hatimaye madrid wakafanya maamuzi ya kumuondoa JORGE VALDANO, ni matumaini yangu tatizo hili halitajitokeza ndani ya manchester united.
Tatizo kubwa ambalo pia naliona kwa sasa ni kwamba bado hatujamfahamu ole gunnar solskajer kwenye soko la usajili kiundani zaidi, hatujui kama OGS ni asset kama walivyo makocha wengineo mfano guardiola, jose mourinho au jamaa ni liabilities kama alivyokuwa LVG na david moyes. Kama jamaa atakuwa ni hodari kwenye kutafuta wachezaji wanaoendana na ubora tunaouhitaji basi ushirikiano wake na DOF utakuwa ni wa mafanikio makubwa sana lakini kama itakuwa ni kinyume chake basi tujiandae kisaikolojia kutafuta mwalimu ajaye dirisha lijalo la usajili pamoja na DOF mpya.
- kuandaa mipango imara ya uendeshaji wa klabu kuanzia academy kwa kuweka kipaombele cha umri kwa wachezaji tunaowatafuta, kama tungelikuwa makini miaka iliopita hatukupaswa kuruhusu dili la rafael kwa darmian, falcao kwa chicharito, cleverley kwa schneiderlin na schwensteiger.
- kuhakikisha utamaduni wa klabu unafuatwa vilivyo na makocha waliopo hususani linapokuja suala la usajili wa wachezaji, barcelona wamewasajili arthur melo, de jong ni kwa sababu wanaendana na utamaduni wao lakini ukija kwetu ni tofauti, tunacheza counter attack lakini usajili tunaoufanya ni wa marouanne fellaini na juan mata.
- DOF anapaswa kuwa ni daraja kati ya viongozi wa klabu na kocha mkuu na si kinyume chake, kama DOF atakuwa ni paka wa familia ya glazer itakuwa ni kazi bure.
- awe ni mtaalamu kwenye sekta ya usajili na kusaka vipaji ili kuepusha tena kuuziwa wachezaji kwa bei za gharama, mfano usajili wa fred kutoka shakhtar donetsk.
- masikilizano na kushauriana ndio msingi wa mafanikio.
wiki mbili zilizopita niliona habari ya arsenal kumuhitaji monchi awe DOF ili afanye tena kazi na unai emery.
leo hii nimeona taarifa ya sevilla wanahitaji kumrudisha monchi ndani ya klabu yao.
kama namuona monchi muda huu anavyotikisa gilasi yake ya wine.
View attachment 1046928
The Spanish club’s president Jose Castro said: "We're looking for the best Sporting Director, and that is Monchi.
“We have begun negotiations and we want to reach an agreement soon. Our conversations go very well with him. We hope to reach an agreement soon.”
Lakin utambue man u hawez kucheza kati au kutawala hasa kwa timu kama Barcelona,
Man u miaka yote kwa timu zinazopossess huwa hachez mpira wa katikati, zaid huwa anatumia counter attack akitumia zaid winger za kulia na kushoto ,
Na hiyo ndio njia pekee ya man u kupata matokeo ,
Na kitu kingine kitakachowaponza ni kumkabidhi MTU amkabe au atembee na messi, hiyo itawaletea madhara makubwa ,kwanza sio rahis kumkaba,pili mtaacha nafas kwa wengine waadhibu,
Kama umemsikiliza mou anasema njia ya kuwadhibiti barca ni kuziba mianya yao ya mipira ,huku mkicheza counter, hapo alikuwa anazungumzia jinsi inter ilivyoidhibit barca kipind chake
Sent using Jamii Forums mobile app
Poor you kila ukielezea tukio unamtaja Messi tu kwani anachezaje pekeake..... Ngojeni muone nini kitawakuta then huyo Messi can be injured too....Nilitaka hivi vijamaa, nyinyi nyumbani napiga 3+ , ugenini napiga 4+. Eti Smalliñg atamkabà Messi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nikupongeze kwa analysis nzuri,sina uelewa mkubwa sana wa masuala ya mpira hususani kwenye tactics kama wengineo lakini miaka yangu yote tokea niifahamu manchester united nikiri ya kwamba manchester united hatujawahi kuwa bora kwenye kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa sana kama timu nyengine mfano zile zinazotoka Hispania, Germany (bayern munich).
kama nitakuwa nipo sahihi manchester united ndio timu kubwa pekee ambayo bado imeshikilia falsafa za kiingereza huku timu nyengine mfano liverpool na man city wameshaachana kitambo na mpira wa kiingereza wa kuziba nafasi nyeti kwenye maeneo ya hatari (Space Oriented Zonal Marking). Ni mfumo ambao nimeushuhudia kwa miaka yangu yote ya kuishabikia manchester united tokea mwaka 2001 ukitupa faida kubwa sana hususani tunapokutana na timu zenye uwezo mdogo sana wa kumiliki mpira kama zilivyo timu za uingereza lakini tunapokutana na timu zinazo dominate possession na counter pressing tunapata tabu sana na kwa ushahidi wa hilo jni pale tunapokutana na timu za spain na hata timu ya taifa ya uingereza bado ni waumini wa style hii ya kiuchezaji.
Ili uweze kudominate possession mara kwa mara unapaswa kwanza umdhibiti adui kwenye eneo lake la kujidai kitu ambacho manchester united hatufanyi mara kwa mara labda tuwe kwenye situation ya kutafuta magoli kama ilivyokuwa kwenye mechi yetu ya southampton au kuna mechi fulani mwaka 2008 tulikwenda half time tukiwa nyuma kwa magoli mawili dhidi ya spurs ya darren bent, lennon, pavlyuchenko n.k, ukija upande wa wapinzani wetu wakubwa kama liverpool na manchester city wao wanaanzia kukaba juu ndio maana ukiangalia mechi zao unakuta eneo la kati kati wapo wengi hivyo basi inakuwa ni vigumu kwa timu pinzani kufika maeneno yao ya hatari na hata wanapopoteza mpira wanarudi kwenye maeneo yao kwa haraka sana, ndio maana mechi ya guardiola na klopp inakuwa ni ngumu sana kwa pande zote mbili.
kama hatuwezi kuachana na utamaduni wetu wa soka la kuziba maeneo yetu ya kujidai basi atleast wachezaji wetu wanapaswa wabadilike kifikra na kiuchezaji ndipo baadae tuelezekeze shutuma kwa kocha na benchi lake la ufundi, msingi mkuu wa kuhakikisha timu inakuwa na umiliki mzuri wa mpira unapaswa uanzie eneo la ulinzi ndio maana guardiola alipotaka kuingiza falsafa yake ndani ya manchester city alianza kurekebisha eneo la ulinzi hivyo basi na sisi tunapaswa kuliangalia kwa jicho la tatu eneo letu la ulinzi kwa kuanzia golikipa.
Tuna golikipa mzuri sana linapokuja suala la kuokoa michomo ya magoli lakini ukigeuza sarafu utagundua ya kwamba kwa timu kubwa za uingereza (man city, liverpool, chelsea) sisi ndio tuna golikipa muoga wa kucheza ukilinganisha na hao niliowataja. mipira mingi anayoianzisha david de gea ni ile ambayo yupo kwenye presha ndogo sana, pengine safu yetu ya ulinzi ndiyo inamfanya david awe mzito wa kuanzisha mipira mara kwa mara bila ya kuwa na khofu yoyote. ukiwaangalia makipa kama ederson, allison, ter stegen, buffon, arrizabalaga, manuel neur wote hawa wanazidiwa na david degea kwenye saving lakini wanamzidi kwenye kucheza.
Josep guadiola hakumuondoa joe hart kwa sababu ni mbovu bali alimuondoa kwa sababu hii ya kutokuwa na uwezo wa kucheza hivyo basi david degea anapaswa aende na wakati kama wenzake. ukiangalia ukuta wa juventus nyakati zile ulikuwa unaundwa na walinzi wasiokuwa na degree yoyote ya skills mfano chiellini, barzagli, bonucci, lichsteiner lakini cha ajabu unamkuta buffon anaanzisha mipira hata kama adui yupo karibu.
smalling, young, jones, darmian:utawezaje kumiliki mpira kwa kiwango cha 60 - 70% kila mechi ikiwa mchezaji wako wa kikosi cha kwanza ni ashley young ambaye kila mechi anayocheza lazima apoteze mipira kipumbavu zaidi ya mara 5 kwa kupiga long pass zisizo na uhakika na mara tano akiwa out of possession ya kuanziwa mipira kama wanavyofanya walinzi wengine mfano wa jordi alba, walker, robertson, pique n.k.
ndio maana nawapenda sana manchester city na sera zao za kuendesha timu kwa sababu kocha mpya anapokuja anapewa uhuru wa kufanya anachokihitaji tofauti na sisi, timu yetu imejaza wachezaji wazito wanaoshindwa kufanya maamuzi ya haraka hata kama wapo under pressure, ndio maana tunapokutana na timu bora mfano wa juventus, barcelona, liverpool, man city tunaishia kudhalilishwa kimpira japokuwa tunapata ushindi, wachezaji kama ashley young, smalling, jones hata kama utawapeleka barcelona hawezi kubadilika tena kimpira kwa sababu wao wenyewe hawataki kubadilika kiuchezaji.
unapomuangalia gerrard pique jinsi anavyojiamini halafu unamuangalia smalling utafikiri mmoja kati yao amezaliwa na miguu minne kumbe wote ni sawa kihuduma wanazopewa na klabu zao. Ili tuimprove kwenye kumiliki mpira ni lazima eneo letu la ulinzi liundwe na wachezaji mfano wa lindeloff, shaw na hata eric bailly linapokuja suala la ubunifu na si nguvu.
marcus rashford, mctominay, sanchez, martialkwa ufupi wachezaji wengi wa kiingereza tabia zao zinafanana kiuchezaji kwa sababu ni wazito wa kuomba mipira tofuti na ilivyokuwa kwa paul scholes nyakati zake vile vile ukiangalia timu yetu kwa sasa tuna wachezaji takribani 6 ambao viwango vyao vinategemea na jinsi wanavyoamka.
kiukweli napenda sana kumuona rashford akifanikiwa kwa sababu ametoka kwenye damu ya manchester united lakini baadhi ya nyakati haeleweki anapomiliki mpira anakuwa ovyo sana utafikiri uwanjani anacheza na mbuzi. mimi nadhani kwanza waingereza waache kumjaza sifa za kumuaminisha ya kwamba uwezo wake anaweza kumfikia ronaldo, kabla hajafikia level za ronaldo ajaribu kwanza kufikia level za andy cole mmoja kati ya washambuliaji waliokuwa wanakupa faida kubwa sana kwenye eneo la ushambuliaji hata kama hafungi magoli.
kama nilivyosema mwanzo hata nyakati za alex ferguson tulikuwa hatumiliki mpira kama manchester city ya guardiola au chelsea ya maurio sarri kwa sababu si utamaduni wetu, tulichokuwa tukikifanya ni kumiliki mpira kwa kiwango cha wastani huku tukishambulia kwa posession, kwa ufupi ulikuwa unafahamu ni wapi movement za kutengeneza magoli zinaanzia na wapi zitaishia ndio maana safu yetu ya ushambuliaji ilikuwa na uwezo wa kufunga na kutengenezeana magoli mengi kupitia maeneo tofauti ukilinganisha na nyakati hizi ambapo tunategemea zaidi miujiza ya upande wa kushoto.
lakini pia kama umiliki wa mpira ni muhimu sana basi nyakati za LVG tulikuwa tunamiliki mpira kwa kiwango kikubwa lakini hatukuwa na mipango imara ya kushambulia ndio maana si ajabu kukuta mechi nyingi tuliishia kutoa suluhu. jambo muhimu ni kuhakikisha tunapokuwa na mpira adui anapaswa kuwa na pressure kubwa ya kufungwa na si kuwa katika hali ya kumfanya adui arelax kama kilichotukuta kwenye mechi zetu dhidi ya juventus na PSG uwanjani kwetu.
ball possession ni muhimu sana lakini bila ya kuwa na mipango imara ya kutengeneza nafasi na kujilinda tutakuwa hatuna tofauti na manchester united ile ya LVG au arsenal ya wenger.
kwa hili la kuwa na possession ndogo kwenye mechi kubwa tumhukumu ole msimu ujao ndio itakuwa ni muda sahihi zaidi kuliko wakati huu ambao ameikuta timu bila ya kuongeza chochote.
Swansea anatupa kombe la FA leo